Askofu Gwajima atangaza mfungo wa kumng'oa AMALEKI katika nchi

Askofu Gwajima atangaza mfungo wa kumng'oa AMALEKI katika nchi

Hiyo nguvu mbona haikusaidia rafiki yake kipenzi asionsoke duniani? Au anajua tu kuangamiza hajui maombi ya kuokoa.
Nani alikuambia mtu kuondoka duniani ndio mwisho wa mambo yake yote? Hata Yesu na Muhammad walishaondoka duniani kitambo.
 
Miaka 60 ya UHURU nchi ni masikini huku wananchi wanalima juu ya ardhi yanye dhahabu, almas, Ruby, mafuta,gesi nk.Yaani wamepigwa upofu aibu sana.
Yaani watz hata kugeuza udongo kuwa tofali za kuchoma au interlocking plus kugeuza udongo kuwa vigae waezeke nyumba waishi pazuri,au kugeuza takataka za plastic kuwa tofali,mbao, vigae vya kuezekea, tiles za sakafu eti nao hawawezi kama sio kufungwa ni nini.
Viongozi wa dini waungane tuvunje maagano ya kipepo yaliyowekwa na washirikina Ili upofu ututoke.
Iweje wageni ndo wanufaika wa madini.
Hahhahaah utaambiwa sio mzalendo
 
Kwani huyo Amaleki katika nchi ni nani? Yaani wafutiwe usajili wao kwa sababu ya huyo Amaleki? What if huyo Amaleki ni wakala wa shetani hapa nchini?
Kama inaleta mgogoro si watu waulize sifa za amaleki kwa wanazuoni wa maandiko, halafu wachague kama amaleki wanamuhitaji nchi hii ama vipi, kwani tatizo lipo wapi,
Maombi kama hayo nchi hii makanisani yanapigwa kila siku , mifungo ipo kila siku, mikesha ya kuombea taifa ipo kila siku,
 
SHERIA IANGALIE UPYA BAADHI YA HAYA MAKANISA AMBAYO HUWA YANACHUKUA MUDA MWINGI ZAIDI KUHUBIRI HABARI ZA CHUKI NA SIASA BADALA YA KULISHA WAUMINI CHAKULA CHA KIROHO UPENDO UMOJA MSHIKAMANO NA KUMLILIA NA KUMSUJUDIA MOLA WETU JUU YA USTAWI MWEMA WA TAIFA LETU NADHANI WIZARA YA MAMBO YA NDANI IPITIE SAJILI ZAO UPYA WAKUMBUSHWE MAJUKUMU YA LESENI ZAO [mpwa wangu simbachawene wakumbushe wana]
Pia tambua kwamba makanisa yanapaswa kujali ustawi wa watu wake kimwili (haki, uhuru na amani) maana bila hivyo kuhudumia roho itakua ngumu. Kwenye kutimiza hayo msisitizo umewekwa zaidi kuhudumia roho maana imeandikwa kamwe hatuwezi kutimiza tamaa za mwili na mwili hushinda na roho. Kuhusika kwa kanisa kwenye siasa ni katika kubalance mahitaji mwili na yale ya roho.
 
... AMALEK WAMEANZA KUTOKA SHIMONI!
1639814110721.png
 
Maswali ya Bibilia yajibiwa
SWALI

Waamaleki walikuwa nani?​

JIBU

Waamaleki walikuwa kabila waliotajwa kwanza wakati wa Ibrahimu (Mwanzo 14: 7). Ingawa Waamaleki hawatajwajwa katika meza ya mataifa katika Mwanzo 10, katika Hesabu 24:20 wanaitwa " wa kwanza kati ya mataifa." Mwanzo 36 inataja wana wa Amaleki, mwana wa Elifazi na mjukuu wa Esau, kama Waamaleki (mistari 12 na 16). Hivyo, Waamaleki walikuwa kwa namna fulani kuhusiana na, lakini tofauti na, Waedomu.

