Askofu Benson Bagonza (PhD) azungumzia kilichoitwa “Kongamano la Viongozi wa Dini” Dar es Salaam

Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
________
Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao.

2. Nyakati za uchaguzi huwa kuna kutumiana. DINI kuitumia serikali au serikali kuitumia DINI. Lakini Mungu yuko pande zote na hatumwi wala hatumiwi bali ANATUMA.

3. Taifa linaunganishwa na kamati za AMANI na HAKI. Waandaaji wa kongamano wamesema hili ni Kongamano la AMANI. Wanaotaka HAKI wasubiri jingine.

4. Uchaguzi maana yake ni kuchukua kimoja kati ya vingine. Tusichukiane kwa mtu kuutumia Uhuru wake kuchagua anachopenda. Kila mtu aheshimu uchaguzi wa mwenzake. Tuache kuhukumu wengine kwamba wanachanganya DINI na SIASA. Kongamano hili halijachanganya DINI na maharage.

5. DINI si mali za viongozi, Vyama si mali ya viongozi na Serikali si mali ya viongozi. Lakini vyote (DINI, vyama na serikali) havimmiliki Mungu. Hata hivyo Kongamano limemtanguliza Mungu. Inapendeza, lakini wakumbuke:
-Mungu halindwi, analinda
-Mungu habebwi, anabeba
-Mungu haamrishwi, anaamrisha
-Mungu hamilikiwi, anamiliki
-Mungu si tukio ni mchakato.

Haya ni maoni yangu, nawe una yako. Uwe na AMANI katika Mambo yako Kama nilivyo na AMANI na Mambo yangu.!
 
*Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe kuhusu kilichoitwa Kongamano la Viongozi wa Dini*
________
Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao...
1 SAM. 29:5

Je! Siye huyo Daudi, ambaye waliimbiana habari zake katika michezo, wakisema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake?

Kongole Baba Askofu, kwa kuwa Watanzania wanahitaji vyote haki na amani, lkn si utulivu vile ambavyo kusanyiko la leo la viongozi wa kidini walivyotaka kutuaminisha.
 
*Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe kuhusu kilichoitwa Kongamano la Viongozi wa Dini*
________

Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao...
Delete ccm Oct 28
 
Hivi kuna tofauti kati ya wale waliokutana pale uhuru kwenye the so called tanasha la CCM na huu unaitwa mkutano wa viongozi wa dini!

Nimesikia hata shetani humuomba Mungu kwa nguvu kuliko hata Binadamu wanafiki
 
*Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe kuhusu kilichoitwa Kongamano la Viongozi wa Dini*
________

Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao...
Huyu ndo kiongozi wa dini aliyebaki na wenzake wachache sana akiwemo Askofu Mwamakula, Sheikh Ponda na huyu aliyeanza kujirudi saivi Father Kitima.

Wengine wote kama hawa waliokutana leo Eti kumuunga mkono Magufuli wote ni wafanyabiashara wa dini na sio viongozi wa dini!
 
*Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe kuhusu kilichoitwa Kongamano la Viongozi wa Dini*
________

Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao.

2. Nyakati za uchaguzi huwa kuna kutumiana. DINI kuitumia serikali au serikali kuitumia DINI. Lakini Mungu yuko pande zote na hatumwi wala hatumiwi bali ANATUMA...
Ubarikiwe
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
________
Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao...

Duuh, this is too philosophical...

Wachache watakuelewa ndugu Bishop.

Otherwise, wewe ni mtu wa pekee sana. Mungu amekupa akili, maarifa na busara ya kutosha, mshukuru sana Mungu muumba wako....
 
*Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe kuhusu kilichoitwa Kongamano la Viongozi wa Dini*
________

Watu wengi wameniuliza sana kuhusu kongamano la viongozi wa DINI. Siwezi kumjibu kila mtu peke yake. Maoni yangu ni haya:

1. Hakuna DINI inayoiwakilisha nyingine. Wasikilizeni walioenda. Msiwapuuze ambao hawakwenda maana nao wana DINI zao...
HAKIKA WEWE NI ASKOFU WA KWELI
 
Huyu ndo kiongozi wa dini aliyebaki na wenzake wachache sana akiwemo Askofu Mwamakula, Sheikh Ponda na huyu aliyeanza kujirudi saivi Father Kitima.
Wengine wote kama hawa waliokutana leo Eti kumuunga mkono Magufuli wote ni wafanyabiashara wa dini na sio viongozi wa dini!

Absolutely, Yes...

Sisi hatuwahukumu lakini tunaona wayafanyayo na tunayasema hayo....
 
Huyu askofu anampenda Mungu na ni mtumishi wake kweli kweli,Hana unafiki Kama wale walioanza kampeni ya chama Cha mbogamboga kule Dar leo.
 
Amani kwanza ndo haki ipatikane.bila amani akuna haki. Lissu kesha andaa watu wa kuvuruga amani baada ya uchaguzi,kasema yeye mwenyewe ataingia barabarani...
Acha kupotosha jambo ambalo liko wazi.Haki ndiyo inayozaa Amani. kwahiyo haki ndiyo inayotangulia kisha inafuata Amani.Kamwe huwezi kuhubiri Amani kisha ndo uje utende haki.Unapaswa utende haki kisha Amani itazaliwa. Na Amani haijadiliwi kwasababu sio kitendo,kitendo ni Haki.Kwahiyo haki ndiyo ya kuijadili ili itoe matunda ya Amani.
 
Naunga mkono hoja na Tanzania tungekuwa na viongozi wa dini wenye msimamo kama 20 hakika tungekuwa mbali maana hawa wengine ni walamba viatu
Ungemuelewa vyema usingeandika hayo.
 
Asante Baba Askofu,Hili ni Kongamano la Leo limechanganya dini na Maharage[emoji3]
 
Ameongea vizuri ila kumbuka, huwezi kutenganisha dini na serikali, pia huwezi kutenganisha siasa na watu. Kila mmoja ana mtegemea mwenzake
Ndiyo maana kasema " wasikilizeni walioenda" nae alilijua hilo.
 
Back
Top Bottom