Askofu Benson Bagonza: Kuweka nchi sawa ni kazi isiyoisha

Askofu Benson Bagonza: Kuweka nchi sawa ni kazi isiyoisha

Nadhani wengi wenu hamjatafakari kauli ya SSH kwa umakini ,hivi mnadhani ni kazi ndogo kuweza kurudisha nchi kwenye mstari kwa hali tuliokuwa tumefika?

Swala la katiba mama ameshalikubali ila msilazimishe ashughulikie katiba wakati wenu mnaotaka ,bado ana mika taktibani kumi na amini hatamaliza muda wake bila uwepo wa katiba mpya.
 
Mama ni mzanzibar hawajui watanganyika vizuri... kadri unavyowanyenyekea watataka kukupanda kichwani ... kila unavyoangaika uonekane mwema wenzio wanakudharau ... MBWA ANATAKIWA APELEKWE KIMBWAMBWA
Zinakutosha kichwani
 
Uchumi ni Endelevu sio swala la Mwaka mmoja au miwili hivyo hakuna Siku tutasema sasa Uchumi wetu umekuwa tuache kushughulikia Uchumi tushughulikie Katiba.

Serikali ina Matumizi Makubwa yasiyo ya Lazima Pesa nyingi za Walipa KODI Zinaishia huko kwa Mfano Mishahara ya Wabunge 400,DC 140,Das140,Ded 200 na Magari yao Unatarajia UCHUMI Uwe Mzuri?
hamjawai kuridhika nyie, mbna magu alinarbu kubana maazi ya mambo na kupunguza ukubwa wa wizara mbalimbali kwa kuziunganisha il kupunguza upotevu wa pesa, na mengi alfanya kama kuondoa ama kusimamusha baazi ya sherehe za kitaifa, na zile fedha kuzielekeza ktk maendeleo, na watu mlipinga sana, sasa mishahara ya wabunge ikibanwa huko na kuingilia ajira za watu huko huoni kuwa kuna bomu jipya ltalipuka,...hii point yaki ishafanyika sana haina maana
 
Samahani, hongera askofu kwa kumpongeza mama Samia, ila day akitokea kiongozi yoyote ambae ataongoza nchi kibabe msiache kuongea ukweli pia kumwambia ukweli.
Labda kama umezaliwa Leo humjui...Dr Bagonza
 
Hapa tatizo ni kurasmisha wazo la kikundi Cha watu wachache kutekeleza mawazo Yao huku wakisingizia kwamba hayo ni matakwa ya wananchi wote.

Kuna kila sababu za kikundi chochote chenye fikra chanya kipate kibali kwanza kutoka kwa wale wanaodhani hitaji lao ni hilo wanalolipigania vinginevyo miruzi mingi itavuruga wananchi.

Kwa bahati nzuri Jambo la Katiba siyo geni nchini pia tunamifano mingi ya nchi zilizofanya mabadiliko kuona kama Kuna tija ya kiwango gani.

Harakati za kisiasa mara kadhaa zimekuwa zikituacha hoi wananchi mfano harakati za uhuru zilimalizika kwa mafanikio makubwa lakini baada ya uhuru nchi nyingi zilidumaa kwasababu hawakuwa na dira nyingine zaidi ya kupata uhuru.

Je,nikweli Kuna mtu hapendi Katiba mpya kwa Nia ovu?
Nia Yao ovu ni ipi ni muhimu tutafari upande huu unaopendekeza kuanza na vipau mbele vingine badala ya Katiba kama Wana Nia ovu au la.

Ni hatari Sana kuwa na watu ambao watashinikiza matakwa Yao yatimie kwasababu wanauwezo wa kushawishi wafuasi wao.

Makundi haya mawili ni muhimu yakaweka hoja wasizokubaliana Mezani ili zijadiliwe kwa mapana na kuachana na tabia ya Mwamba ngoma.
 
Mchakato wa Katiba mpya ni gharama ambayo inatakiwa kufidiwa na pesa za walipakodi ambao wanategemea kodi itumike kujenga uchumi badala ya kutumika kwa vitu ambavyo haviongezi uzalishaji. Rais Samia yupo sahihi, kujenga uchumi kwanza Katiba baadaye.
Hu kuwa na akiri basi. Askofu amesema uongozi wa kisheria yaani katiba mpya huweza kuwafanya wawekezaji waje kwa kujiamini kwamba kuna mfumo imara. Je uwekezaji siyo uzalishaji?

