Askofu Gwajima: Kawe tuna barabara za urefu wa KM 1400 sawa na Dsm - Kigoma tumepewa fedha ya km 130 tu hii haikubaliki!

Askofu Gwajima: Kawe tuna barabara za urefu wa KM 1400 sawa na Dsm - Kigoma tumepewa fedha ya km 130 tu hii haikubaliki!

Nenda Youtube uone vichekesho. Ameshageuka. Sasa hivi anasema masimamo wa Magufuli kwenye corona utafanya wamarekani wapange foleni kwenye ubalozi wa Tanzania huko kwao kwa nia ya kuomba visa za kuja kuishi Tanzania. Kwa kifupi amesema hakuna watanzania watakaokimbilia tena kwenda Ulaya na USA bali wao ndiyo watapigana vikumbo kuja kwetu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo aliacha uchungaji ili akalielie bungeni, kama kutoka Dar kwenda Mwanza ni zaidi ya km. 1700, inawezekana vipi Dar-Kigoma iwe 1400, au ndo ujanja ujanja wa kutafuta kiki, basi aendelee kubweka huenda hata hiyo 130 akaitafuta kwa tochi....
 
Anaongea sana tatizo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mbunge wa Kawe baba askofu Gwajima amesema jimbo lake la Kawe lina barabara zenye urefu wa takribani kilomita 1400 sawa na umbali wa kutoka DSM hadi Kigoma lakini Tarura wamepewa bajeti ya kukarabati kilomita 130 tu.

Gwajima amesema hii haikubaliki na kuwataka watu wa Tarura kujiongeza kwani wao wanahitaji kupewa fungu kubwa la fedha za ukarabati kuliko Tanroads.

Gwajima alikuwa akichangia hotuba ya Rais Magufuli bungeni jijini Dodoma leo.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
Hebu wapime tena urefu wa hizo barabara maana nina wasiwasi na huo urefu. Yaani jimbo la Kawe lina jumla ya Km 14000 za barabara, mbona ni Km nyingi saana???? Kindly revisit the measurement please!!!
 
..barabara[miradi] zilizoko chini ya Tanroads kitaalamu ni za gharama kubwa kuliko barabara zilizoko chini ya Tarura. kwa msingi huo sio ajabu Tanroads kupangiwa bajeti kubwa kuliko Tarura. Askofu alitakiwa atafute ushauri wa wataalamu kabla ya kwenda kuzungumza bungeni.
 
Hebu wapime tena urefu wa hizo barabara maana nina wasiwasi na huo urefu. Yaani jimbo la Kawe lina jumla ya Km 14000 za barabara, mbona ni Km nyingi saana???? Kindly revisit the measurement please!!!
Umeambiwa 1400km siyo 14,000 bwashee!
 
Zitaje mzee. Pengine kuna mwanafunzi wa Public Economy utampa majibu akikutana na hilo swali.
Hii ni elimu unaweza ipata kwa wajasiria mali, Nunua vitabu soma, hudhuria madasa yao utapata majibu kwa nini Nchi zao nimeendelea na zetu zinadumaa. Nanini Serikali ifanye ili Nchi iwe Tajiri. Kwa mwanafunzi anayetaka majibu kwa ajili ya kufaulu mtihani aende kwa Prof.
 
Wasianze kutoa sababu, mwanzoni ilikuwa inaonekana Wapinzani wanachelewesha maendeleo. Saivi huko Bungeni wapo 99% ni CCM.

Kwahiyo wananchi tunasubiri maendeleo tuliyohaidiwa tu
 
Ile ahadi ya kutupeleka Birmingham imefikia wapi? Tumeshatayarisha passport zetu
 
Hii ni elimu unaweza ipata kwa wajasiria mali, Nunua vitabu soma, hudhuria madasa yao utapata majibu kwa nini Nchi zao nimeendelea na zetu zinadumaa. Nanini Serikali ifanye ili Nchi iwe Tajiri. Kwa mwanafunzi anayetaka majibu kwa ajili ya kufaulu mtihani aende kwa Prof.
Hehehe mjasiriamali atoe majibu ni vipi nchi itashughulikia budget deficit? Hahaha dah
 
Back
Top Bottom