Askofu Bagonza: Kupoteza mtu ni kutunza amani lakini kulalamika kuwa mtu amepotea ni kuvuruga amani

Askofu Bagonza ulipinga ujenzi wa bwawa la mwl Nyerere kwa hiyo huna legitimacy yoyote ya kukaa unalitajataja
Watu wa CCM utawagundua tu,akili yao ni ndogo sana,hicho ndicho ulichokiona
 
Askofu Bagonza ulipinga ujenzi wa bwawa la mwl Nyerere kwa hiyo huna legitimacy yoyote ya kukaa unalitajataja

Wewe huna legitimacy wala right ya kumzuia mtu kutaja chochote.
 
Si bora huyo kuna yule askofu anaitwa sijui mamakula huwa anavaa kofia kama ganda la chungwa alafu anaivalia kisogoni

Wajinga wanaangalia mavazi ya mtu, wenye akili hawana muda na mavazi ya mtu, bali yale atendayo na kutamka, alimradi hayupo uchi..
 
Vaa chupi utembee nayo mtaani huku unaongea maneno ya busara
 
Wewe unaishi wapi? Mbona Mvaa chupi Jokate alionekana maneno yake ndipo akateuliwa kuwa DC na sasa ni boss huko kwenye chama cha mapendekezo
 
Leta picha yake akiwa amevaa chupi niione
 
Hizi habari zote zilianza na nyie! Msijitie uziwi bila sababu!

Wakati ule CUF ilipigwa vita vikali kwa kisingizio Cha kuchanganya dini na siasa!

Wakati ule WAISLAM wananyanyasika kupigwa na kufungwa kwa uonevu, mlikuwa mnasema magaidi wanaharibu amani! Hata kama walikuwa wanadai haki na usawa!

Leo unafunga mashairi yale yale ukiwa kwa kuwa wahusika wa tamthilia Yako ni tofauti!

Onjeni uchungu wa dawa yenu wenyewe, Kisha tukae chini tujitafakari kama taifa!
 
KUNA MAMBO HAYAKO SAWA

Kuna mambo yanayotuunganisha wote bila kujali itikadi, dini, jinsia, kabila, hali ya mtu kiuchumi, ufupi au urefu wa mtu kama mimi. Haya yote yanaunganishwa na neno HAKI au kwa Kijaluo JUSTICE.

Kuna mambo 10 hayako sawa kwa sababu:

1. Hivi sasa, Mtu anapozungumzia HAKI, anatazamwa yeye ni dini gani badala ya kusikiliza anaongea nini!

2. Mtu akiongelea HAKI anatazamwa ni wa chama gani badala ya kusikiliza anaongea nini?

3. Mtu akilalamika amepotelewa na nduguye, anaambiwa anavuruga amani.

4. Mbuzi akipotea anapatikana lakini mtu akipotea hapatikani.

5. Kupoteza mtu ni kutunza amani lakini kulalamika kuwa mtu amepotea ni kuvuruga amani.

6. Kutumia dini kueneza siasa ni dhambi lakini kutumia siasa kueneza dini ni sawa tu.

7. Kumsifu mtu akifanya vizuri inapendeza, lakini kumkosoa akikosea ni sawa na kumdai marehemu kabla hajazikwa.

8. Yaonekana kuna dini inayohubiri amani bila kuhubiri HAKI na kuna dini “inajifanya”kuhubiri HAKI bila kuhubiri amani. Mimba ya HAKI ni amani lakini AMANI bila HAKI ni tasa. HAKI na AMANI vyote ni tunu za taifa letu.

9. TUMEGAWANYIKA: Wapo wanaoona mtutu wa bunduki unavuruga amani. Na wapo wanaoona mtutu wa bunduki unatunza amani. Msuluhishi wa kweli anaitwa HAKI. Tunahitaji mradi wa kimkakati wa kujenga Bwawa la Haki ya kuzalisha Amani.

10. Rais ni wetu sote. Anaongoza wapenda HAKI na wapenda AMANI. Hatuna shaka na mahaba yake kwa AMANI. Wapenda HAKI wanasikia baridi. Tulimsikia akiapa kuongoza kwa HAKI. Bahati njema, HAKI ilimbeba. Akiibeba kama ilivyombeba, AMANI itafurika kama Bwawa la Mwalimu Nyerere. HAKI na AMANI vipeane busu.

Kiapo kinasema, “…Nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria, mila na desturi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila woga, bila upendeleo, huba wala chuki”.

Hekima ya Wajaluo: “Kuchelewa kwenda msalani, hakuzuii njaa kuuma”.

Anaandika Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza
 
Anaandika Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)

KUNA MAMBO HAYAKO SAWA

Kuna mambo yanayotuunganisha wote bila kujali itikadi, dini, jinsia, kabila, hali ya mtu kiuchumi, ufupi au urefu wa mtu kama mimi. Haya yote yanaunganishwa na neno HAKI au kwa Kijaluo JUSTICE.