Na je kwa kuacha kuwa na katiba mpya huoni uzalishaji ndo unaporomoka kwa sababu wawwkeza watakimbilia nchi zinazozwa na sheria na uhuru wa siasa kama kenya?
 
Hii nchi haiwezi kuwa Sawa kwa kipindi Chake hata miaka 20,nchi tunaijenga taratibu hata kama anataka kufanya kila kitu haiwezekani,kama kwa miaka 60,ccm wameishindwa kuweka nchi Sawa,ataweza vipi kwa miaka 10.
 
UKUU WA KATIBA NA SHERIA.

Ni hatari kuahirisha (suspend or postpone) matumizi ya sheria na katiba katika kuongoza nchi kwa sababu yoyote ile. Tawala za kijeshi ndizo zenye tabia hii. Tawala za kiraia huweza kufanya hivyo wakati wa vita au hali ya hatari kwa ruhusa maalum ya bunge.

Hivi karibuni tumeshuhudia haya:

1. Kuzuia mikutano ya kisiasa ili
kwanza "kunyoosha nchi".

2. Kuzuia nyongeza mishahara ili
kwanza kukamilisha miradi ya
kimkakati.

3. Kuzuia upandishaji wa madaraja
na vyeo kazini ili kwanza tuhakiki
mambo.

4. Kukamata watu na kuwaweka
ndani bila utaratibu kwa sababu
tuko kwenye vita ya kiuchumi na
huko nyuma "tumepigwa sana".

5. Kulikuwa na tetesi kuwa watu
fulani walijaribiwa kuahirisha
katiba wakati wa msiba ili kwanza
tuzike. Huwezi jua waliwaza nini
na ahirisho hilo. Nani ajuaye labda
walikuwa na kigugumizi cha
kumpokea mama?!

Unapoanza kuahirisha matumizi ya Katiba au sheria unakuwa umekabidhi nchi iongozwe na mtu au kundi. Hatari zake zinajulikana. Madhara yake ni haya:

1. Hata wawekezaji hawawezi kukuamini kwa sababu hawajui kesho utaamua Nini? Usalama wa mitaji huletwa na sheria siyo matamshi wala ahadi.

2. "Kuweka nchi sawa kwanza" ni Kazi isiyoisha na ni ya kila siku. Nchi huwekwa sawa kwa kutumia katiba na sheria si kwa kuahirisha matumizi ya Katiba na sheria.

3. Aliyepita alifanya mambo. Huyu amefanya mambo kwa siku 100 yakafurahisha. Akija mwingine kwa mazingira ya alivyokuja huyu (hatuombei), naye aondoe haya na kuleta mengine? Tutamaliza lini?

4. Uhuru wa Kisiasa ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi. Ukiahirisha maisha ya siasa, umesimamisha ukuaji wa uchumi. Tufikiri upya.

5. HAKI na UHURU ni misingi imara ya kuweka nchi sawa. Ukiyaahirisha unajitwisha mzigo mzito. Dai la katiba mpya lina faida kubwa kwa Rais kuliko kwa taasisi nyinginezo. Katiba mpya ni dawa si kikwazo.

Nampongeza mama kwa "100 kwanza". Namwombea "100 tena" zenye maono mapana zaidi.

Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza
 
Enzi za meko alikua wapi? Tumewaskia kina mdude, Tundu Lissu, Lema, Sugu, Fatma karume, Maria Sarungi, Jaji warioba nk but yeye kaja juzi
Ndio maana nakwambia huenda umezaliwa leo au ulikuwa unasoma sana taarifa za Bashiru na polepole
 
Vyote hivi vinatakiwa viende sambamba au kimojawapo kisubiri kwa maslahi mapana ya nchi?
Hakuna maslahi mapana ya nchi kama kuwa na katiba nzuri yenye kujenga taasisi imara kwa ajili ya maendeleo endelevu na sio hii ya kutegemea hisani na maamuzi ya mtu mmoja
 
Back
Top Bottom