BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan!
Kama nilivyoandika hapo awali, ninapenda kuchukua tena nafasi hii kutoa salaam zangu za pole kwako wewe binafsi kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika, hiki ni kipindi kigumu sana kwako wewe binafsi na kwa Tanzania kama Taifa na nchi.
Imenipasa katika kipindi hiki cha Maombolezo haya makubwa kushiriki katika kutoa maoni, maonyo na ushauri kuhusu mambo muhimu yaliyo na maslahi mapana kwa Taifa ambayo hayana budi kufanyika ili kuliweka Taifa pamoja. Ninaona ni muhimu haya kuyasema sasa wakati ambao pia nchi inajiandaa kupokea mabadiliko makubwa ya kiuongozi.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa Rais wa nchi kwa kipindi chote cha miaka minne na nusu iliyosalia. Ninaahidi kuendelea kukuombea wewe pamoja na Serikali yako katika jukumu hili zito.
Ni kwa sasabu hiyo, mimi Askofu Mwamakula, nisimamaye katika zamu yangu kama mtumishi wa Mungu katika zama hizi, ninao wajibu wa kukuangaliza mambo kadhaa lakini yaliyo ya muhimu ambayo itakupasa uyatafakari sana wakati huu unapoanza safari ya kuliongoza Taifa hili (Ezekieli 33:1-20)!
Ninapenda kukurejesha wewe pamoja na washauri wako katika tukio kama hili lililotukia miaka mingi iliyopita muda mfupi mara baada ya kifo cha Mfalme Sulemani ambapo mrithi wake alijikuta katika wakati mgumu kufuatia kukataa ushauri wa wazee na kufuata ushauri wa vijana wahuni. Tukio hilo limetunzwa vizuri kama kumbukumbu katika Biblia Takatifu katika Kitabu cha 1Wafalme 12:1-24 na Kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 10:1-11:4.
Ni kwa sababu hiyo, mimi pamoja na wengine tunaona mambo yafuatayo ni ya muhimu sana kwa uongozi wako kuyarekebisha ili kuliunganisha Taifa lililogawanyika:
1. Tunashauri utawala mpya uondoe zuio la Vyama vya Siasa kufanya Siasa na hivyo mruhusu mikutano ya hadhara katika nchi nzima na mambo yote ya kisiasa yaliyoruhusiwa na Katiba ya Nchi.
2. Tunashauri utawala mpya uwaachie huru wafungwa wote wa kisiasa na kufuta kesi pamoja na kuwaachilia huru Mahabusu wote wanaoshikiliwa katika Mahabusu na Magereza zote nchini kwa tuhuma za kisiasa ambazo zimepewa majina ya uchochezi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, madawa ya kulevya nk.
3. Tunashauri utawala mpya ujenge mazingira ya kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili Chaguzi ndogo zote (by-elections) zinazofuata pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao visimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi.
4. Tunashauri utawala mpya usikilize maoni ya makundi mbalimbali nchini yanayodai Katiba Mpya na ujenge mazingira ya kuanza upya kwa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ili Uchaguzi Mkuu ujao ufanyike chini ya Katiba Mpya.
5. Tunashauri utawala mpya uachie Vyombo vya Habari kufanya kazi zao kwa Uhuru pasipo kuingiliwa na dola.
6. Tunashauri utawala mpya uanzishe mazungumzo na Vyama vya Upinzani nchini ili kufanya maridhiano kuhusu namna ya kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao uliharibiwa mwaka 2019.
7. Tunashauri utawala mpya uangalie na kurekebisha mazingira ya wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali nchini ikiwemo kuzifungua Akaunti zilizozuiliwa kwa sababu mbalimbali hasa ambazo mazingira ya kufungiwa kwazo yalikuwa na harufu za kisiasa.
8. Tunashauri utawala mpya uache kutumia Vyombo vya Dola hasa Jeshi la Polisi katika kuhujumu vyama vya Upinzani na makundi mbalimbali yanayotetea Haki nchini.
9. Ikiwa njia ya maridhiano, tunashauri utawala mpya ufungue milango ya mazungumzo na maridhiano kwa kutoa mwaaliko kwa wanasiasa, wanaharakati na Wafanyabiashara walio uhamishoni warudi nchini.
10. Tunashauri utawala mpya ufungue majadiliano na maridhiano na viongozi wa Vyama vya Upinzani kuhusu malalamiko yao kufuatia Uchaguzi Mkuu uliopita.
11. Tunashauri utawala mpya uwapandishe madaraja Watumishi wa umma wanaostahili pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote.
Tunapenda kukuhakikishia kuwa sisi viongozi wa dini ambao tumejipambanua katika kutetea Haki na kusema kweli katika nchi hii tutatoa ushirikiano kwa utawala mpya kwa kila jema litakalofanywa kwa ajili ya kuweka upya na kuendeleza misingi ya Haki na Maridhiano katika nchi yetu.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfutate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani