Askofu Bagonza: Ushindi wa kishindo ni kaburi la maendeleo Afrika

Na utatoka vipi kwenye siasa wakati kuna ndugu zako wamebambikizwa kesi za ugaidi ?? wengine wamepigwa risasi , wengine tunadaiwa kulipa shuleni , wengine tunapoumwa madakitari wanataka kitu kidogo watuhudumie kwani mshahara hauwawatoshi , list haishi
Hayo ni mambo ya kupambana nayo kama vile unavyotakiwa kupambana na hali yako! Usitafute visingizio vya aina yoyote katika kupambana na udhalimu wa aina yoyote katika jamii kama kweli wewe unapenda haki. Mambo kama rushwa, kubambikiwa kesi, kudaiwa ada au michango na walimu mamluki, ni mambo yako ndani ya uwezo wetu, ni suala la "kujilipua" na kudai haki yako, hata kama ikibidi kwenda IKULU sawa, nenda! Haki haipatikani kwa kulalamika au kusema mauongo. Haki inapatikana kwa kusema ukweli wenye vielelezo bila WOGA!
 
Na vipi hawa viongozi wanaouwa watu ili kujibakiza madarakani?? wengine wanawachukulia watu mashamba yao na kujimilikisha wao, kama huyu Mzee Mwinyi na marehemu Mkapa ?? na huyu mfalme wa Chato kule Tanga ?? Na wengine wananunua ndege bila kutaja walinunua kwa bei gani ?? na wengine wanapewa hela na hao mabeberu wa EU za kusaidia wenye corona , wanazitafuna bila wasiwasi.??? listi ni ndefu
Haya usemayo siyo mageni! Ni UONGO tuliowahi kuusikia toka kwa Lissu na BOB wake; na wewe unauleta tena. Haya ya watu kupigwa risasi za ndege ya akina Lissu tulishayaeleza humu kuwa ulikuwa ni muendelezo wa vita ya kugombea UENYEKITI ndani ya CHADEMA ndiyo maana hamtaki kumsalimisha dereva wa Lissu kwani atamwaga mambo yote hadharani. UONGO usio na ushahidi ni kama kumpigia mbuzi gitaa, unapoteza muda na rasilimali zako.
 
Una elimu gani wewe? Tuanzie hapo kwanza. Kama umeshindwa kumuelewa askofu kwa maelezo mepesi hivi, nina shaka na uwezo wa kichwa chako.
Askofu, Askofu! Basi aje na maelezo ya kweli siyo suala la kunakiri vifungu vya Biblia Takatifu na kutaka ASIHOJIWE! Huko ni kujificha na kukwepa ukweli. Tutakuhoji tu mpaka ueleweke! Na wewe unaye muelewa Askofu, basi yaelezee hayo asemayo kwa lugha nyepesi ili hao unawashakia uwezo wa vichwa vyao wakuelewe!
 
USHINDI WA KISHINDO NI KABURI LA MAENDELEO AFRIKA

Tumemaliza Uchaguzi. Walioshinda wamepata asilimia 84 (urais) na bunge asilimia 99. Huu ni ushindi wa kishindo au kishindo cha ushindi?

Tukubaliane: Tuna watu wengi ni waaminifu kwa sababu hawana cha kuiba au wanaogopa kukamatwa. Serikali nyingi ziko hivyo. Zinahitaji kusimamiwa, kuchunguzwa, kukosolewa ili zifanye vizuri. Hata katika ulimwengu wa Imani, uwepo wa shetani ni msingi wa jitihada za kufundisha uadilifu.

Marekani wamemaliza Uchaguzi wao. Urais umeenda kwa chama Cha Democrat kwa kupata viti 306 dhidi ya 232 vya Trump (electoral colleges).

Bungeni (Cogress), Democrat wamepata viti 232 dhidi ya 197 vya Republican.

Kwenye Senate Republican wamepata viti 50 dhidi ya 48 vya Democrat. Viti 2 bado kuchaguliwa.

Kwa hiyo Rais mteule Biden atakuwa Ikulu bila kuwa na wingi wa kutisha wa wabunge na kwenye Senate chama pinzani ndicho kina viti 2 zaidi ya chama tawala. Hali hii inaweza kubadilika baada ya miaka miwili utakapofanyika Uchaguzi mdogo wa baadhi ya majimbo ya Bunge na senate. Kwenye uchaguzi huo, Biden anaweza kukosa wingi kwenye bunge na senate. Kwa nini?

1. Wamarekani hawapendi kuweka mayai yote kikapu kimoja (urais, ubunge na useneta). Ukipewa urais unanyimwa ama wabunge au maseneta ili ujifunze kushirikiana na wapinzani kwa kutumia hoja siyo bunduki.

