Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Katika muendelezo wa hali inayoonyesha kuwasikitisha sana wananchi juu ya uonevu na unyanyaswaji wa dhahiri anaofanyiwa mheshimiwa Lissu nchini. Baada ya Ndugu Lissu kuzuiliwa kuendelea na safari yake ya mlandizi kinyume cha haki yake ya kikatiba, Askofu Mwamakula amekwenda eneo la tukio hapo kibaha ili kumfariji na kumtia Nguvu.
Askofu Mwamakula ameongea kwa huzuni na masikitiko makubwa juu ya aliyotendewa ndugu Lissu na kusema kuwa si vizuri viongozi kutokutenda haki namna hii, Askofu ameonya kuwa hali ya namna hii ya uonevu wa waziwazi juu ya mtu ambaye hajavunja sheria yoyote inaweza kukwaza dhima ya taifa ya maridhiano huko mbele.
Wakati huohuo wananchi wameonyesha kushangazwa na kitendo cha kumzuia mheshimiwa Lissu kuendelea na safari yake wakati yeye ni mwananchi na anazo haki zote za kisheria na kikatiba kwenda mahali popote.
Wakati huohuo muendelezo wa uvamizi wa ofisi za Chadema na shughuli zao umeendelea nchini, hali hii inawatia hofu wananchi hasa wa vyama vya upinzani na kujihisi hawako salama katika nchi yao wenyewe.
Wakati matendo ya watu wasiojulikana yalianza kupungua, wananchi wanashtushwa na utumiaji nguvu wa dhahiri wa jeshi la polisi kuingilia shughuli halali za kisiasa za wananchi.
Hii hali ikiendelea kuna uwezekano wa kutoleta sintofahamu nchini na kwa kweli Polisi hawatakwepa lawama kwa kuvuruga amani ya nchi maana wao wamekuwa ni chanzo kikubwa cha kuchochea migongano isiyo ya lazima.
Tunalitaka jeshi la polisi lisiwe chanzo cha vurugu, liheshimu sheria na lifanye kazi kwa weledi na kwa kufuata miiko ya kazi zao.
Hapa chini ni maelezo ya askofu Mwamakula.