Askofu Benson Bagonza: Kuweka nchi sawa ni kazi isiyoisha

Askofu Benson Bagonza: Kuweka nchi sawa ni kazi isiyoisha

Mheshimiwa rais Samia naomba ukipata muda upitie hii kanuni ya kisayansi iiywayo:
Heisenberg's Uncertainty Principle.
 
Samahani, hongera askofu kwa kumpongeza mama Samia, ila day akitokea kiongozi yoyote ambae ataongoza nchi kibabe msiache kuongea ukweli pia kumwambia ukweli
Bagonza unamjua au unamskia unachoongea wewe ni past tense tulishatawalia na dikteta bagonza aliongea Sana hakunyamaza Kama viongozi wengine wa dini unless ndio unamskia leo.
 
Askofu Dkt. Benson Bagonza, Askofu Mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe

"Nampongeza mama kwa "100 kwanza". Namwombea "100 tena" zenye maono mapana zaidi"

"Haki na uhuru ni misingi imara ya kuweka nchi sawa. Ukiyaahirisha unajitwisha mzigo mzito. Dai la katiba mpya lina faida kubwa kwa Rais kuliko kwa taasisi nyinginezo. Katiba mpya ni dawa si kikwazo"

"Uhuru wa kisiasa ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi. Ukiahirisha maisha ya siasa, umesimamisha ukuaji wa uchumi. Tufikiri upya"

"Aliyepita alifanya mambo. Huyu amefanya mambo kwa siku 100 yakafurahisha. Akija mwingine kwa mazingira ya alivyokuja huyu (hatuombei), naye aondoe haya na kuleta mengine? Tutamaliza lini?"

"Kuweka nchi sawa kwanza" ni kazi isiyoisha na ni ya kila siku. Nchi huwekwa sawa kwa kutumia katiba na sheria si kwa kuahirisha matumizi ya katiba na sheria"

"Unapoanza kuahirisha matumizi ya Katiba/sheria unakuwa umekabidhi nchi iongozwe na mtu au kundi. Madhara yake ni haya: Hata wawekezaji hawawezi kukuamini kwa sababu hawajui kesho utaamua nini? Usalama wa mitaji huletwa na sheria siyo matamshi wala ahadi"

"Kulikuwa na tetesi kuwa watu fulani walijaribiwa kuahirisha katiba wakati wa msiba ili kwanza tuzike. Huwezi jua waliwaza nini na ahirisho hilo. Nani ajuaye labda walikuwa na kigugumizi cha kumpokea mama?"

"Hivi karibuni pia tumeshuhudia haya: Kukamata watu na kuwaweka ndani bila utaratibu kwa sababu tuko kwenye vita ya kiuchumi na huko nyuma "tumepigwa sana"

"Hivi karibuni tumeshuhudia haya: 1. Kuzuia mikutano ya kisiasa ili kwanza "kunyoosha nchi". 2. Kuzuia nyongeza mishahara ili kwanza kukamilisha miradi ya kimkakati. 3. Kuzuia upandishaji wa madaraja na vyeo kazini ili kwanza tuhakiki mambo"

"Ni hatari kuahirisha(suspend or postpone) matumizi ya sheria na katiba katika kuongoza nchi kwa sababu yoyote ile. Tawala za kijeshi ndizo zenye tabia hii. Tawala za kiraia huweza kufanya hivyo wakati wa vita au hali ya hatari kwa ruhusa maalum ya bunge
Piga spana
 
Mchakato wa Katiba mpya ni gharama ambayo inatakiwa kufidiwa na pesa za walipakodi ambao wanategemea kodi itumike kujenga uchumi badala ya kutumika kwa vitu ambavyo haviongezi uzalishaji. Rais Samia yupo sahihi, kujenga uchumi kwanza Katiba baadaye
Mawazo finyu.
Bunge linaendeshwa kwa kodi zetu, mahakama nayo inategemea kodi zetu sasa tuseme kwa vile tunahitaji kujenga uchumi basi Bunge, mahakama zisimame mpaka miradi ikamilike?
 
Well said Doctor!

Ni kweli kabisa kazi ya kuweka nchi sawa ni kazi isiyoisha. Hata Biden anahangaika kuiweka nchi sawa huko USA baada ya vurugu za Trump ...!

Vile vile Trump alidai anaiweka nchi sawa baada ya Obama ....... Same as Obama alidai anaiweka nchi sawa baada ya Bush .....!!

Badala ya Mama kuja na story aseme tu nini msimamo wake .....!!
 
Samahani, hongera askofu kwa kumpongeza mama Samia, ila day akitokea kiongozi yoyote ambae ataongoza nchi kibabe msiache kuongea ukweli pia kumwambia ukweli.
Labda wewe humjui Bagonza.

Enzi za mwendazake mbona alikuwa anaweka nondo Kama kawa .

Maza aelewe soon ataanza pita kwenye mstari wa mwendazake watu hawatakuwa nae Tena .

Watu wanataka Uhuru ukiwanyima hata ukiwapa mishahara na posho na marupurupu watakulaani tu watataka siku yako ya kuondoka ifike haraka unawachosha tu .

Ameanza vizuri Ila anaelekea kubaya
 
Mchakato wa Katiba mpya ni gharama ambayo inatakiwa kufidiwa na pesa za walipakodi ambao wanategemea kodi itumike kujenga uchumi badala ya kutumika kwa vitu ambavyo haviongezi uzalishaji. Rais Samia yupo sahihi, kujenga uchumi kwanza Katiba baadaye.
Tuna katiba ya warioba Ina maoni na mapendekozo toka kwa wananchi .

Kinachoweza fanyika Ni marekebisho machche then itakapigiwa kura na wananchi na ikaanza tumika rasmi .

Sidhani Kama Kuna gharama kubwa naa tulishaingia gharama kwenye mchakato wa awali ambao hatukufika hitimisho.

Mwambieni mama katiba MPYA Ni hitaji la wakati sio hisani yake .

Tanzania ili iendelee mwarobaini wake Ni KATIBA MPYA.

ashupazaye shingo huvunjika.
 
Mchakato wa Katiba mpya ni gharama ambayo inatakiwa kufidiwa na pesa za walipakodi ambao wanategemea kodi itumike kujenga uchumi badala ya kutumika kwa vitu ambavyo haviongezi uzalishaji. Rais Samia yupo sahihi, kujenga uchumi kwanza Katiba baadaye.
Kama huna muongozo kamwe huwezi kufikia huo uchumi imara.mambo mengine ni porojo tu za wana siasa.
 
"Ni hatari kuahirisha(suspend or postpone) matumizi ya sheria na katiba katika kuongoza nchi kwa sababu yoyote ile. Tawala za kijeshi ndizo zenye tabia hii. Tawala za kiraia huweza kufanya hivyo wakati wa vita au hali ya hatari kwa ruhusa maalum ya bunge"Askofu Dk.Benson Bagonza
Kwa kifupi Mama kachemsha, sijui ndio KUDEMKA huko
 
Mama ni mzanzibar hawajui watanganyika vizuri... kadri unavyowanyenyekea watataka kukupanda kichwani ... kila unavyoangaika uonekane mwema wenzio wanakudharau ... MBWA ANATAKIWA APELEKWE KIMBWAMBWA
 
Ngoja sasa na hili la korona ulazimishwe lockdown na mbowe
 
Back
Top Bottom