#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona


Wameaminishwa na kina msukuma kuwa hata darasa la 7 ni bora kuliko wasomi.
 
Mbona Nchi haina university Teaching hospital
 


Kuna Watanzania wanapenda ushabiki badala ya kusikiliza Madaktari wa watu wana sikiliza madaktari wa mapambio! Tena eti wenye kudanganya walalahoi wanauwezo wa kusalia watu waliokufa na kufufuka. Wale wanao waambia waumini pesa yao ya mapato asilimia 10% ya zaka inaenda kwa Mungu kumbe inaenda kununua ndege na helikopta binafsi. Tuacheni ujinga wa kusikiliza matapeli tumechoka kufanywa wajinga na huyu jamaa
 
Gwajima ametoa hoja, badala ya kuchangia hoja kwa kukosoa au kuongezea nyama unaanza kumjadili mtoa mada, sasa una akili au matope

Huwezi kuwa na hoja katika eneo usilokuwa na ujuzi nalo. Kwamba wewe umeona hoja ya "microbaolojia na virusi" tokea kwa Gwajima asiyekuwa na mbele wala nyuma kwenye eneo hili? Wewe una akili au matope?

Haya si ndiyo mambo ya nyungu?

Kwenye masuala hayo, tunawasikiliza hawa:

"Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara."

Wenye bahati zao.

Kina Gwajima hata kama wakikaa kimya tu, kwenye masuala haya hawana tofauti na kina msukuma au hata wale very illitrates vijijini ambao hawakwenda shule kabisa.
 
Gwajiboy kaongea point.
Ushauri wake ufanyiwe kazi
Hatutakiwi kuchukulia issue ya chanjo kama fashion lazima tujiridhishe na hii issue iwe ni hiyari ya mtu, isiwe lazima
Nakazia...

HII KITU IWE NI HIARI YA MTU ISIWE LAZIMA hasa kwa sisi watumishi wa ngazi za chini ambao tumekuwa tukifanywa chambo kwa kila kitu
 
What have we done to protect our people from dying ....secondary to HIV,MALARIA,DIABETES,HEART DESEASES AND MATERNAL DEATHS?
 
 
Nchi gani imelazimisha chanjo zake zinunuliwe? Mbona Russia na China wametengeneza za kwao na WHO imewapa endorsement?

Okay unasema vifo laki 5 kwa miaka 70 ni halali ila vifo 50 kati ya watu million zaidi ya 30 waliochanjwa kwa Astra Zeneca ndio sample nzuri ya kudiscredit chanjo?

Kingine chanjo sio tiba na hapa ndio mnakosea.... Chanjo ni kama condom tu inazuia maambukizi ila yakipenya haiwezi kukuokoa tena!! Hata ARVs kuna watu wanatumia na bado wanakufa kwa maradhi ya VVU so its not a big deal to be honest
 
Acha kupotosha watu aliyekudanganya Kenya na Rwanda wamepata shida na chanjo ni nani. Mmemponza ndugu yenu mpaka corona imemla kichwa
 
hivi watalaamu wetu wa ndani wana capacity ya kujua ubora, udhaifu, madhara, faida ya cnanjo zilizopo kwa sasa na years to come?

Hawana uwezo wowote wa kufanya chochote zaidi ya kutuambia waliojifunza kupitia peer review. Kama wanaweza kuwa kimya karibu miezi sita toka habari za chanjo zianze, umuhimu wao haupo tena!! Magonjwa hatari miezi sita inatosha kabisa kuleta madhara makubwa. Ungonjwa huu umeanza 2019, sasa 2021 bado hata hawajasema wamegundua kitu kimoja!!! Wanakuja na ushauri wa NIMCARF, Covidol, nyungu huku wakiita ugonjwa huu “changamoto ya upumuaji”.

Kwa ujumla Gwajima ana point - kama anayosema ndio yangekuwa yanatokea. Tutaingia kwenye chanjo ya covid kama tulivoingia kwenye za polio, dondakoo, surua, kifaduro nk. Hatukufanya utafiti wa hizo!!!
 
Chanjo si unajikinga tu bila kujali ugonjwa upo ama haupo!! Ni precautionary motive tu na ndio alichosema Rais kwamba hata kma Covid Haipo Tz ila wave ikija lazima ikute mmejiandaa.
 
Hivi unajua kuwa wataalamu wanapuuzwa na corona inapelekwa kisiasa zaidi kuliko kisayansi? Kasome kitabu cha Corona False Alarm? Fact and figures.
Mkuu ww hujawahi kuamini Covid 19 ipo..... Nili conclude kwamba utaamini siku Ikimpata ndugu yako wa karibu akafia mikononi mwako ICU bila kupewa chance ya kumuaga ndio utakiri kuwa it's real.
 
Watu washasaini mkataba wa mkopo we unaulizia haya sahizi! Tulieni mtiwe astra zeneca muanze kupuputika!
 
Huyu Mnafiki kwenye yale mabanda yake anayojiita ni kanisa anawadanganya wapuuzi wanaomfata eti Chanjo ya Corona ni Alama ya Mnyama, Mpinga Krist
Health education as primary prevention,drugs priscription(ant malaria,ant dm,ART ,ant hypertensive ) as secondary prevention ,mnx of complications associated mentioned conditions to avoid disiabililities as tertiary prevention
What have we done to protect our people from dying ....secondary to HIV,MALARIA,DIABETES,HEART DESEASES AND MATERNAL DEATHS?
 
Swali ni je, tuna wataalamu au utaalamu wa kutambua chanjo ipi ni salama na ipi si salama? Otherwise naunga mkono hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…