Askofu Mwamakula: Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan, mambo yafuatayo ni muhimu

Askofu Mwamakula: Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan, mambo yafuatayo ni muhimu

Kwa madudu haya yaliyotajwa na Baba Askofu taifa lilikuwa linajenga ukuta mkubwa sana wa machafuko. Ni wakati muafaka sasa haya yakaangaliwa kwa umakini.
 
Asisahau ajira kwa kada mbali mbali kama ualimu, udaktari na zinginezo ambazo wahitimu wake wamejazana mitaani bila kazi maalumu huku kukiwa na uhitaji mkubwa sana wa madaktari mahospitalini na walimu mashuleni.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Bi mkubwa toa ajira kwa vijana, usiwasahau wafanyabiashara wa bureau de change waliofanyiwa umafia.
 
Kwa hii historia, Magufuli alirisk sana uhai wake kubeba jukumu la kuhudumia wananchi
Ni upendo
Walilifahamu hilo walipopendekeza jina 2015.

Yaonekana kila kitu kilipangwa na yaonekana hata yeye alikuwa akifahamu hilo.

Ila kashikashi za chuki kutoka pande zote za dunia ndizo zimechangia kwa kiasi kikubwa.
 
Uliyoyasema kama msimamizi wa haki aaiuechoka tutayaheahimu Na Mama atayasikia. Amen
 
Kwa hii historia, Magufuli alirisk sana uhai wake kubeba jukumu la kuhudumia wananchi
Ni upendo
Kuhudumia wananchi mbumbumbu na hoya hoya huku akiwatia adabu wote wasio tayari kuburuzwa kifikra!! Huwezi kuua watu na wengine kuwatia gerezani halafu useme eti alijitolea kuhudumia wananchi kwa upendo!

Bwana Yesu hajatoa maagizo ya watu kuwa maadui wa wale wanaodhani maadui wao!! Uhudumu wenye upendo ni ule tulioachiwa na Bwana Yesu na sio huu mnaohubiri nyie kwamba eti alikuwa na upendo!
 
Walilifahamu hilo walipopendekeza jina 2015.

Yaonekana kila kitu kilipangwa na yaonekana hata yeye alikuwa akifahamu hilo.

Ila kashikashi za chuki kutoka pande zote za dunia ndizo zimechangia kwa kiasi kikubwa.
Kwahiyo unataka kutuaminisha kwamba amekufa kwa sababu anachukiwa dunia mzima?! Hivi ni kipi cha kumfanya achukiwe na dunia mzima?! Kati ya marais mbalimbali wa Iran, Syria, North Korea au hata Kagame, ukiwalinganisha wao na Magufuli ni yupi alikuwa anapata kashikashi za wababe wa dunia?! Mbona hawajafa?

Acheni kujitoa ufahamu! Magufuli alikuwa mgonjwa, PERIOD! Na alivyo mtu wa ajabu, mtu anajiona kabisa kwamba spana mkononi halafu analetea ujeuri kwenye mambo ya kiafya! Na kwa kiburi cha Magufuli kuna kila dalili alikuwa hazingatii hata maelezo ya wataalamu wake, na sina shaka hicho ndicho kimemuua na wala sio hizo porojo zenu! Kwa mtu aina yake ungemtarajia awe very careful kwenye korona lakini ndo kwanza akawa mbele kuwajaza ujinga wananchi kwenye suala zima la korona.
 
Hivi maandamano ya amani ya kudai katiba mpya yaliyokuwa yakiratibiwa na huyu askofu yalishafanyika?
 
Askofu amesema yote, cha msingi ambacho mama anatakiwa kukiona mapema ni kuhusu viongozi almost wote waliofanya kazi na Hayati, wameonesha udhaifu mkubwa sana. Ni waongo wa wazi, wana dharau, wana viburi, ni wajeuri na wengi ni wasema hovyo, kwa ufupi hawana karama ya uongozi, labda wanafaa kuwa askari wanyamapori wakapambane na majangili, maana hakuna negotiation kati ya jangili na askari, au wakawe askari magereza napo nina wasiwasi kama hawatakandamiza haki za wafungwa...
Umenena vyema.
 
Mungu mkubwa tunatawala zenji
Na Sisi tunatawaliwa na zenji
Hii ni ngoma droo
Mungu huwa anawasaidia wanyonge na ndio utaamini Mungu yupo
Nani ni best loser hapo ni wewe na akili zako
 
Kama alijijua kuwa Afya yake haiwezi mikiki ya ofisi hiyo kuu baada ya kaumaliza Ngewe yake ya miaka mitano angewaambia CCM kuwa imetosha
Sasa betrii kwenye Moyo na mikiki yote hiyo so kujitafutia kifo
Tatizo lilikuwa kwa waliomzunguka... Bashite, Bashiru, Dotto, na majuha na mataga mengine...
Walifanya kumtanguliza mgonjwa wao ili maisha yawe nafuu kwao...
 
11. Tunashauri utawala mpya uwapandishe madaraja Watumishi wa umma wanaostahili pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote.
Hili ni kati ya mawazo ya hovyo sana katika uongozi wa taifa kiuchumi. Kupandisha mishahara kunasababisha gharama za maisha pia zipande na inflation kuongezekaa nathamani ya shillingi kutelemka; ndiyo mambo yaliyovuruga thamani ya shilingi kutoka dola 1 kwa shilling 5 hadi kufikia leo dola 1 kwa shilingi ~2300+. Kenya wana curreny stable sana kwa sababu hawapandishipandishi mishahara yao kufurahisha wapiga debe.

Hata Marekani mishahara yao imekuwa hivi ilivyo kwa zaidi ya miaka 15; ile 1% -3.5% adjustement ya inflation inategemea sana na namba za iflation mwaka huo, siyo wanasiasa kusema tu kuwa wamepandisha mishahara ya watumishi wote.

Wakati wa Magufuli mishahara haikupanda, lakini pia inflation haikupanda, na hivyo thamani ya shillingi ikabaki pale pale kwa muda wote wa utawala wake hadi anatangulia mbele ya haki.
 
Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan!

Kama nilivyoandika hapo awali, ninapenda kuchukua tena nafasi hii kutoa salaam zangu za pole kwako wewe binafsi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika, hiki ni kipindi kigumu sana kwako wewe binafsi na kwa Tanzania kama Taifa na nchi...
BAK hivi kulikuwa na figisu gani mpaka JWTZ wakaingilia kati kuhusu kuapishwa suluhu?
 
Back
Top Bottom