Uchaguzi 2020 Askofu Gamanywa: Mungu amemteua Rais Magufuli kuwa kiongozi wa Tanzania, uchaguzi ni utaratibu wa kikatiba tu!

Uchaguzi 2020 Askofu Gamanywa: Mungu amemteua Rais Magufuli kuwa kiongozi wa Tanzania, uchaguzi ni utaratibu wa kikatiba tu!

Ni njaa na unafiki mtupu.
Huyo askofu amegeuza madhabahu ya kanisa lake kuwa genge la kuipigia kampeni CCM. Ni mpiga dili fulani mzuri sana. Siku si nyingi nitaleta hapa uchafu wake.

Halafu mkimuona kwenye kile kikundi chao kinachojiita 'kamati ya amani' utamsikia akisema viongozi wa dini hawapaswi kuwapigia kampeni wagombea wa vyama vya siasa.
 
Askofu Gamanywa amesema kuna watu wanamzushia kuwa yeye ni usalama wa taifa ila kiukweli yeye ni " usalama wa mbinguni"
Anasema yeye huwa habwabwaji kwa sababu yuko well informed na ndio sababu anawataka wampigie kura Rais Magufuli kwa sababu ni mtu mwenye hofu ya Mungu.

Askofu Gamanywa amesema amepokea vitisho kwamba atakiona cha mtemakuni lakini yeye haogopi chochote.

Gamanywa amesisitiza kuwa Rais Magufuli kuidhibiti Corona ni ishara kuwa Mungu wa mbinguni ameshamteuwa kuwa Kiongozi wa Tanzania na tarehe 28 utakuwa ni utaratibu wa kutekeleza matakwa ya kikatiba tu.

Uchaguzi huu ni kati ya Baraka na Laana tena ni kati ya Uzima na mauti hivyo watanzania chagueni baraka, chagueni uzima.
Amehitimisha askofu Gamanywa.

Source Shallom tv/ WAPO radio

Maendeleo hayana vyama!
Huyu hajachanganya dini na siasa. mungu anayemuongelea siyo Mungu Mwenyezi, anamaanisha mungu wa Lumumba.
 
Back
Top Bottom