View attachment 1870225
Niwakumbushe wenye madaraka nchi hii
1. Askofu Mwamakula na Sheikh Ponda waliomba dua ya Maangamizi kwa ambao wangeshiriki kuvuruga uchaguzi wa mwaka 2020, Nyote mnaona leo yule mvurugaji mkuu katwaliwa mapema kabisa hata miezi 6 ya kipindi cha pili hakuifaidi
7. Leo Askofu anatangaza dua kuhusu suala la Mbowe.
Hizi dua zichukulieni poa tu, lakini Siyo za kufanyia mchezo.
Zikianza kuwatafuna, msitafute mchawi!
ZABURI 20:7
"...Wengine hujigamba kwa magari ya vita; wengine kwa farasi wao. Lakini sisi tunajivunia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu..."
AMINA, na iwe hivi...!!
Mimi nitashiriki maombi haya kuanzia leo...
Kama watazuia kukasanyika, msipate tabu wala mtu asisikitike...
Na kamwe msilazimishe kukusanyika kimwili kwa sababu watawaumiza kweli kama waseamavyo mara kwa mara...
Ni kwa sababu Neno la Mungu linampa uwezo kila mtu kupigana vita yoyote ya kiroho ikiwemo hii ya kumwokoa ndugu yetu Freeman Mbowe toka midomoni mwa simba efficiently hata ukiwa ndani ya chumba chako..
Kumbukeni hili: "...Mungu ni Roho (siyo mwili) na wote wamuabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli..."
Maombi yoyote katika Mungu aliye hai ni IBADA takatifu...
Hivyo, hii vita tunayoindea ni ya kiroho si ya kimwili...
Hebu soma hapa chini mamlaka na nguvu iliyo katika Neno la Mungu juu ya vita yoyote:
2 WAKORINTO 10: 3 - 5
"....Kweli tunaishi duniani, lakini hatupigani vita kidunia. Maana silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu ya Mungu yenye kuharibu ngome zote za adui. Tunaharibu hoja zote za uongo na kubomoa kila kizuizi cha majivuno kilichowekwa kuipinga elimu (haki) ya Mungu; tunaziteka fikra zote na kuzifanya zimtii Kristo Yesu... "
Sikilizeni ndugu zangu, Hii vita kwelikweli. Ukiingia ktk vita hii kichwa kichwa tu bila kuwa tayari, utaumizwa na tutashindwa vibaya sana...
Neno la Mungu lina sema "kuweni na hekima na busara"...
Lakini pia kila mwombaji NI MUHIMU akumbuke NA LAZIMA avae/abebe silaha zote muhimu ktk vita hii....
Silaha hizo ni soma Biblia katika ;
[ WAEFESO 6: 12 - 19]
In summary, silaha hizo ni:
1. UTAYARI - Kila mtu aamue kweli
2. UKWELI - Kama mkanda kiuononi mwako
3. UADILIFU - Vazi la kivita kujikinga na mashambulizi yote ya adui dhidi yako
4. HAMU YA KUTANGAZA UADILIFU NA HAKI (HABARI NJEMA) - Viatu vya kivita vya miguu yako
5. IMANI - Ngao ya mikononi mwako ya kuzuia/kuzimia mishale ya adui , yule mwovu akitumia mawakala wake.
6. WOKOVU - Ni kama kofia ya chuma (helmet) ya kuzuia majeraha ya mashambulizi ya adui
7. NENO LA MUNGU - Huu ndiyo upanga mkali sana unaomkata kata adui au kwa lugha rahisi ni bunduki yako yenye risasi kumpigia adui popote alipo..
Ndugu zangu, hatuko pamoja kimwili. Lakini katika ulimwengu w roho tuko pamoja bila kujali utakuwa unaomba ukiwa sehemu gani...
Sikilizeni tena hili:
Yesu Kristo anatuambia hivi katika hili;
MATHAYO 18: 20
"...Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika [wamepatana au wamenia pamoja] kwa jina langu, nami nipo hapo hapo katikati yao..."
Sisi hatuko wawili au watatu bali tuko maelfu kwa maelfu Tanzania yote na duniani, na kwa kuwa tumepatana na kunia pamoja, Mungu Yehova katika YESU KRISTO yupo pamoja nasi...!!
MSIOGOPE, AMININI TU...
NB: Nukuu ya maandiko ni kutoka BIBLIA HABARI NJEMA - BHN, toleo la Kiswahili cha kisasa/rahisi..