2. Check and balance (kuwajibishana) ni msingi maamuzi ya kila kitu. Hata kwenye vyombo vya habari ni lazima kikisemwa kitu sharti upande wa pili uwekwe ili wasomaji/ wasililizaji wajue pande mbili na kuamua wenyewe.

Kimantiki, ushindi wa kishindo chaweza kuwa chanzo cha mdororo wa Maendeleo katika bara letu linalopenda sana neno NDIYO. Tabia ya kuchukia maoni tofauti inadumaza utundu, ugunduzi, na ubunifu. Badala yake dhana ya NDIYO inakomaza kukariri, woga, utii usio na dhamiri na kuondoa uendelevu(sustainability) katika maamuzi mengi. Mfumo wa Elimu ndilo jiko la kupika Taifa linalohoji au linaloimba NDIYO kwa kila kitu.

Mfungwa katika mfumo wa NDIYO akiwekewa mkate na funguo za gereza akaambiwa achague moja, atachagua mkate.

Mfungwa katika gereza la KWA NINI, akiwekewa hivyo viwili, anaweza akahoji kwa nini si vitatu badala ya KUCHAGUA kama alivyoelekezwa.

Zawadi ya mfungwa ni Uhuru si sabuni ya kuoga akiwa gerezani. Kumwachia huru mfungwa ni sawa na kumweka huru Askari magereza anayemlinda. Hiyo ndiyo faida kuu ya Uhuru. Unanufaisha pande zote.
Muulize huyo mzee kama ana imani na akijua mungu husikiliza maombi ya wateule wake,
na kama mungu ameshindwa kuwasililiza watu wa mungu wanne (4) Bagonza, Mwamakula, Katimba na Ponda, basi ajue hata mungu hayupo upande wao, wanapaswa kutubu zaidi na kumuomba mungu ili siku moja maombi yao yasikilizwe.
Na kama ni muumini mzuri hiyo nafasi angejiuzuru kwa kuwa mungu amekataa maobi yao.
Sasa kabaki kubwabwaja kama mke mwenza badala ya kuomba mungu awape kondoo wake uzima na afya.

Bagonza kama anafikiri yeye anapendwa zaidi aje ajipime aone wangapi watamchagua.
 
Ni aibu na dhambi inayohitaji MTU muungwana kutubu pale mgombea anaposema msipomchagua fulani wa chama changu msinidai maji,Barabara etc.
Sikuwahi kuwaza tunaweza kuwa na kiongozi kwenye kauli zahivi!!!
 
Afrika inaangamia kwa kulazimisha mfumo wa kiutawala wa kuazima ambao hauendani hata kidogo na uhalisia. Kwa wanaojua historia wanajua kuwa kabla ya huu wendawazimu wa kimagharibi jamii zetu hazikuwahi kuwa na migogoro ya ndani kwa ndani.

Huyo askofu wenu akumbuke kuwa watanzania kwa mfano hawajaanza leo kuukataa huo upuuzi unaoitwa demokrasia. Hayo pia ni madhara ya kupuuza maoni ya watu wengi.

Hii demokrasia ya kimagharibi inajifanya kuwa sauti ya watu ilhali ujio wake ulikuwa wa kibabe usiojali sauti za watu walioukataa (rejea kura ya maoni ya mwaka 92).

Pia pengine aliyeturoga waafrika alikufa kweli. Huyo askofu na wafuasi wake wa mitandaoni hawakumbuki kuwa hao wazungu walitutawala (ukoloni) bila demokrasia? Kwa nini wao hawakutumia demokrasia kututawala? Ni rahisi, wanajua waafrika wengi wa kisasa (wasomi) ni marehemu kifikra.
 
Wahaya wana shida sana, kwa dharau zile za Bagonza kisa ule udokta wake, basi yeye kwake Mungu si lolote mbele ya phd yake.
Bagonza sio Mhaya.

Nasikia kabila lake ni Mnyambo.

Ukweli kuhusu makabila ya Kagerauko hivi :
  1. Waziba wa Kiziba,
  2. Wahamba wa Muhutwe,
  3. Wayoza wa Bugabo
  4. Waendangabo wa Bugabo,
  5. Wanyaiyangilo wa Muleba,
  6. Wakara wa Ukerewe,
  7. Wasubi wa Biharamulo
  8. Wazinza wa Ukerewe.
 
