Askofu Bagonza: Ushindi wa kishindo ni kaburi la maendeleo Afrika

Haki, uhuru na demokrasi ni wajibu wa Taifa lolote kuhakikisha inapatikana kwa raia wote wa kila Nchi duniani na siyo USA tu.
Bagonnza karefer USA kama.mfano

Kumbe hujamsoma
 
Haki, uhuru na demokrasi ni wajibu wa Taifa lolote kuhakikisha inapatikana kwa raia wote wa kila Nchi duniani na siyo USA tu.
Hujajibu hoja

Our democracy ni ipi?
 
Haki, uhuru na demokrasi ni wajibu wa Taifa lolote kuhakikisha inapatikana kwa raia wote wa kila Nchi duniani na siyo USA tu.
I wish CDM wangeanzia ndani hayo wanayoabudu
 
But not maccm because over there their house is in excellent condition. Usinilazimishe kuelewa pumba zako.
Tayari umenielewa

Charity begins at home
 
But not maccm because over there their house is in excellent condition. Usinilazimishe kuelewa pumba zako.
Ukitaka haki, usawa, Uhuru na dwmokrasia usinyooshe kidole.... Zungusha pangaboi liguse kila kona

Usicheze double standards... Iwe CCM, CDM, democrats, PLO, unita etc.

That was my point

Ndio maana nikauliza bagonnza mlengo wake ni upi?

Maana kama ni hivyo unavyohubiri basi marekani sio mfano bora

Na haya yanaenda Hadi kwenye familia

Huwezi kutaka haki na usawa wakati wewe ni abusive even to your family and friends

Tuitazame haki Kwa kiini chake na sio milengo ya wachache
 
Na utatoka vipi kwenye siasa wakati kuna ndugu zako wamebambikizwa kesi za ugaidi ?? wengine wamepigwa risasi , wengine tunadaiwa kulipa shuleni , wengine tunapoumwa madakitari wanataka kitu kidogo watuhudumie kwani mshahara hauwawatoshi , list haishi
Ni maneno ya siasa ayo.
Iyo list yako yoote imekataa kuandamana inamaana wameridhika na maisha yao na bado mnaemtuhumu akipitana msafara barabarani wanajaa barabarani uku wakimshangilia.
 
USHINDI WA KISHINDO NI KABURI LA MAENDELEO AFRIKA

Tumemaliza Uchaguzi. Walioshinda wamepata asilimia 84 (urais) na bunge asilimia 99. Huu ni ushindi wa kishindo au kishindo cha ushindi?

Tukubaliane: Tuna watu wengi ni waaminifu kwa sababu hawana cha kuiba au wanaogopa kukamatwa. Serikali nyingi ziko hivyo. Zinahitaji kusimamiwa, kuchunguzwa, kukosolewa ili zifanye vizuri. Hata katika ulimwengu wa Imani, uwepo wa shetani ni msingi wa jitihada za kufundisha uadilifu.

Marekani wamemaliza Uchaguzi wao. Urais umeenda kwa chama Cha Democrat kwa kupata viti 306 dhidi ya 232 vya Trump (electoral colleges).

Bungeni (Cogress), Democrat wamepata viti 232 dhidi ya 197 vya Republican.

Kwenye Senate Republican wamepata viti 50 dhidi ya 48 vya Democrat. Viti 2 bado kuchaguliwa.

Kwa hiyo Rais mteule Biden atakuwa Ikulu bila kuwa na wingi wa kutisha wa wabunge na kwenye Senate chama pinzani ndicho kina viti 2 zaidi ya chama tawala. Hali hii inaweza kubadilika baada ya miaka miwili utakapofanyika Uchaguzi mdogo wa baadhi ya majimbo ya Bunge na senate. Kwenye uchaguzi huo, Biden anaweza kukosa wingi kwenye bunge na senate. Kwa nini?

1. Wamarekani hawapendi kuweka mayai yote kikapu kimoja (urais, ubunge na useneta). Ukipewa urais unanyimwa ama wabunge au maseneta ili ujifunze kushirikiana na wapinzani kwa kutumia hoja siyo bunduki.

2. Check and balance (kuwajibishana) ni msingi maamuzi ya kila kitu. Hata kwenye vyombo vya habari ni lazima kikisemwa kitu sharti upande wa pili uwekwe ili wasomaji/ wasililizaji wajue pande mbili na kuamua wenyewe.