Kuna mambo 10 hayako sawa kwa sababu:

1. Hivi sasa, Mtu anapozungumzia HAKI, anatazamwa yeye ni dini gani badala ya kusikiliza anaongea nini!

2. Mtu akiongelea HAKI anatazamwa ni wa chama gani badala ya kusikiliza anaongea nini?

3. Mtu akilalamika amepotelewa na nduguye, anaambiwa anavuruga amani.

4. Mbuzi akipotea anapatikana lakini mtu akipotea hapatikani.

5. Kupoteza mtu ni kutunza amani lakini kulalamika kuwa mtu amepotea ni kuvuruga amani.

6. Kutumia dini kueneza siasa ni dhambi lakini kutumia siasa kueneza dini ni sawa tu.

7. Kumsifu mtu akifanya vizuri inapendeza, lakini kumkosoa akikosea ni sawa na kumdai marehemu kabla hajazikwa.

8. Yaonekana kuna dini inayohubiri amani bila kuhubiri HAKI na kuna dini “inajifanya”kuhubiri HAKI bila kuhubiri amani. Mimba ya HAKI ni amani lakini AMANI bila HAKI ni tasa.

9. TUMEGAWANYIKA: Wapo wanaoona mtutu wa bunduki unavuruga amani. Na wapo wanaoona mtutu wa bunduki unatunza amani. Msuluhishi wa kweli anaitwa HAKI.

10. Rais ni wetu sote. Anaongoza wapenda HAKI na wapenda AMANI. Hatuna shaka na mahaba yake kwa AMANI. Wapenda HAKI wanasikia baridi. Tulimsikia akiapa kuongoza kwa HAKI. Bahati njema, HAKI ilimbeba. A
kiibeba kama ilivyombeba, AMANI itafurika kama Bwawa la Mwalimu Nyerere. HAKI na AMANI vipeane busu.

Hekima ya Wajaluo: Kuchelewa kwenda msalani, hakuzuii njaa kuuma.
View attachment 3289378
Yuko vizuri intellectually, socially he is hopeless. Kuunganisha nchi, socially he is hopeless kama Lissu, wengi chadema hayuko vizuri. Heche anaongea maisha, matatizo ya Watanzania kwa lugha wanayoielewa.

Huyu, Lissu, Mbowe Hatambui yoyote yaliyofanywa kuboresha mamilioni ya maisha ya Watanzania sababu aliefanya hayo hampendi, kuna vitu alikosea.

Wapo zaidi kiitikadi, kuliko kuunganisha Taifa kwa watanzania wote. Anahubiri kwa watu walewale asilimia ambayo tayari inamkubali. Hawezi kuwafikia Watanzania wengi, kupewa nchi. Wabadilishe mikakati yao.
 
Hekima ya Wajaluo: “Kuchelewa kwenda msalani, hakuzuii njaa kuuma”.📌🔨
 
Anaandika Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)

KUNA MAMBO HAYAKO SAWA

Kuna mambo yanayotuunganisha wote bila kujali itikadi, dini, jinsia, kabila, hali ya mtu kiuchumi, ufupi au urefu wa mtu kama mimi. Haya yote yanaunganishwa na neno HAKI au kwa Kijaluo JUSTICE.

Kuna mambo 10 hayako sawa kwa sababu:

1. Hivi sasa, Mtu anapozungumzia HAKI, anatazamwa yeye ni dini gani badala ya kusikiliza anaongea nini!

2. Mtu akiongelea HAKI anatazamwa ni wa chama gani badala ya kusikiliza anaongea nini?

3. Mtu akilalamika amepotelewa na nduguye, anaambiwa anavuruga amani.

4. Mbuzi akipotea anapatikana lakini mtu akipotea hapatikani.

5. Kupoteza mtu ni kutunza amani lakini kulalamika kuwa mtu amepotea ni kuvuruga amani.

6. Kutumia dini kueneza siasa ni dhambi lakini kutumia siasa kueneza dini ni sawa tu.

7. Kumsifu mtu akifanya vizuri inapendeza, lakini kumkosoa akikosea ni sawa na kumdai marehemu kabla hajazikwa.

8. Yaonekana kuna dini inayohubiri amani bila kuhubiri HAKI na kuna dini “inajifanya”kuhubiri HAKI bila kuhubiri amani. Mimba ya HAKI ni amani lakini AMANI bila HAKI ni tasa.

9. TUMEGAWANYIKA: Wapo wanaoona mtutu wa bunduki unavuruga amani. Na wapo wanaoona mtutu wa bunduki unatunza amani. Msuluhishi wa kweli anaitwa HAKI.

10. Rais ni wetu sote. Anaongoza wapenda HAKI na wapenda AMANI. Hatuna shaka na mahaba yake kwa AMANI. Wapenda HAKI wanasikia baridi. Tulimsikia akiapa kuongoza kwa HAKI. Bahati njema, HAKI ilimbeba. A
kiibeba kama ilivyombeba, AMANI itafurika kama Bwawa la Mwalimu Nyerere. HAKI na AMANI vipeane busu.

Hekima ya Wajaluo: Kuchelewa kwenda msalani, hakuzuii njaa kuuma.
View attachment 3289378
Very phylosophical, Akili kubwa hii...