Hayo ni mambo ya kupambana nayo kama vile unavyotakiwa kupambana na hali yako! Usitafute visingizio vya aina yoyote katika kupambana na udhalimu wa aina yoyote katika jamii kama kweli wewe unapenda haki. Mambo kama rushwa, kubambikiwa kesi, kudaiwa ada au michango na walimu mamluki, ni mambo yako ndani ya uwezo wetu, ni suala la "kujilipua" na kudai haki yako, hata kama ikibidi kwenda IKULU sawa, nenda! Haki haipatikani kwa kulalamika au kusema mauongo. Haki inapatikana kwa kusema ukweli wenye vielelezo bila WOGA!
Wewe ni kijana uliyezaliwa hivi majuzi labda kwenyebio za mwenge. Hao viongozi wako wamewaweka wengi gerezani kwa kuambiwa matatizo ya nchi
mbele yao. Hivi hawa watu waliouliwa ,kuteswa na kuibiwa majumbani hao wanasiasa wako si ndio wanaowakingia kifua wauwaji majukwaani. Hivi siasa kwako wewe ni kikundi cha majambaji kujitwalia madaraka kwa kulitumia jeshi?
 
Haya usemayo siyo mageni! Ni UONGO tuliowahi kuusikia toka kwa Lissu na BOB wake; na wewe unauleta tena. Haya ya watu kupigwa risasi za ndege ya akina Lissu tulishayaeleza humu kuwa ulikuwa ni muendelezo wa vita ya kugombea UENYEKITI ndani ya CHADEMA ndiyo maana hamtaki kumsalimisha dereva wa Lissu kwani atamwaga mambo yote hadharani. UONGO usio na ushahidi ni kama kumpigia mbuzi gitaa, unapoteza muda na rasilimali zako.

Ni uongo na mashamba yetu mengine yamenyakuliwa na hao wezi? Mbona wenyewe hawajawahipo kukanusha popote??Au wewe ni msemaji wao??
 
USHINDI WA KISHINDO NI KABURI LA MAENDELEO AFRIKA

Tumemaliza Uchaguzi. Walioshinda wamepata asilimia 84 (urais) na bunge asilimia 99. Huu ni ushindi wa kishindo au kishindo cha ushindi?

Tukubaliane: Tuna watu wengi ni waaminifu kwa sababu hawana cha kuiba au wanaogopa kukamatwa. Serikali nyingi ziko hivyo. Zinahitaji kusimamiwa, kuchunguzwa, kukosolewa ili zifanye vizuri. Hata katika ulimwengu wa Imani, uwepo wa shetani ni msingi wa jitihada za kufundisha uadilifu.

Marekani wamemaliza Uchaguzi wao. Urais umeenda kwa chama Cha Democrat kwa kupata viti 306 dhidi ya 232 vya Trump (electoral colleges).

Bungeni (Cogress), Democrat wamepata viti 232 dhidi ya 197 vya Republican.

Kwenye Senate Republican wamepata viti 50 dhidi ya 48 vya Democrat. Viti 2 bado kuchaguliwa.

Kwa hiyo Rais mteule Biden atakuwa Ikulu bila kuwa na wingi wa kutisha wa wabunge na kwenye Senate chama pinzani ndicho kina viti 2 zaidi ya chama tawala. Hali hii inaweza kubadilika baada ya miaka miwili utakapofanyika Uchaguzi mdogo wa baadhi ya majimbo ya Bunge na senate. Kwenye uchaguzi huo, Biden anaweza kukosa wingi kwenye bunge na senate. Kwa nini?

1. Wamarekani hawapendi kuweka mayai yote kikapu kimoja (urais, ubunge na useneta). Ukipewa urais unanyimwa ama wabunge au maseneta ili ujifunze kushirikiana na wapinzani kwa kutumia hoja siyo bunduki.

2. Check and balance (kuwajibishana) ni msingi maamuzi ya kila kitu. Hata kwenye vyombo vya habari ni lazima kikisemwa kitu sharti upande wa pili uwekwe ili wasomaji/ wasililizaji wajue pande mbili na kuamua wenyewe.

Kimantiki, ushindi wa kishindo chaweza kuwa chanzo cha mdororo wa Maendeleo katika bara letu linalopenda sana neno NDIYO. Tabia ya kuchukia maoni tofauti inadumaza utundu, ugunduzi, na ubunifu. Badala yake dhana ya NDIYO inakomaza kukariri, woga, utii usio na dhamiri na kuondoa uendelevu(sustainability) katika maamuzi mengi. Mfumo wa Elimu ndilo jiko la kupika Taifa linalohoji au linaloimba NDIYO kwa kila kitu.

Mfungwa katika mfumo wa NDIYO akiwekewa mkate na funguo za gereza akaambiwa achague moja, atachagua mkate.

Mfungwa katika gereza la KWA NINI, akiwekewa hivyo viwili, anaweza akahoji kwa nini si vitatu badala ya KUCHAGUA kama alivyoelekezwa.

Zawadi ya mfungwa ni Uhuru si sabuni ya kuoga akiwa gerezani. Kumwachia huru mfungwa ni sawa na kumweka huru Askari magereza anayemlinda. Hiyo ndiyo faida kuu ya Uhuru. Unanufaisha pande zote.
Njia ya kwenda Mbinguni ni nyembamba.
Waionao ni wachache na wanaoipita ni wachache. Jitahidini kuipita....

