Askofu Benson Bagonza: Kuweka nchi sawa ni kazi isiyoisha

Askofu Benson Bagonza: Kuweka nchi sawa ni kazi isiyoisha

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Askofu Dkt. Benson Bagonza, Askofu Mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe

"Nampongeza mama kwa "100 kwanza". Namwombea "100 tena" zenye maono mapana zaidi"

"Haki na uhuru ni misingi imara ya kuweka nchi sawa. Ukiyaahirisha unajitwisha mzigo mzito. Dai la katiba mpya lina faida kubwa kwa Rais kuliko kwa taasisi nyinginezo. Katiba mpya ni dawa si kikwazo"

"Uhuru wa kisiasa ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi. Ukiahirisha maisha ya siasa, umesimamisha ukuaji wa uchumi. Tufikiri upya"

"Aliyepita alifanya mambo. Huyu amefanya mambo kwa siku 100 yakafurahisha. Akija mwingine kwa mazingira ya alivyokuja huyu (hatuombei), naye aondoe haya na kuleta mengine? Tutamaliza lini?"

"Kuweka nchi sawa kwanza" ni kazi isiyoisha na ni ya kila siku. Nchi huwekwa sawa kwa kutumia katiba na sheria si kwa kuahirisha matumizi ya katiba na sheria"

"Unapoanza kuahirisha matumizi ya Katiba/sheria unakuwa umekabidhi nchi iongozwe na mtu au kundi. Madhara yake ni haya: Hata wawekezaji hawawezi kukuamini kwa sababu hawajui kesho utaamua nini? Usalama wa mitaji huletwa na sheria siyo matamshi wala ahadi"

"Kulikuwa na tetesi kuwa watu fulani walijaribiwa kuahirisha katiba wakati wa msiba ili kwanza tuzike. Huwezi jua waliwaza nini na ahirisho hilo. Nani ajuaye labda walikuwa na kigugumizi cha kumpokea mama?"

"Hivi karibuni pia tumeshuhudia haya: Kukamata watu na kuwaweka ndani bila utaratibu kwa sababu tuko kwenye vita ya kiuchumi na huko nyuma "tumepigwa sana"

"Hivi karibuni tumeshuhudia haya: 1. Kuzuia mikutano ya kisiasa ili kwanza "kunyoosha nchi". 2. Kuzuia nyongeza mishahara ili kwanza kukamilisha miradi ya kimkakati. 3. Kuzuia upandishaji wa madaraja na vyeo kazini ili kwanza tuhakiki mambo"

"Ni hatari kuahirisha(suspend or postpone) matumizi ya sheria na katiba katika kuongoza nchi kwa sababu yoyote ile. Tawala za kijeshi ndizo zenye tabia hii. Tawala za kiraia huweza kufanya hivyo wakati wa vita au hali ya hatari kwa ruhusa maalum ya bunge
 
Mchakato wa Katiba mpya ni gharama ambayo inatakiwa kufidiwa na pesa za walipakodi ambao wanategemea kodi itumike kujenga uchumi badala ya kutumika kwa vitu ambavyo haviongezi uzalishaji. Rais Samia yupo sahihi, kujenga uchumi kwanza Katiba baadaye.
 
Mchakato wa Katiba mpya ni gharama ambayo inatakiwa kufidiwa na pesa za walipakodi ambao wanategemea kodi itumike kujenga uchumi badala ya kutumika kwa vitu ambavyo haviongezi uzalishaji. Rais Samia yupo sahihi, kujenga uchumi kwanza Katiba baadaye
Katiba ya warioba ipo ni kumalizia mchakato tu kama ilitumia billion 200

Tutashindwa kutenga hata bilion 2 kumalizia ?
 
... uko ushahidi wa wazi kwamba hata Malaika Mkuu Gabrieli aingie CCM ndani ya muda mfupi sana atakuwa polluted tu! Mna haja tena ya kutafuta kujua adui wa nchi hii ni nani?
Adui si mlisema ni dikteta na kafariki?

Sasa mnabweka bweka nini?
 
Mchakato wa Katiba mpya ni gharama ambayo inatakiwa kufidiwa na pesa za walipakodi ambao wanategemea kodi itumike kujenga uchumi badala ya kutumika kwa vitu ambavyo haviongezi uzalishaji. Rais Samia yupo sahihi, kujenga uchumi kwanza Katiba baadaye
Uchumi ni Endelevu sio swala la Mwaka mmoja au miwili hivyo hakuna Siku tutasema sasa Uchumi wetu umekuwa tuache kushughulikia Uchumi tushughulikie Katiba.

Serikali ina Matumizi Makubwa yasiyo ya Lazima Pesa nyingi za Walipa KODI Zinaishia huko kwa Mfano Mishahara ya Wabunge 400,DC 140,Das140,Ded 200 na Magari yao Unatarajia UCHUMI Uwe Mzuri?
 
Back
Top Bottom