Kuhubiri AMANI tu bila kuioanisha na HAKI na kujua kuwa AMANI ni tunda la HAKI, ni ulaghai, uchizi na usanii wa kijinga kuliko usanii wenyewe...!

Lakini kuna watu wanajiita "Mufti fulani" au "Shekhe fulani" lakini kiwatokacho midomoni mwao ni uharibifu mtupu..

Bi Chura Kiziwi a.k.a Bi Tozo a.k.a Chief Hangaya a.k.a Chawa mkuu a.k.a Bi Kizimkazi na watu wake huko CCM hawaelewi haya au wameamua tu kujifanya hamnazo...

CC: Tlaatlaah Lucas Mwashambwa Paul Makonda FaizaFoxy Samiaagain2025 MamaSamia2025 na chawa wengine waione hii na kuisoma kisha waelewe na wafanye yawapasayo kufanya...
 
akili kubwa kiaje hali ya kua kila uchaguzi wa askofu mkuu wa kanisa la KKKT yeye hunung'unikia mfumo wa uchaguzi na kuzira?

kwamba nyani haoni kundule right?
au ni rahisi sana kuona kipanzi kwenye jicho la mwingine na ikawa ngumu kuona boriti jichoni pako?🐒
 
Kirusi hiki cha mfumo hovyo wa ki - CCM wa utawala na uchaguzi si tu umeharibu nchi kiasi hiki tuonavyo....

Bali umeshaingia na kuathiri kila mahali i.e familia, taasisi za umma, za kidini na kuchafua kila kitu....

Kashfa/Scandal ya Tegeta Escrow Account mwaka 2013 iliyohusisha wuzi wa fedha za umma iliyofanywa na wanasiasa wachafu wa CCM, si tu ilishiia kwao bali waliingiza uchafu wao mpaka makanisani wakahonga maaskofu, wakahonga majaji na kuchafua kabisa taswira ya u - KRISTO na mfumo wa haki (justice system) hapa nchini...

Kama Askofu hulalamikia rafu ndani ya chaguzi ktk kanisa lake, basi tambua kuwa hizi ndizo athari hasi za mfumo mbovu wa kisiasa na utawala tuluonao hapa nchini kwetu kwa sbb umeingia kila mahali na kuchafua...

Na hii ndiyo maana kutaka REFORMS ili kusafisha uchafu kila mahali ktk nchi yetu...
 
Nimeyashangaa mashekhe ubwabwa nchi nzima yanaongea ujinga kisa tu yamepewa ubwabwa na Samia. Haya majitu hamnazo kabisa. Yanatokwa na akili kisa ubwabwa na ahad za kujengewa misikiti!!
Kwa kujua au kutokujua, hapa ndipo mnapofirika nyumbu. Ni hapa tu.
 
Anaandika Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)

KUNA MAMBO HAYAKO SAWA

Kuna mambo yanayotuunganisha wote bila kujali itikadi, dini, jinsia, kabila, hali ya mtu kiuchumi, ufupi au urefu wa mtu kama mimi. Haya yote yanaunganishwa na neno HAKI au kwa Kijaluo JUSTICE.

Kuna mambo 10 hayako sawa kwa sababu:

1. Hivi sasa, Mtu anapozungumzia HAKI, anatazamwa yeye ni dini gani badala ya kusikiliza anaongea nini!

2. Mtu akiongelea HAKI anatazamwa ni wa chama gani badala ya kusikiliza anaongea nini?

3. Mtu akilalamika amepotelewa na nduguye, anaambiwa anavuruga amani.

4. Mbuzi akipotea anapatikana lakini mtu akipotea hapatikani.

5. Kupoteza mtu ni kutunza amani lakini kulalamika kuwa mtu amepotea ni kuvuruga amani.

6. Kutumia dini kueneza siasa ni dhambi lakini kutumia siasa kueneza dini ni sawa tu.

7. Kumsifu mtu akifanya vizuri inapendeza, lakini kumkosoa akikosea ni sawa na kumdai marehemu kabla hajazikwa.

8. Yaonekana kuna dini inayohubiri amani bila kuhubiri HAKI na kuna dini “inajifanya”kuhubiri HAKI bila kuhubiri amani. Mimba ya HAKI ni amani lakini AMANI bila HAKI ni tasa.

9. TUMEGAWANYIKA: Wapo wanaoona mtutu wa bunduki unavuruga amani. Na wapo wanaoona mtutu wa bunduki unatunza amani. Msuluhishi wa kweli anaitwa HAKI.

10. Rais ni wetu sote. Anaongoza wapenda HAKI na wapenda AMANI. Hatuna shaka na mahaba yake kwa AMANI. Wapenda HAKI wanasikia baridi. Tulimsikia akiapa kuongoza kwa HAKI. Bahati njema, HAKI ilimbeba. A
kiibeba kama ilivyombeba, AMANI itafurika kama Bwawa la Mwalimu Nyerere. HAKI na AMANI vipeane busu.

Hekima ya Wajaluo: Kuchelewa kwenda msalani, hakuzuii njaa kuuma.
View attachment 3289378
Askofu umeupiga mpaka umemwagika.
 
Back
Top Bottom