Kimantiki, ushindi wa kishindo chaweza kuwa chanzo cha mdororo wa Maendeleo katika bara letu linalopenda sana neno NDIYO. Tabia ya kuchukia maoni tofauti inadumaza utundu, ugunduzi, na ubunifu. Badala yake dhana ya NDIYO inakomaza kukariri, woga, utii usio na dhamiri na kuondoa uendelevu(sustainability) katika maamuzi mengi. Mfumo wa Elimu ndilo jiko la kupika Taifa linalohoji au linaloimba NDIYO kwa kila kitu.

Mfungwa katika mfumo wa NDIYO akiwekewa mkate na funguo za gereza akaambiwa achague moja, atachagua mkate.

Mfungwa katika gereza la KWA NINI, akiwekewa hivyo viwili, anaweza akahoji kwa nini si vitatu badala ya KUCHAGUA kama alivyoelekezwa.

Zawadi ya mfungwa ni Uhuru si sabuni ya kuoga akiwa gerezani. Kumwachia huru mfungwa ni sawa na kumweka huru Askari magereza anayemlinda. Hiyo ndiyo faida kuu ya Uhuru. Unanufaisha pande zote.
Mkuu, tukuombe uwatafsirie MATAGA uzi huu kwa lugha nyepesi kwani ninaamini wote wametoka hola hapa!
 
Usijifanye unanijua! Chadema huwezi kufanananisha na yanayojiri maccm. Huyo anayejiita mwendawazimu amefikia hadi kubambikia watu kesi na hata kuwaua kwa sababu tu wamemkosoa hadharani au kumuandika vibaya.

Hakuna uwiano wowote ule kati yanayojiri ndani ya maccm na Chadema.

Narudia tena mlengo hauhusu kitu kwenye kuhakikisha raia wa Nchi yeyote ile duniani kuhakikishiwa haki, uhuru na demokrasia ya kweli.
Ukitaka haki, usawa, Uhuru na dwmokrasia usinyooshe kidole.... Zungusha pangaboi liguse kila kona

Usicheze double standards... Iwe CCM, CDM, democrats, PLO, unita etc.

That was my point

Ndio maana nikauliza bagonnza mlengo wake ni upi?

Maana kama ni hivyo unavyohubiri basi marekani sio mfano bora

Na haya yanaenda Hadi kwenye familia

Huwezi kutaka haki na usawa wakati wewe ni abusive even to your family and friends

Tuitazame haki Kwa kiini chake na sio milengo ya wachache
 
Rais Magufuli alituomba sana tumuombee na tuliombee taifa letu na biblia inasema maombi ya mwenye haki ni manukato mbele za Mungu

Na pia biblia pia inasema tusiwaseme viongozi wa dini vibaya na tuzitii mamlaka za dunia kwani mamlaka zote zatoka kwa Mungu. Niishie hapo tuu, mimi ni nani nimgombanishe askofu, shehe au rais na Mungu?!
Mimi uwa natembelea nchi za jirani mara kwa mara.
wenyeji wa izonchi ukifika tu wanaanza kukuuliza habari za JPM,yani uwaambii kitu.
kwenye mioyo yao wanatamani na wanaomba wapate kiongozi kama JPM,yani uwaambii kitu.
JPM anafanyiwa maombi mpaka na majirani.
 
USHINDI WA KISHINDO NI KABURI LA MAENDELEO AFRIKA

Tumemaliza Uchaguzi. Walioshinda wamepata asilimia 84 (urais) na bunge asilimia 99. Huu ni ushindi wa kishindo au kishindo cha ushindi?

Tukubaliane: Tuna watu wengi ni waaminifu kwa sababu hawana cha kuiba au wanaogopa kukamatwa. Serikali nyingi ziko hivyo. Zinahitaji kusimamiwa, kuchunguzwa, kukosolewa ili zifanye vizuri. Hata katika ulimwengu wa Imani, uwepo wa shetani ni msingi wa jitihada za kufundisha uadilifu.

Marekani wamemaliza Uchaguzi wao. Urais umeenda kwa chama Cha Democrat kwa kupata viti 306 dhidi ya 232 vya Trump (electoral colleges).

