#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Nje ya mada kidogo, hivi lissu kule ugaibuni amechanjwa ? kama ndio mbona hatujaona picha zake kama wakina hamisi?
 
Ni hali ya hatari kubwa kwa ugonjwa huu unaouwa (ambalo ni tatizo la kisayansi) unapoachwa kufanyiwa siasa au mzaha.

Ni hatari zaidi hali hiyo inapoachwa kuendelea, wakati serikali iliyo na dhamana ya kutulinda, ikiwa imechagua kuwa kama mpenzi mtazamaji tu.

View attachment 1868361

Haiingii akilini ni vipi serikali kutumia nguvu kwenye kongamano la Chadema kwa sababu za kudhihibiti Corona lakini si huyu anayehamasisha watu kutochukua tahadhari!

Kwa mwendo huu wa kuzikumbatia siasa uchwara zenye kuweka maslahi binafsi mbele tungali na safari ndefu sana.

-------
My take:

Uzi huu chini unaihusu sana serikali kwa sasa na hasa mheshimiwa SSH:

Sijawahi kutoa neno kuhusu siasa. Leo hii nina neno. Hili la Josephat Gwajima ni mundelezo wa Sukuma Ngang kuliyumbisha taifa na kumuyumbisha Mh. Rais wa JMT. Kwa hili na simama na serikali yangu. Vyombo vya ulinzi na salama mkiliacha hili lipite hivi hivi itakuwa sawa na hujuma kwa serikali.

Msimamo kuhusu Corona ilishatolewa na serikali naomba tusimame na serikali yetu. Tusiyumbishwe. Kama njisi waliopingana na msimamo wa rais walivyoondolewa CCM huyu naye aondolewe asituvuruge. Ni ushauri kama raia mwema na mzalendo.

Ilikiwachwa kwenda hivi hivi watatuvuruga.
 
Sawa covid ipo, na variants zake and whatever waves we are expecting in the future, hata lije wimbi la 40, ni hivi tutahimiza watu wasichanjwe... hawa watu wametengeneza tatizo ku create fear ili wachome watu masindano(chanjo) bila kuwa na uhakika na content ya hizo chanjo? Kachome wewe na familia yako... wanaopinga sio wajinga kama unavyofikiri, we are well informed and we know exactly what is goin on huko duniani... Tumesoma na kujifunza mambo mengi sana kuhusu hizi chanjo. Wajinga pekee ndio watachoma hizo chanjo.
Una kiwango gani cha elimu?
 
Hapo usinidanganye kuwema wamechanjwa take care ndg.

Umeshasema hatuwezi kuwafikia na sisi as afrikan hatujawai toa mchango wowote, (labda) BUT...

Iyo chanjo kama ina madhara unadhani vile vichupa is serious vina kile kimiminika chenyewe cha k8nga ya covid?.

Wale jamaa ni great thinker na wanatumia akili sana, so usione wanadungana masindano ukadhani ni kinga ya corona NO!.

Kwahiyo kwenye hicho kimiminika kuna nini? Watanzania tuna shida kweli.Dunia inapambana kuutokomeza huu ugonjwa wa corona sisi wabongo tuko busy kudanganyana.eti hatuamini mpaka tuwe na uhakika nayo.haha.chanjo zingine mlizowahi kupigwa mlikuwa na uhakika nazo?mbona bado mnazaliana tu tena kwa wingi na bila shida yoyote.Wazungu wawaue nyie ili iweje? Na wangekuwa na haja hiyo mbona wangeshatuondoa zamani tu.Gwaji boy yeye anatafuta umaarufu,wafuasi na utajiri zaidi kwa sadaka zenu.Sio daktari na hana uwezo na mamlaka yoyote ya kushauri mambo ya taaluma ya afya.anachukulia advantage ya ujinga wa watanzania kupotosha.Anaweza akawa amechanjwa tayari na bado akadanganya watu bado.Wajinga ndio waliwao.We kaa msikilize Gwaji boy corona ikupitie au ipitie ndugu au jamaa zako wa karibu ndio labda utatia akili.The choice is yours and yours alone.Labda tu kwa watakao amua kupata chanjo wahakikishe tu wanapata chanjo kwenye sehemu ambazo zimeidhinishwa na serekali na atleast wanasoma na kueilewa kiaina aina ya chanjo anayopata kabla ya kuipata.Stay safe and be blessed!!
 
Nani kakulazimisha upigwe chanjo? Kama unataka sindano takoni wew sema tu utapigwa bila tatizo
Mbowe anataka tulazimishwe tupigwe chanjo
wote kuwe hakuna hiari na kuna watu humu pia wanataka chanjo iwe lazima.
 
Mbowe anataka tulazimishwe tupigwe chanjo
wote kuwe hakuna hiari na kuna watu humu pia wanataka chanjo iwe lazima.
Una kiwango gani cha elimu ? . ukipewa kazi ya kutathimi kwa wewe ambaye hutachanjwa ndani ya miaka 5 Ijayo utakuwa katika sehemu gani ya kukubalika au kukataliwa kupata huduma yeyote ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. Mfano mdogo tu kusajili kadi ya simu bila kitambulisho cha Taifa au kusafiri bila kadi ya manjano?
 
Una kiwango gani cha elimu ? . ukipewa kazi ya kutathimi kwa wewe ambaye hutachanjwa ndani ya miaka 5 Ijayo utakuwa katika sehemu gani ya kukubalika au kukataliwa kupata huduma yeyote ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. Mfano mdogo tu kusajili kadi ya simu bila kitambulisho cha Taifa au kusafiri bila kadi ya manjano?
Wewe unafikiri hivyo vyitu ni mhimu kuliko uhai wako????
 
Pamoja na yote, tumepoteana zaidi tokea awamu ile. Tulipo ni kama tumemwagiwa petroli. Akitokea mvuta sigara na moto wake karibu inaweza kuwa hatari kubwa.

Walioko madarakani walikuwa na dhamana kubwa ya kuiondoa hali hii wala si kuipalilia.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Kinadharia hilo linawezekana ila hawa Watanzania siyo wa kuikabili serikali na vyombo vyake. DNA yetu haina ujasiri huo hata watufanyie nini. Huo ndiyo ukweli, sorry!
 
Mungu unayemuamini wewe ni tofauti na wa wengine?, kwani kumuanini mungu kunahitaji akili zipi na kukataa chanjo ni kutumia nini?.
Hiyo ni hoja dhaifu, kumbuka hata shetani anamwamini Mungu, hivyo yawezekana kabisa Mungu wangu ni tofauti na wako ndo maana hata mawazo tunapingana kwenye hili!!!
 
Mungu unayemuamini wewe ni tofauti na wa wengine?, kwani kumuanini mungu kunahitaji akili zipi na kukataa chanjo ni kutumia nini?.
Kujua mema na mabaya na kuacha mabaya na kutenda mema, hiyo tu ni akili ya mtu anayemjua Mungu, ni mtu asiye na akili ndo anaamini kwenye barakoa na chanjo!!
 
Una kiwango gani cha elimu?
Well educated than your entire family. Nenda telegram ka join group linaitwa LA QUINTA COLUMNA utapata information kibao kuhusiana na hizo chanjo...na sio group la waswahili ni hao hao wazungu mnao waamini na kuwaabudu.
 
Hiyo ni hoja dhaifu, kumbuka hata shetani anamwamini Mungu, hivyo yawezekana kabisa Mungu wangu ni tofauti na wako ndo maana hata mawazo tunapingana kwenye hili!!!
Unamjua shetani au umepokea mapokeo ya maandiko bila kujua wewe asili yako ni wapi?
 
Back
Top Bottom