Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima ametaka kuwepo umakini wa kuchagua Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19. Amesema hayo akiwa Bungeni Dodoma leo wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Afya iliyowasilishwa na Waziri Dorothy Gwajima.
Amefafanua, "Mimi sipo kinyume na Chanjo za Corona wala Chanjo yoyote. Mtu asininukuu napinga Chanjo, hapana! Tanzania tulishachanjwa Chanjo ya Kifua Kikuu, Surua, Kifaduro na Polio".
Amesema ni kweli Tanzania ikikataa Chanjo
inaweza kuwekewa zuio la kwenda Ulaya. Ameeleza, "Tunakabiliwa na uchaguzi mbaya sana, tuchanjwe kitu tusichokijua sawa sawa au tusichanjwe tuzuiwe kwenda Ulaya".
Ameiomba Wizara ya Afya kuangalia suala la Chanjo kwa umakini, akisema waangalie madhara ya sasa, ya siku zijazo na ya Taifa. Ameongeza kuwa, tatizo lililopo ni kufikiri kila kinachotoka Ulaya kinafaa.
Amesema, "Before we venture into what kind of vaccine we should take, tunatakiwa tuwe na wataalamu wetu wa hapa".
Hizo chanjo alizochanjwa zamani alizijua na alizifanyia utafiti kwanza kabla ya kuchanjwa na zilimletea madhara gani mpaka aanze kuwa na wasiwasi? Kwenye haya mambo ya kitaalamu lazima tuwe na trust na honesty pia maana hatutawezi kuthibitisha kila kitu. Ndiyo maana tukienda hospitali tukiambiwa tunaumwa na tunatakiwa tutumie dawa fulani ili tupome, tuna'trust' maana hatuwezi kuthibitisha (hatuna utaalamu huo). Huu ni muda mzuri wa kuimarisha urafiki wetu na marafiki wetu wa enzi na enzi na ambao hawajawahi kutufanyia ubaya wowote. Sidhani kama kwa sababu ya Covid-19 wamegeuka kuwa wabaya kiasi cha kuanza kuwatilia mashaka kama ambavyo kauli mbalimbali zilikuwa zikitolewa hapo nyuma. Nilimsikia wakati fulani (kama wiki 2 au tatu zilizopita) kuhusu hizi chanjo, nikashangaa sana. Alikuwa ana'speculate' mambo na nilishangaa sana kuona wahubiriwa walikuwa tu wakipiga makofi na kushangilia na kwa kufanya hivyo aliendelea kuwafunga kamba utadhani alishafanya utafiti wowote wa kumfanya aanze kuzitilia mashaka. Tujitafakari!