Bungeni (Cogress), Democrat wamepata viti 232 dhidi ya 197 vya Republican.

Kwenye Senate Republican wamepata viti 50 dhidi ya 48 vya Democrat. Viti 2 bado kuchaguliwa.

Kwa hiyo Rais mteule Biden atakuwa Ikulu bila kuwa na wingi wa kutisha wa wabunge na kwenye Senate chama pinzani ndicho kina viti 2 zaidi ya chama tawala. Hali hii inaweza kubadilika baada ya miaka miwili utakapofanyika Uchaguzi mdogo wa baadhi ya majimbo ya Bunge na senate. Kwenye uchaguzi huo, Biden anaweza kukosa wingi kwenye bunge na senate. Kwa nini?

1. Wamarekani hawapendi kuweka mayai yote kikapu kimoja (urais, ubunge na useneta). Ukipewa urais unanyimwa ama wabunge au maseneta ili ujifunze kushirikiana na wapinzani kwa kutumia hoja siyo bunduki.

2. Check and balance (kuwajibishana) ni msingi maamuzi ya kila kitu. Hata kwenye vyombo vya habari ni lazima kikisemwa kitu sharti upande wa pili uwekwe ili wasomaji/ wasililizaji wajue pande mbili na kuamua wenyewe.

Kimantiki, ushindi wa kishindo chaweza kuwa chanzo cha mdororo wa Maendeleo katika bara letu linalopenda sana neno NDIYO. Tabia ya kuchukia maoni tofauti inadumaza utundu, ugunduzi, na ubunifu. Badala yake dhana ya NDIYO inakomaza kukariri, woga, utii usio na dhamiri na kuondoa uendelevu(sustainability) katika maamuzi mengi. Mfumo wa Elimu ndilo jiko la kupika Taifa linalohoji au linaloimba NDIYO kwa kila kitu.

Mfungwa katika mfumo wa NDIYO akiwekewa mkate na funguo za gereza akaambiwa achague moja, atachagua mkate.

Mfungwa katika gereza la KWA NINI, akiwekewa hivyo viwili, anaweza akahoji kwa nini si vitatu badala ya KUCHAGUA kama alivyoelekezwa.

Zawadi ya mfungwa ni Uhuru si sabuni ya kuoga akiwa gerezani. Kumwachia huru mfungwa ni sawa na kumweka huru Askari magereza anayemlinda. Hiyo ndiyo faida kuu ya Uhuru. Unanufaisha pande zote.
Bagonza NI mwanasiasa aliyejificha kwenye kivuri Cha dini
 
Mimi uwa natembelea nchi za jirani mara kwa mara.
wenyeji wa izonchi ukifika tu wanaanza kukuuliza habari za JPM,yani uwaambii kitu.
kwenye mioyo yao wanatamani na wanaomba wapate kiongozi kama JPM,yani uwaambii kitu.
JPM anafanyiwa maombi mpaka na majirani.

Rafiki zangu raia wa Jumuiya ya ulaya wananiambia Dunia nzima hakuna rais kama Magufuli

Sababu wanayotoa ni kwamba Magufuli ni rais wa watanzania na anafanya kazi kwaajili ya watu wake

Sasa wewe mtanzania kama huelewi maana basi tena
 
Kutunga jambo ni simple tu,endeleen kujidanganya
Mimi uwa natembelea nchi za jirani mara kwa mara.
wenyeji wa izonchi ukifika tu wanaanza kukuuliza habari za JPM,yani uwaambii kitu.
kwenye mioyo yao wanatamani na wanaomba wapate kiongozi kama JPM,yani uwaambii kitu.
JPM anafanyiwa maombi mpaka na majirani.
 
Usijifanye unanijua! Chadema huwezi kufanananisha na yanayojiri maccm. Huyo anayejiita mwendawazimu amefikia hadi kubambikia watu kesi na hata kuwaua kwa sababu tu wamemkosoa hadharani au kumuandika vibaya.

Hakuna uwiano wowote ule kati yanayojiri ndani ya maccm na Chadema.

Narudia tena mlengo hauhusu kitu kwenye kuhakikisha raia wa Nchi yeyote ile duniani kuhakikishiwa haki, uhuru na demokrasia ya kweli.
Unabehave kama.mataga
 
Back
Top Bottom