Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali

Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali

Sheria za nchi hazitoshi kushughulika nao?..

.Sasa sheria zina kazi gani kama mnatumia uhalifu kushughulika uhalifu?

Sheria na demokrasia ni mali ya waerevu na sio primitive society...Taifa letu bado liko kwenye Primitive stage...

Wapumbavu wapo kila mahala, na ukifuata sheria basi huwezi kutoa hukumu sahihi dhidi ya wapumbavu..

Ukishakuwa na file la mtu fulani na matendo yake mabaya kwa Taifa ni kutoa amri ashughulikiwe, tukiwamaliza hawa basi upumbavu utakuwa umeisha na waerevu watakaobaki watatungiwa sheria na kupewa demokrasia waifuate...Stage hii imepitiwa na mataifa yote tunayoyaita yameendelea..
 
Hasira za Mwingira ni benki yake ya Efatha kufilisika na ilipoomba loan from BOT ikakutana na kizingiti kwakuwa benki ilikuwa na janja janja nyingi ktk kujiendesha kwake ikiwemo fedha kumiliki baadhi ya mali ambazo ziliingia nchini kwa mgongo wa kanisa na kukwepa kodi nk

Ila hizo porojo za kusema eti watu wa Serikali walitaka kuniua mara tatu apeleke hizi pumba kwa wahuni wenzake, ajue tu kwamba mkono wa Serikali ukikutaka haukukosi
Mlidhan boss wenu angeishi milele mbwa nyie
 
Kweli mtu akiguswa Mali ndio utamjua.
Siko miongoni wa wanaotumia ujinga wa WaTz kujimbilikizia mali kwa mwamvuli wa dini.
Wajipa majina ya Mitume, Manabii na mengine kemkem ili wawatishe wajinga halafu wachukue hela zao

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Haya kuchomwa na wananchi, usidhani mtatupoteza kirahisi. Ameshawataja wahusika, hivyo hata mseme nini, Ukweli uko palepale.
Yalichomwa na wanakijiji wenye hasira baada ya mwingira kuexpand kwenye eneo lenye mgogoro buffer zone, na walinzi wake wakamuua mwanakijiji kwa risasi
 
Mungu aendelee kukupigania dhidi ya hawa wana wa iblisi wanaoabudu ktk vita ya damu na nyama
 
Mnayosema yote ni kweli wala hatuwakatalii, ila alichosema leo huko kanisani ni kweli tupu. Hivyo ibueni uchafu wake mwingine wowote, lakini hamuwezi kufifisha ukweli aliosema leo.

Ukweli upi mkuu aliousema...hebu uweke tuone huo the so called ukweli...
 
Sheria na demokrasia ni mali ya waerevu na sio primitive society...Taifa letu bado liko kwenye Primitive stage...

Wapumbavu wapo kila mahala, na ukifuata sheria basi huwezi kutoa hukumu sahihi dhidi ya wapumbavu..

Ukishakuwa na file la mtu fulani na matendo yake mabaya kwa Taifa ni kutoa amri ashughulikiwe, tukiwamaliza hawa basi upumbavu utakuwa umeisha na waerevu watakaobaki watatungiwa sheria na kupewa demokrasia waifuate...Stage hii imepitiwa na mataifa yote tunayoyaita yameendelea..
Hao wapumbavu walishawahi kumalizwa wapi?....utajuaje umewamaliza?
 
NUKUU ZA ASKOFU MWINGIRA:

1. "Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali."

2. "Mali zangu zenye thamani ya 10 bilioni yakiwemo Matrekta yaliteketezwa Shambani kwangu."

3. "Dereva wangu alihusishwa katika mauaji na nilipogundua nilimnyang'anya simu."

4. "Dada aliyetoa taarifa za mipango ya kuuawa kwangu aliuawa Rombo Hotel Shekilango Dar es Salaaam."

5. "Mwaka unaokuja Watanzania watakuwa Salama."

26/12/2021.

Stay tuned.

View attachment 2058518
Mtume na Nabii Josephat Mwingira ni Mtumishi wa Mungu na kiongozi wa huduma ya Efatha Ministries nchini Tanzania.

Pia, soma:

Uchaguzi 2020 - Askofu Mwingira: Lissu ni mshindi, hajajenga flyover wala reli. Watu wanamfuata

Kazi ya Yesu ilikuwa kuhubiri injili sio kufanya biashara kwa kutumikisha mnaowaita waumini.

Mwingira ana mashamba ya ngano kwa maelfu Sumbawanga na huwa anatumikisha Sana waumini.Usikute hata Kodi halipi.
 
Nikama vike hali inastaajibisha, hii nchi haijulikanai nani ni nani, naanza kuamini taratibu maneno ya mwingira kuwa inawezekana kuna shetani nchi hii

Hayati Magufuli alisema wazi kuwa alinusurika kuuwawa

Lengai Ole Sabaya nae alieleza mahakamani kuwa alinusurika kuuwawa mara mbili,

Lissu nae alinusurika kuuwawa,

Mzee mangula pia Alinusutika kuuwawa,

Lema alinusurika kuuwawa,

Nabii Mwingira nae alinusurika kuuwawa

Zakaria alinusurika kuuwawa,

lakini cha ajabu hawawataji waliotaka kuwauwa hawakamatwi na mpaka leo hawajulikani,

Nchi hii kuna nini? kuna kundi la watu waliojificha wanatenda haya? je mpaka walitaka kumuua JPM na alipopata Urais akashindwa kuwakamata? Je, waliotaka kumuua Mangula kwa kumnywesha sumu? vipi kwa sabaya?

tuendelee kukaa na kitendawili hiki?

NANI MUUWAJI NCHI HII?
 
Back
Top Bottom