The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Duuh, sasa mambo yameanza kufumuka na kunoga. Siri siyo siri tena...
Wote tunakumbuka tuhuma za Tundu Lissu kwa mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan aitwaye Abdul kwenda nyumbani kwake mwanzoni mwa mwaka huu 2024 kumshawishi apunguze kasi ya mashambulizi dhidi ya utawala mama yake na yeye atampa mapesa (rushwa) ya kumsaidia kwenye mambo yake...
Katika maelezo ya Tundu Lissu, alisema, ili huyu Abdul amfikie ilibidi kuwatumia viongozi fulani wa CHADEMA very influential ndani ya chama kumfanyia "connection" Ili kuonana naye na ikawa hivyo....
Ktk maelezo ya Tundu Lissu aliyopewa na Abdul alipokutana naye nyumbani kwake (TL) kupelekewa "mzigo" ni kwamba, baadhi ya wenzie ndani ya CHADEMA huyu Abdul alishamalizana nao kwa kupokea migawo yao ya "mzigo wa rushwa ya kuwafunga midomo", kwamba, amebaki yeye tu Tundu Lissu...
Kama tunakumbuka vyema, Tundu Lissu ktk tuhuma dhidi ya baadhi ya viongozi wenzake ndani ya CHADEMA kuhongwa na Rais Samia kupitia kwa mwanae Abdul, actually alikuwa hataji majina yao zaidi ya kusema wapo...
Sasa leo, Askofu Mwanamapinduzi akihojiwa ktk mahojiano maalumu na Mwanahalisi Online TV, ametegua kitendawili kwa kumtaja kiongozi mmojawapo wa CHADEMA aliyetumiwa na Abdul Ili amwone Tundu Lissu na kumshawishi kuchukua rushwa ya kuziba midomo toka kwa mama yake Rais Samia Suluhu Hassan...
Pamoja na mambo mengine, hebu tazama na msikilize mwenyewe huyu Askofu Mwanamapinduzi...
Sasa mambo yameanza kunoga....