Askofu Gwajima: Nchi imekosa maono, kila Rais anakuja na lake, ipo siku tutajuta

Askofu Gwajima: Nchi imekosa maono, kila Rais anakuja na lake, ipo siku tutajuta

Ukiangalia PLANNING SYSTEM ya Tanzania ipo vizuri sana.
.
Yaani haimtaki kila RAIS aje na mipango yake au mambo yake.
.
Kila Planning kuna kitu kinaitwa INCREMENTAL PLANNING
.
Shida ya kuingiza siasa kwenye maendeleo ndio hii.
.
SHIDA YA KUIPA SIASA NAFASI KUBWA KULIKO UTENDAJI.
Umeongea la maana sana ila vichwa maji kamwe hawatakuja kuelewa ulichoandika.
 
Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe kasema nchi imekosa maono kwa kuwa kila Rais akiingia madarakani anaachana na ya mtangulizi wake, kuongeza hilo kamwe halitaweza kutuletea maendeleo

Gwajima amesema nchi inatakiwa kuwa na mikakati yake ya muda mrefu na kila rais anayeingia madarakani anaongozwa na mikakati na maono hayo na sio kuleta vitu vyake vipya, ama sivyo anaweza akaja Rais wa ajabu ambaye atavuruga kila kitu na hakuna atakeyeweza kumbana kwa kuwa hakuna maono.


Ukimwambia haya basi tuandike katiba mpya, atakuambia barabara, Maji madarasa na upuuzi kibao
 
Gwajima ana hoja

Umemwelewa alichoongea ?
Kila Raisi akija anakuja na yake na kuponda ya mtangulizi wake

Nyerere aliponda ya wakoloni taifisha viwanda,Majumba,biashara mashule ya private nk na kufanya ya umma,Mwinyi akaponda ya Nyerere ,Mkapa akaponda ya Mwinyi,Kikwete akaponda ya Mkapa ,Magufuli akaponda ya Kikwete na Mama Samia anaponda ya Magufuli

Nchi utafikiri kichwa cha mwendawazimu kila Raisi ajaye anajifunzia kunyoa

Tunaposema katiba inampa rais madaraka makubwa kuliko inavyopaswa, na suluhisho lake ni katiba mpya itakayo punguza madaraka ya rais, mnasema wananchi wanataka maendeleo na sio katiba! Ukitaka kucheka mpaka uchanganyikiwe toka enzi za Magufuli kila maendeleo yanayofanyika unaambiwa ni fedha za rais! Kwa sifa hizo za kijinga kila rais ataacha kufanya atakacho ili sifa zimuendee yeye?
 
Marais wote wamefeli ndiyo maana kila mmoja anafanya kivyake. Tungepata Rais mmoja aliyefanya kazi nzuri, angeigwa.
 
Hivi kuhamia Dodoma na Bwawa la Nyerere zilikuwa kwenye ilani ya CCM?
Ndio, kuhamia Dodoma ni tangu miaka ya TANU. Bwawa la Nyerere pia ni maamuzi ya miaka mingi iliyopita ambayo utekelezaji wake ulikuwa unapigwa danadana kila kukicha.
 
Unaona mazuzu haya! Nje ya nchi ndiko maendeleo yanakotokea? Niambia nchi ambayo imeendelea kwa sababu marais wake walikuwa wanasafiri sana nje! Nchi inajengwa na wananchi siyo fedha kutoka nje. Miafika ndiyo tulivyo, kazi kuwaza vya bure tu. Bila shaka wewe asili yako ni kutoka kwenye ule mkoa ambao wakazi wake husambaa nchi nzima kuomba omba ndiyo maana una mawazo fyongo namna hii.
Zuzu ni wewe mkuu, inaonekana umri wako bado ni mdogo na umeanza kufuatilia masuala ya kiuchumi hii miaka ya karibuni.

Kujitegemea ni dhana inayobakia kuwa ni ya kinadharia tu katika kuwapa moyo wananchi na kuwajenga kisaikolojia, ukweli ni kwamba mikopo ndio tunaitegemea kwa kipindi kirefu tangu tuwe taifa huru.

Magufuli aliwadanganya watu wa aina yako kwamba tunaweza kujitegemea, wakati akishuka kutoka jukwaani anawatuma wasaidizi wake wakae na mabalozi na wakubwa wa taasisi za fedha za kimataifa ili waombe pesa.
 
Yani vision za kizazi cha miaka ya 1967 zipewe sheria juu ya kizazi cha miaka ya 2022?!
Binafsi sikubaliani nae kwa sababu amesema hatuna vision wakati kwenye mfano kasema tunayo inayoishia 2025/2026..

Sasa anajua ilianza lini kutekelezwa? Point kuu ingekuwa kwamba hiyo vision itungiwe sheria isiache inaelea.

Mfano Nyerere aliacha tuu kwamba Serikali inatakiwa kuhamia Dodoma,alitunga sheria lakini hakuhamia.

Mwendazake alipohamia katungia sheria kabisaa kwamba hakuna option tena.

So vision zetu tuzipe nguvu za kisheria tusiache option ya utashi wa kisiasa hata kama zipo..
 
