Askofu Bagonza: Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA



Mbona hayo mambo na zaidi ya hayo yalikuwepo na yapo hapa Zanzibar kabla hata Lisu hajaenda shule ???

Ila sasa yameanza huko Tanganyika na Lissu anapigania yaondoke ndio mnaona ni mapya??

Wacha kujipakazia ASKOFU
 
Buku 7 mbona mnavua nguo hamuon ata aibu mwenzenu yule anasubiria aongoze malaika nadhan na nyiny itakuwa poa mkatangalia mbele za hak labda nawewe unaweza pewa teuzi huko mbingun
Na huyu mwingine anataka aongoze n.y.u.m.b.u
 

Huyu ndio askofu wa kweli, sio zile takataka za kusujudia sanamu.
 
Hivi nani anayemuogopa mwenzake? Yule ambaye kila akihojiwa anamtaja taja mwenzio kila baada ya maneno mawili au yule ambaye yupo bize na spidi yake ile ile ya kuchapa kazi ambaye hana muda hata kujibizana?

Huyu anayemtaja mwenzake hana jinsi zaidi ya kumtaja, na mwenzake yuko kimya maana anamiliki kundi la watu wasiojulikana.
 
Mbona hayo mambo na zaidi ya hayo yalikuwepo na yapo hapa Zanzibar kabla hata Lisu hajaenda shule ???

Ila sasa yameanza huko Tanganyika na Lissu anapigania yaondoke ndio mnaona ni mapya??

Wacha kujipakazia ASKOFU
Whats your point mkuu
 
Whats your point mkuu


Point ni kuwa Watawala wa CCM siku zote wanaendeleza dhuluma na hakuna jipya . Sasa wakitokea watu kama huyu Lisu wanaotetea haki inakuwa noma.

Watajaribu kila hali wamnyamazishe.

Hapa Zanzibar wengi watu wa Style ya Lisu wamepoteza maisha na hao watu wa dini waliojaribu kusema ndio wamezushiwa kesi za ugaidi wako magerezani wanateswa.
 
Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
Kazi yake moja wapo ni kuwaonya watu kujiepusha na maovu! Sasa kama mtumishi wa serikali mtenda maovu akionywa ndo Askofu aonekane mwanasiasa?

And the judgment is based on this fact: God’s light came into the world, but people loved the darkness more than the light, for their actions were evil.
John 3:19.

Kwa hiyo watenda waovu huwa wanapenda mambo ya kificho sana ili matendo yao mabaya yasijulikane
 
Hapo nimekupata sana mkuu
 
Askofu mtiifu wa mabeberu, Msanii, Msaliti na Mnafiki ameshindwa kutumia elimu yake ya thiolojia kuongoa roho za waumini wake badala yake anakubali kutumiwa na mabeberu kueneza hoja butu zisizoweza kumkwamua mwananchi anayeishi chini ya dola moja kwa siku, Jesus Christ alishawaonya watu wasidanganyike na roho zidanganyazo, na alienda mbali akawaonya mitume wake kuwa making na mafarisayo kwa unafiki wao, Mwambieni askofu kwenye janga la Covid-19 vyombo vya habari vya nje vilikuwa bize na Covid-19 ya Tanzania, Licha ya kuwa nchi zinazopossess media hizo raia wao walikuwa wakiangamia Kila siku, Lakini Rais Magufuli alikuwa anapingwa na hao wafuasi wa Lissu Kila hatua alizokuwa akijitahidi kuzipiga, mtu anayejiita kiongozi anashabikia lockdown, angalia waganda waliojifungia ndani wiki 2, Nini kiliwatokea?? Namshukuru Mungu muumba wa mbingu na ardhi anaendelea kusimama na Rais Jpm mpaka Sasa hajayumba, amekuea mfano wa mbele kuwatoa hofu watanzania juu ya janga hilo, Askofu mfuasi wa mabeberu mwambie afanye toba ya kweli amrudie Mungu wake naye ataoneshwa uwezo wa kiongozi bora.
 
Shikamoo baba askofu Bagonza
 
Halafu unajiita Paulo, hata akili za kufikiri hauna umekuwa kama zumbukuku
 
Halafu unajiita Paulo, hata akili za kufikiri hauna umekuwa kama zumbukuku
Laiti Kama ungekuwa unahisi hata 0.01% ya feeling ungeweza kumgudge askofu wako lkn kwa kuwa ni rika la tunataka mapinduzi pambana unaweza kuwa balozi hata wa nyumba 10
 
Hongera Baba Askofu, endelea kutimiza wajibu wako wa kukemea na kuyapazia sauti yanayoendelea katika nchi yetu ambayo unaona hayako sawa, wajibu wa viongozi wa dini si kutupatia sakramenti na kutuombea tu mbele ya madhabahu hapana wajibu mkubwa kabisa ni kusimamia maadili yetu sisi na viongozi wetu ili nchi itawaliwe wa HAKI na USAWA.

Hazina yako ipo mbinguni....piga kazi.
 
Mbona kapiga kote kote?? Kawapiga Chadema na CCM lakin mnaonekana kupanic zaid ccm kulikoni??? Mbona kasema wazi LISSUPHOBIA na LISSUPHORIA, msome vizuri achana na personal issue zake chukua hiyo content
Elimu iliyeyuka kitambo,darasa la kwanza wapo watoto 200 chumba kimmoja,bado utaita elimu au mkutano?
 
Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
Huyu ndiye mtumishi halisi wa neno la MUNGU hana unafiki kwa maana daima ni mkweli na ni mkweli daima. Na kumbuka msema kweli ni mpenzi wa MUNGU
 
Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
Huyu ni Mwanasiasa aliejificha kwenye kivuli cha Uaskofu. kwa ufupi ni kamanda wa CHADEMA
 
Hana muda wa kujibizana na mtu aliyeathirika na madawa ya tiba kichwani kwa miaka miwili..yule mkemia anajua
Lile dubwana liko empty kichwani. Ndio maana liliandikiwa pihechidi na jamaa wa jalalani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…