Maandiko yana kumbukumbu ya kudumu ya vita kati ya Waamaleki na Waisraeli na mwongozo wa Mungu wa kuwaondoa Waamaleki duniani (Kutoka 17: 8-13; 1 Samweli 15: 2; Kumbukumbu la Torati 25:17). Suala la Mungu kuwaita watu wake kuangamiza kabila nzima ni swali ngumu, lakini kuangalia historia inaweza kutoa ufahamu fulani.

Kama makabila mengi ya jangwa, Waamaleki walikuwa wahamaji. Hesabu 13:29 huwaelezea kama wazaliwa wa Negev, jangwa kati ya Misri na Kanaani. Wabiloni waliwaita Sute, Wamisri Sittiu, na bamba za Amarna huwaita Khabbati, au "waporaji."

Ukatili wa Waamaleki kwa Waisraeli ulianza kwa shambulio la Refidimu (Kutoka 17: 8-13). Hii inaelezewa katika Kumbukumbu la Torati 25: 17-19 na shauri hili: "Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau!"

Waamaleki baadaye wakajiunga na Wakanaani na kuwashambulia Waisraeli huko Hormah (Hesabu 14:45). Katika Waamuzi walijiunga na Wamoabu (Waamuzi 3:13) na Midiani (Waamuzi 6: 3) ili kupigana vita kwa Waisraeli. Walisababisha uharibifu wa mara kwa mara katika ardhi ya Israeli na ugavi wa chakula.

Katika 1 Samweli 15: 2-3, Mungu anamwambia Mfalme Sauli, "Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."

Kwa kujibu, Mfalme Sauli kwanza anawaonya Wakeni, marafiki wa Israeli, kuondoka eneo hilo. Halafu akawashambulia Waamaleki lakini hakukamilisha kazi hiyo. Akamwacha Mfalme Agagi hai, akajinyakulia mali yake mwenyewe na jeshi lake, na kisha akadanganya ni kwa nini alifanya hivyo. Uasi wa Sauli dhidi ya Mungu na amri zake ni mbaya sana kwamba anakataliwa na Mungu kama mfalme (1 Samweli 15:23).

Waamaleki waliokimbia waliendelea kuvuruga na kuwapora Waisraeli kwa vizazi vilivyofuata mamia ya miaka baadaye. Samweli wa kwanza 30 inaripoti uvamizi wa Waamaleki huko Ziklagi, kijiji cha Yudea ambapo Daudi alimiliki mali. Waamaleki waliteketeza kijiji na wakawachukua mateka wanawake na watoto wote, ikiwa ni pamoja na wake wawili wa Daudi. Daudi na jeshi lake waliwashinda Waamaleki na wakaokoa mateka wote. Hata hivyo, mamia chache ya Waamaleki walitoroka. Baadaye, wakati wa utawala wa Mfalme Hezekia, kikundi cha Washimeoni "waliwaua Waamaleki" waliokuwa wakiishi katika mlima wa Seiri (1 Mambo ya Nyakati 4: 42-43).

Waamaleki wametajwa mara ya mwisho katika kitabu cha Esta ambapo Hamani wa uzao wa Agagi, Uzao wa mfalme wa Waamaleki Agagi, anashiriki katika mpango wa kuwaangamiza Wayahudi wote wa Persia kwa amri ya Mfalme Ahasuero.Mungu aliwaokoa Wayahudi katika Uajemi, hata hivyo, Hamani, wanawe, na maadui wengine wa Israeli waliangamizwa badala yake (Esta 9: 5-10).

Chuki cha Waamaleki kwa Wayahudi na majaribio yao ya mara kwa mara ya kuwaangamiza watu wa Mungu yalipelekea adhabu yao ya mwisho. Hatma yao inapaswa kuwa onyo kwa wote ambao watajaribu kupinga mpango wa Mungu au ambao watalaani kile ambacho Mungu amebariki (tazama Mwanzo 12: 3).
Asante kwa ufafanuzi mzuri kuhusu hao waamaleki.

Ni watu waliowanyanyasa sana waisraeli mpaka waisraeli wakatamani wawafute kwenye uso wa dunia...swali la kujiuliza huyu AMALEKI anayemzungumzia Gwajima ni nani haswa??
 
Back
Top Bottom