Askofu Bagonza: Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA

Anaandika Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.

Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA. Inaonekana viliingia nchini tarehe 27/7/2020 kupitia jiji la DSM.

Madaktari wanadai dalili za LISSUPHOBIA ni hizi:
1. Hofu ya vyombo vya habari
2. Hofu ya mikusanyiko
3. Hofu ya matumizi ya mitandao ya kijamii
4. Kirusi kinashawishi kupindisha sheria na taratibu za kawaida
5. Hudhoofisha uwezo wa kutenda kwa haki
6. Hudhoofisha uwezo wa kukumbuka yaliyopita
7. Huzuia uwezo wa kujifunza kwa majirani na kinaongeza uwezo wa kujipendekeza kwa vyombo vya dola
8. Dalili mpya hujitokeza kwa mgonjwa kila wakati na kuhitaji kupimwa kila wakati
9. Kirusi kinamsukuma mgonjwa kuwa karibu na Mungu kinadharia na kumkimbia Mungu anapomkaribia mgonjwa

Dalili za kirusi cha LISSUPHORIA ni hizi:
1. Ujasiri uliopitiliza
2. Kuhisi kuonewa kila wakati
3. Kujiona ni tiba ya LISSUPHOBIA kwa sababu ndiye amesababisha LISSUPHORIA
4. Kuamini kuwa kinatibu kukosekana kwa ajira, na kuleta utawala bora
5. Kumfanya mgonjwa ajione ana uwezo wa kutibu kila ugonjwa ikiwemo kukosa "nguvu za kiume"
6. Mgonjwa kuamini anaanza na Mungu na kumaliza na Mungu
7. Kumfanya mgonjwa aamini kirusi hiki kinastawisha uzalendo
8. Kinamfanya mgonjwa kupoteza uwezo wa kutunza siri zake
9. Kinamfanya mgonjwa amshuku kila mtu aliyewahi kuwa karibu na mgonjwa wa LISSUPHOBIA

Virusi hivi viwili visambaa kwa kasi hapa nchini. Madaktari wanashauri wagonjwa wa virusi hivi viwili vya hatari, kutumia dawa moja inayofanana na wakiishapona wadungwe chanjo ili wasiambukizwe tena.

Dozi ya dawa hiyo ni:
1. Matumizi sawa ya vyombo vya habari kutwa mara tatu.
2. Matumizi ya hoja mara 12 kwa siku
3. Kuheshimu sheria mara 24 kwa siku
4. Kula upendo mara 2, kunywa uvumilivu mara 3 na kujipaka mafuta ya umoja mara 6 kwa siku.

Wakati wote wa kutumia dozi hii, wagonjwa waepuke:
1. Matusi na kejeli
2. Matumizi ya vyombo vya dola
3. Kutumia raslimali za nchi kwa masuala ya kiitikadi
4. Kutumia dini, kabila, au ubaguzi wa namna yoyote
5. Wote wajiepushe na imani ya kuwa mwisho wa dunia ni siku ya uchaguzi mkuu wa 2020. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Wamwogope Mungu na Teknolojia.

Hana tofauti na Nabii TITO.
 
Anajitia upo busy anaogopa akitaja jina la Lissu damu yaweza kumrudia mwishowe Wanancho washtuke lkn tushamshtukia ukitaka kujua ni nan alimpiga tundu lisasi fatilia ni nan alimtembelea afisa wa jesh aliepigwa risasi sasa utajiuliza risas apigwa lissu kutembelewa atembelewe mwingine ni kukwepa aibu
Hana muda wa kujibizana na mtu aliyeathirika na madawa ya tiba kichwani kwa miaka miwili..yule mkemia anajua
 
Askofu amelaniwa ndiyo maana anababaika hajui afanye siasa au dini ndiyo maana kipindi cha korona alifunga makanisa wakati hapakuwa na maelekezo ya serikali kufunga makanisa hilo peke yake linatosha kututhibitishia kwamba anawafundisha watu uwepo wa Mungu wakati yeye mwenyewe haamini uwezo wa Mungu.
Maaskofu tumbo hawa..sasa amerudia tena kanisa?? Maana dunia haijasema kama corona imeisha.
 
Hana muda wa kujibizana na mtu aliyeathirika na madawa ya tiba kichwani kwa miaka miwili..yule mkemia anajua
Nyiny ndo wale bendera fata upepo nan alikuambia mkemia anajua maswala ya medicine kaz kusifia tu ata msivypvijua kuna course inaitwa Doctor of medicine hawa ndio wataalamu wa madawa ndio maana TMDA na GCLA ni taasis mbili tofaut uyu jamaa yko anachojua ni mambo ya COPPER SULPHATE na catalyst
Msitufanye wote wajinga
 
Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
WEWE NI KIAZI KULIKO GWAJIMA.....!!
Baba Askofu Rev. Dkt. Benson Bagonza maono mazuri na kwa wakati....ubarikiwe baba askofu!
 
