Uchaguzi 2020 Askofu Gamanywa: Mungu amemteua Rais Magufuli kuwa kiongozi wa Tanzania, uchaguzi ni utaratibu wa kikatiba tu!

Uchaguzi 2020 Askofu Gamanywa: Mungu amemteua Rais Magufuli kuwa kiongozi wa Tanzania, uchaguzi ni utaratibu wa kikatiba tu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Askofu Gamanywa amesema kuna watu wanamzushia kuwa yeye ni usalama wa taifa ila kiukweli yeye ni " usalama wa mbinguni"
Anasema yeye huwa habwabwaji kwa sababu yuko well informed na ndio sababu anawataka wampigie kura Rais Magufuli kwa sababu ni mtu mwenye hofu ya Mungu.

Askofu Gamanywa amesema amepokea vitisho kwamba atakiona cha mtemakuni lakini yeye haogopi chochote.

Gamanywa amesisitiza kuwa Rais Magufuli kuidhibiti Corona ni ishara kuwa Mungu wa mbinguni ameshamteuwa kuwa Kiongozi wa Tanzania na tarehe 28 utakuwa ni utaratibu wa kutekeleza matakwa ya kikatiba tu.

Uchaguzi huu ni kati ya Baraka na Laana tena ni kati ya Uzima na mauti hivyo watanzania chagueni baraka, chagueni uzima.
Amehitimisha askofu Gamanywa.

Source Shallom tv/ WAPO radio

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom