Askofu Benson Bagonza (PhD) azungumzia kilichoitwa “Kongamano la Viongozi wa Dini” Dar es Salaam

Askofu kapiga maneno machache mazito. Hoja imeshiba na imejitosheleza hasa.Hakuhitaji mlolongo wa meno marefu kujibu hoja.Nenda nawewe kajifunze labda tutapata matunda yako siku za usoni.
Aisee huyu bishop sijui mwalimu wake wa fasihi bado yuko hai ?!. Nataka nikafanye tuition kwake.

Hawa ndiyo maaskofu . Siyo wasaka fursa [emoji110][emoji120]
 
Yaani maandiko yake huwezi mpeleka popote, anagonga ukweli mtu.

Ni sawa na jiwe linadondoka toka angani na kumdunda mtu kisawasawa...mtu anabaki kulia tu hajua nani kalirusha.

Naifurahia sana falsafa...unaambiwa utajihukumu mwenyewe.

Yupo vizuri sana anaitendea haki Phd yake.
 
Hilo sio kongamano la viongozi wa dini ni kongamano la wajasilia dini ,hawapotezi fursa za awamu ,hongera muandaaji shehe ubwabwa Alhadi na mhasibu wa hazina kutekeleza fedha za walipa Kodi wa Tanzania.
 
"Tuache kuhukumu wengine kwamba wanachanganya DINI na SIASA. Kongamano hili halijachanganya DINI na maharage"
 
-Mungu halindwi, analinda
- Mungu habebwi, anabeba
- Mungu haamrishwi, anaamrisha
- Mungu hamilikiwi, anamiliki
- Mungu si tukio ni mchakato.

Haya ni maoni yangu, nawe una yako. Uwe na AMANI katika Mambo yako Kama nilivyo na AMANI na Mambo yangu.![emoji1548][emoji1548][emoji1548][emoji1548][emoji1534][emoji1534][emoji1534][emoji1534]
 
Huyo askofu wa Ajira wala hatusumbui kwa sababu ni wa mwilini na si wa kiroho.

Hata shetani ana maaskofu wake pia
 
No 3 hapo
 
Looh 🤔🤔🤔🤔
 
Inafaa sisi watanzania kujenga umoja ili kila mwananchi ajisikie kuwa sehemu ya taifa lake. Lakini, tukiwabagua wengine, na kuwafanya wajisikie kuwa wao si sehemu ya taifa lao, basi, ni rahisi hao kujiunga na adui na hatimaye kuisaliti nchi yao.
👍
 
Watanzania nadhani ingekua ni jambo jema sana wakaibuka watu au taasisi isiyo ya kisiasa ikawaunganisha watu kwa mamilioni tukachanga mihela ,vihela na hela tukamtunuku Askofu DR. BAGONZA medali ya Haki ,Utu na Uzalendo. Mwingine anayestahiki medali ni Shekhe Ponda. Kuzungumzia haki na Usawa ni jambo gumu sana kwa watawala tangu mkoloni.

Wanachoshindwa kuelewa wanaCCM ni kimoja ,kuwa haki kamwe haitakuja kuwa ni jambo la mwisho badala ya la Kwanza.

Watawala wanaounda Serikali tangu Mkoloni wanafanana na wanatamani waishi milele na watawale milele na watukuzwe na kila MTU ama kwa hiyari au kwa lazima. Wasipofungwa breki wanageuka kuwa miungu na wakishakuwa miungu basi hakuna wa kuwadai haki wala kuwauliza jambo lolote .
 
Ni kiongozi gani wa biblia alikuwa anajikombakomba kwa watawala kama viongozi wetu wa dini wa leo?

Hivi ninyi mnasoma biblia gani?
 
Nami nimeshtushwa: Hakuna Kiongozi kati ya wote waliohudhuria aliyelaani "Tukio la Kushambuliwa kwa risasi kwa lengo la kuuliwa" mmoja wa watia nia kiti cha Urais 2020. Hili tukio lilipaswa kukemewa kwa nguvu zote kama lengo la kile kikao ni " Kuombea Amani"!!
 
Kunywa maji mwanangu uendelee kutafuna
Uyu hana jipya,ni wa kupuuza tu.aliamasisha maandamano alafu akajificha na wafuasi wake nao wakamshtukia nao hawakukusanyika.
 
Tuache kuhukumu wengine kwamba wanachanganya DINI na SIASA. Kongamano hili halijachanganya DINI na maharage...

Hapa Baba Askofu umewapiga mawe makubwa duh.. Haaa😅
 
Kwenye nondo hizi lazima praise team wanune
 
Uyu hana jipya,ni wa kupuuza tu.aliamasisha maandamano alafu akajificha na wafuasi wake nao wakamshtukia nao hawakukusanyika.
Uwe unaona aibu sometimes ndio nyie mashabiki maandazi unaonekana kabisa ni empty mind bro ficha ujinga wako tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…