Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

View attachment 1703071

View attachment 1703070

View attachment 1703379

====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:

Hivi ni lini polisi wa nchi hii wataacha kufanya kazi kwa misingi ya kitutusa?
 
Yohana Mbatizaji, Alikatwa kichwa kwa kumtuhumu Mfalme Kumchukua mke wa ndugu Yake, na Yesu Akanyamaza kimya.

Unajua kwa nini Yesu Alinyamaza kimya? Tafakari utapata Majibu.

Nikwa sababu Yohana Hakutumia hekima kumweleza Mfalme juu ya Kosa la kumchukua mke wa Ndugu Yake.

Hivyo watumishi wa Mungu, wajue Hekima ni njema ikitumika kufikisha ujumbe kwa Viongozi.

Hakuna kiongozi hasiye shaurika au kuchukua Mawazo ya watu lakini inategemea na jinsi unavyotumia Hekima kuwasilisha hoja yako ndicho kilicho mponza Yohana Mbatizaji.
 
Hivi ni lini polisi wa nchi hii wataacha kufanya kazi kwa misingi ya kitutusa?
Kwa akili zako ulitaka polisi wamvike Nishani?,au ulitaka wampigie vinanda na vinubi?, lini watanzani tumekaa tukamtuma mwamakula kuwa tunahitaji katiba mpya?
 
Bora aliwahi kupost kabla hawajampora simu na kusepa nae. Otherwise angepotea kwa siku kadhaa huku akipokea kipondo heavy huko mafichoni

Hii “terror squad” ya mtu flani ni shida kwelikweli
Mataga mmoja amesema humu kuwa walichelewa kumkamata. Kweli, kwa kujipendekeza kwa Mambosiasa, ilitakiwa akamatwe hata kabla hajaingia mtandaoni. Kazi tukutu ya intelligensia!
Naye alijua atakamatwa. Alijua kama anatumia mtandao wa Voda, wenyewe watazima akamatwe bila taarifa kusambaa. Voda ya kazi tu yanafurahisha. Hivyo aliandika ujumbe bila ya kuweka tarehe. Kaupeleka kunako. Nao bila ajizi waliposikia tu wakatoa huo ujumbe wake. Unakuwa na uzito maradufu kusomeka NIMEKAMATWA kuliko AMEKAMATWA. Ukimwangalia na kumsikiliza anachoongea Mambosiasa unajua kabisa ni uozo mtupu. Sheria hakuna na mantiki ni mfu. Akili ni ile ya nywele tu. Tena taahira ana msitu wa nywele. Weledi, akili, busara na maarifa ni msamiati tosha. Geshi letu!
 
Akimaliza tu kusali anaota mshipa yeye mwenyewe chezea wazee wa ziwani weye
Ziwa gani hilo? Lile la moto? Wapambe hawana akili kabisa. Wachawi wanajua nguvu ya maombi. Wewe mshirikina upo upo na chezea wazee wa ziwani weye. Acha uzwazwa we mshirikina. Hakuna ujualo ziaidi ya tawire!
 
Yule askofu wa katoliki Kayanga kazuiliwa nyumbani
FB_IMG_1613419788423.jpg
 
Ziwa gani hilo? Lile la moto? Wapambe hawana akili kabisa. Wachawi wanajua nguvu ya maombi. Wewe mshirikina upo upo na chezea wazee wa ziwani weye. Acha uzwazwa we mshirikina. Hakuna ujualo ziaidi ya tawire!
Si ajaribu sasa uone
 
'wakutanapo wawili na kulitaja jina langu, nami nipo'
Mkutanapo wawili kulitaja jina la Mungu si lazima mmoja wenu ajipe uaskofu. Huyu muhuni alikimbia Moravian sababu ya uaskofu.
 
View attachment 1703071

View attachment 1703070

View attachment 1703379

====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:

Haki huinua taifa bali dhambi ni aibu na fedheha kwa taifa.
 
Mkutanapo wawili kulitaja jina la Mungu si lazima mmoja wenu ajipe uaskofu. Huyu muhuni alikimbia Moravian sababu ya uaskofu.
Mhuni ni wewe na sidhani kama una dini.Nadhani wewe ni mpagani tu kama mwenzio.................Na hii mada sidhani kama inakuhusu.Wewe umedandia tu.Muhuni mkubwa.
 
View attachment 1703071

View attachment 1703070

View attachment 1703379

====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.

LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:

Habari nzima ya kusema maandamano ni lazima yapate kibali cha polisi ni kuvunja uhuru wa kikatiba.

#FreeMwamakula
 
Back
Top Bottom