Mbna wakati wa kuu la maiblis aliyempa ubunge wa dezo hakunyannyua bakuli lake
Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe kasema nchi imekosa maono kwa kuwa kila Rais akiingia madarakani anaachana na ya mtangulizi wake, kuongeza hilo kamwe halitaweza kutuletea maendeleo

Gwajima amesema nchi inatakiwa kuwa na mikakati yake ya muda mrefu na kila rais anayeingia madarakani anaongozwa na mikakati na maono hayo na sio kuleta vitu vyake vipya, ama sivyo anaweza akaja Rais wa ajabu ambaye atavuruga kila kitu na hakuna atakeyeweza kumbana kwa kuwa hakuna maono.

 
Sio haki vipi wakati tuliona Magufuli akiacha ya kikwete na kufanya yake? Ulikua hujaziliwa au umeamua kujitia upofu?
Hakuacha ya Kikwete, aliendeleza aliposhindwa Kikwete. Haya masuala mfano ya ununuzi wa ndege na upanuzi wa bandari zote yapo kwenye ilani ya CCM alichofanya JPM ni kuhakikisha wanafanyiwa kazi.
 
zungumzia point yake mjibu point aliyosema. ubunge aliupata kwa kura za wananchi mimi moja wapo nilimpa kura yangu na familia yangu na ndugu zangu woote

unajitambua kweli.embu hiko kipindi ulikuwa kaburini au
 
Ndio, kuhamia Dodoma ni tangu miaka ya TANU. Bwawa la Nyerere pia ni maamuzi ya miaka mingi iliyopita ambayo utekelezaji wake ulikuwa unapigwa danadana kila kukicha.
Yaani ulikuwa kwenye ilani ya CCM ya 2015-2020?
Yaani kwa nini kwenye ilani iwe na ujenzi wa reli ya SGR, bwawa la Nyerere, kuhamia Dodoma, kununua ndege ndani ya kipindi kifupi? Bado madaraja na barabara kama ya Kimara- Kibaha

Hao walioandaa hiyo ilani kwa nini waweke mirah mikubwa mingi ndani ya kipindi kifupi. Maana deni la taifa litavuka trilioni 100 muda si mrefu, kisha tuanze kulaumiana
 
Hii nchi haina taasisi kama mataifa mengine ata akijaribu Rais mwingine anaanzia pale pale kwanza sio kukurupuka na mipango yake mipya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani ulikuwa kwenye ilani ya CCM ya 2015-2020?
Yaani kwa nini kwenye ilani iwe na ujenzi wa reli ya SGR, bwawa la Nyerere, kuhamia Dodoma ndani ya kipindi kifupi? Bado madaraja na barabara kama ya Kimara- Kibaha

Hao walioandaa hiyo ilani kwa nini waweke mirah mikubwa mingi ndani ya kipindi kifupi. Maana deni la taifa litavuka trilioni 100 muda si mrefu, kisha tuanze kulaumiana
Ni miradi ya miaka mingi ambayo haikuwa ikipewa kipaumbele. Lakini haina maana kwamba haina umuhimu kwa maisha ya watanzania.
 
Ni miradi ya miaka mingi ambayo haikuwa ikipewa kipaumbele. Lakini haina maana kwamba haina umuhimu kwa maisha ya watanzania.
Mkuu hujaona hatari ya kuanzisha miradi mikubwa mingi kwa kipindi kifupi?

Ushafikiria hadi kumalizia hii miradi deni letu litakuwa kiasi gani? Maana sio kodi za ndani zitaweza kukamilisha
 
Hata mimi nimehangaa. Hapo tunaongelea marais wa CCM. Vipi siku tukipata TLP, CHADEMA, UPDP...?
Hivi kwanini hawa marais wanaoongozwa na ilani ya chama chao lakini bado kila mmoja wao huja na lake na kuacha la mwenzake?

Ina maana hawaifuati ilani ya chama chao?

Kama jibu ni ndio, basi ile kauli ya Kinana kwamba CCM ndio wanaiagiza serikali na sio serikali kuiagiza CCM itakuwa ni batili.
 
Kwani kipi kilicho achwa! Kila siku mama anasema atakamilisha miradi yote, tatizo nini? Ila mambo ya mabavu hayo ameyaacha nami nampongeza kwani si utu na yaliumiza wengi, na si mambo ya maendeleo!
 
Amesema vyema kabisa na ndio inapaswa kua Ila ajabu 2015-2020 alikua akisapoti huo upuuzi..sasa Kama anauona ukweli sasa ni vyema akasimama hapo hapo bila kukwepesha.
 
Bwawa la umeme la Nyerere halikuwepo sio tuu kwenye ilani bali kwenye vision ya 2025/2026.
kasome ilani 2010-15 pia nime attach ktk page ya pili hivyo waweza kusoma ilani zote kuanzia 2005 mpka 2020... utapata kuona vyema series za maendeleo zilivyo pangiliwa vyema...

bila kusahau kuwa vyote viliandikwa kuwa vitatekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha... ukisoma kurasa za mwanzo wa kila ilani utaelewa zaidi pale wanapo toa mjumuisho wa mafanikio ya awamu iliyopita na yaliyobaki yanaingizwa ktk utekelezaji wa awamu mpya au kipindi kipya...

hakuna anaye ingia madarakani anaingia na mpango kazi wake nje ya ilani yetu/zetu...
 
Back
Top Bottom