Askofu anapita njia ya wengi ambayo ina kila aina ya ufahari na ukwasi.

Siku ambayo ataisema CDM kwa kuikosoa hapo ndipo atakuwa amegusa mfupa.

Siku inakuja
 
USHINDI WA KISHINDO NI KABURI LA MAENDELEO AFRIKA

Tumemaliza Uchaguzi. Walioshinda wamepata asilimia 84 (urais) na bunge asilimia 99. Huu ni ushindi wa kishindo au kishindo cha ushindi?

Tukubaliane: Tuna watu wengi ni waaminifu kwa sababu hawana cha kuiba au wanaogopa kukamatwa. Serikali nyingi ziko hivyo. Zinahitaji kusimamiwa, kuchunguzwa, kukosolewa ili zifanye vizuri. Hata katika ulimwengu wa Imani, uwepo wa shetani ni msingi wa jitihada za kufundisha uadilifu.

Marekani wamemaliza Uchaguzi wao. Urais umeenda kwa chama Cha Democrat kwa kupata viti 306 dhidi ya 232 vya Trump (electoral colleges).

Bungeni (Cogress), Democrat wamepata viti 232 dhidi ya 197 vya Republican.

Kwenye Senate Republican wamepata viti 50 dhidi ya 48 vya Democrat. Viti 2 bado kuchaguliwa.

Kwa hiyo Rais mteule Biden atakuwa Ikulu bila kuwa na wingi wa kutisha wa wabunge na kwenye Senate chama pinzani ndicho kina viti 2 zaidi ya chama tawala. Hali hii inaweza kubadilika baada ya miaka miwili utakapofanyika Uchaguzi mdogo wa baadhi ya majimbo ya Bunge na senate. Kwenye uchaguzi huo, Biden anaweza kukosa wingi kwenye bunge na senate. Kwa nini?

1. Wamarekani hawapendi kuweka mayai yote kikapu kimoja (urais, ubunge na useneta). Ukipewa urais unanyimwa ama wabunge au maseneta ili ujifunze kushirikiana na wapinzani kwa kutumia hoja siyo bunduki.

2. Check and balance (kuwajibishana) ni msingi maamuzi ya kila kitu. Hata kwenye vyombo vya habari ni lazima kikisemwa kitu sharti upande wa pili uwekwe ili wasomaji/ wasililizaji wajue pande mbili na kuamua wenyewe.

Kimantiki, ushindi wa kishindo chaweza kuwa chanzo cha mdororo wa Maendeleo katika bara letu linalopenda sana neno NDIYO. Tabia ya kuchukia maoni tofauti inadumaza utundu, ugunduzi, na ubunifu. Badala yake dhana ya NDIYO inakomaza kukariri, woga, utii usio na dhamiri na kuondoa uendelevu(sustainability) katika maamuzi mengi. Mfumo wa Elimu ndilo jiko la kupika Taifa linalohoji au linaloimba NDIYO kwa kila kitu.

Mfungwa katika mfumo wa NDIYO akiwekewa mkate na funguo za gereza akaambiwa achague moja, atachagua mkate.

Mfungwa katika gereza la KWA NINI, akiwekewa hivyo viwili, anaweza akahoji kwa nini si vitatu badala ya KUCHAGUA kama alivyoelekezwa.

Zawadi ya mfungwa ni Uhuru si sabuni ya kuoga akiwa gerezani. Kumwachia huru mfungwa ni sawa na kumweka huru Askari magereza anayemlinda. Hiyo ndiyo faida kuu ya Uhuru. Unanufaisha pande zote.
hana tofauti na nabii tito
 
Bro data za Bunge la marekani umegoogle nini, Mpka sasa republican wana viti 211 Kwa 222 vya democrat
 
Ni uongo na mashamba yetu mengine yamenyakuliwa na hao wezi? Mbona wenyewe hawajawahipo kukanusha popote??Au wewe ni msemaji wao??
Kama wamechukua ardhi kisheria lakini wewe unaona WAMEPORA, basi hiyo ni SHIDA! Hebu nendeni kwa Pilato badala ya kusemasema humu JF bila ushahidi wowote!
 
Ndivyo walivyokuambia kuwa wamechukua kisheria. Mbona haya mambo yamesemwa kwenye majukwaa na wao hawajayakanusha , wacha kujamba jamba tu
 
Serious people do not work from MAJUKWAA, watu wanafanyia kazi mambo yenye ushahidi siyo hoja za kibabaishaji huko kwenye majukwaa. Nani akanushe upuuzi na uongo huo!
 
Back
Top Bottom