Hivi nani anayemuogopa mwenzake? Yule ambaye kila akihojiwa anamtaja taja mwenzio kila baada ya maneno mawili au yule ambaye yupo bize na spidi yake ile ile ya kuchapa kazi ambaye hana muda hata kujibizana?
Anaemwogopa mwenzie ni yule anaezuia vyombo vya habari visiripoti habari za mpinzani wake
 
Anaandika Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.

Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA. Inaonekana viliingia nchini tarehe 27/7/2020 kupitia jiji la DSM.

Madaktari wanadai dalili za LISSUPHOBIA ni hizi:
1. Hofu ya vyombo vya habari
2. Hofu ya mikusanyiko
3. Hofu ya matumizi ya mitandao ya kijamii
4. Kirusi kinashawishi kupindisha sheria na taratibu za kawaida
5. Hudhoofisha uwezo wa kutenda kwa haki
6. Hudhoofisha uwezo wa kukumbuka yaliyopita
7. Huzuia uwezo wa kujifunza kwa majirani na kinaongeza uwezo wa kujipendekeza kwa vyombo vya dola
8. Dalili mpya hujitokeza kwa mgonjwa kila wakati na kuhitaji kupimwa kila wakati
9. Kirusi kinamsukuma mgonjwa kuwa karibu na Mungu kinadharia na kumkimbia Mungu anapomkaribia mgonjwa

Dalili za kirusi cha LISSUPHORIA ni hizi:
1. Ujasiri uliopitiliza
2. Kuhisi kuonewa kila wakati
3. Kujiona ni tiba ya LISSUPHOBIA kwa sababu ndiye amesababisha LISSUPHORIA
4. Kuamini kuwa kinatibu kukosekana kwa ajira, na kuleta utawala bora
5. Kumfanya mgonjwa ajione ana uwezo wa kutibu kila ugonjwa ikiwemo kukosa "nguvu za kiume"
6. Mgonjwa kuamini anaanza na Mungu na kumaliza na Mungu
7. Kumfanya mgonjwa aamini kirusi hiki kinastawisha uzalendo
8. Kinamfanya mgonjwa kupoteza uwezo wa kutunza siri zake
9. Kinamfanya mgonjwa amshuku kila mtu aliyewahi kuwa karibu na mgonjwa wa LISSUPHOBIA

Virusi hivi viwili visambaa kwa kasi hapa nchini. Madaktari wanashauri wagonjwa wa virusi hivi viwili vya hatari, kutumia dawa moja inayofanana na wakiishapona wadungwe chanjo ili wasiambukizwe tena.

Dozi ya dawa hiyo ni:
1. Matumizi sawa ya vyombo vya habari kutwa mara tatu.
2. Matumizi ya hoja mara 12 kwa siku
3. Kuheshimu sheria mara 24 kwa siku
4. Kula upendo mara 2, kunywa uvumilivu mara 3 na kujipaka mafuta ya umoja mara 6 kwa siku.

Wakati wote wa kutumia dozi hii, wagonjwa waepuke:
1. Matusi na kejeli
2. Matumizi ya vyombo vya dola
3. Kutumia raslimali za nchi kwa masuala ya kiitikadi
4. Kutumia dini, kabila, au ubaguzi wa namna yoyote
5. Wote wajiepushe na imani ya kuwa mwisho wa dunia ni siku ya uchaguzi mkuu wa 2020. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Wamwogope Mungu na Teknolojia.

Safi saana Baba, wenye akili na u Mungu wamekuelewa na ninaimani watafanyia kazi ushauliwako

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
Umesoma vyema hoja zake, au umekimbilia kumtusi tu na kumkashifu??
 
Huwa wanaandikaga wapi... Maana kila siku nimekuwa nikiona maandiko yao kupitia kwa watu wengine na sio wao wenyewe
 
Nyiny ndo wale bendera fata upepo nan alikuambia mkemia anajua maswala ya medicine kaz kusifia tu ata msivypvijua kuna course inaitwa Doctor of medicine hawa ndio wataalamu wa madawa ndio maana TMDA na GCLA ni taasis mbili tofaut uyu jamaa yko anachojua ni mambo ya COPPER SULPHATE na catalyst
Msitufanye wote wajinga
We kweli ndio maana mfuasi wa bagonza..maana ujinga mnafanana.
 
Askofu amelaniwa ndiyo maana anababaika hajui afanye siasa au dini ndiyo maana kipindi cha korona alifunga makanisa wakati hapakuwa na maelekezo ya serikali kufunga makanisa hilo peke yake linatosha kututhibitishia kwamba anawafundisha watu uwepo wa Mungu wakati yeye mwenyewe haamini uwezo wa Mungu.
Mbona kapiga kote kote?? Kawapiga Chadema na CCM lakin mnaonekana kupanic zaid ccm kulikoni??? Mbona kasema wazi LISSUPHOBIA na LISSUPHORIA, msome vizuri achana na personal issue zake chukua hiyo content
 
We kweli ndio maana mfuasi wa bagonza..maana ujinga mnafanana.
Buku 7 mbona mnavua nguo hamuon ata aibu mwenzenu yule anasubiria aongoze malaika nadhan na nyiny itakuwa poa mkatangalia mbele za hak labda nawewe unaweza pewa teuzi huko mbingun
 
Back
Top Bottom