Kwakuwa hili ni jukwaa huru, naamini maoni yangu yataachwa bila kuunganishwa na machapisho mengine kwani hayafanani hata kidogo.
Mara baada ya Askofu Gwajima kuuliza maswali ya msingi juzi, nimeona viongozi wengi wamejitokeza kumjibu kana kwamba hana haki ya kutoa maoni. Kimsingi alichosema ndugu Gwajima kina logic sana tu, ila kwakuwa watu wengi wana tabia ya kuamini kila kinachotoka vinywani mwa wataamu basi wanamwona kama vile punguani.
Dr naomba usiyumbishwe, pia watanzania tusikimbilie chanjo, tutumie vyema uhuru tuliopewa kuchagua kuto chanjwa. Tena kama una umri chini ya miaka 45 sikushauri kabisa, sisemi kwamba chanjo ina tatizo, ila katika mambo kama haya nivema kuwatanguliza viherehere halafu unakaa nyuma.
Hebu fikiria kama chanjo hii itasababisha paipu ikalala baada ya miaka 5. Tafakari, chukua hatua. Wazungu wana chanjo zao sio hizi, Hii J&J marekani waliikataa, sisi tunapokea tu kama msaada. Anyway wazungu wanatupenda sana ndomaana walitutawala.
Nasubiri kwa hamu kusikia jinsi mwamba atakavyo jibu mapigo, waliomjibu waandae taulo.