Askofu Niwe Mugizi jimbo Katoliki Rulenge Ngara Kagera, kuongoza kampeni ya kupinga katiba mpya

Askofu Niwe Mugizi jimbo Katoliki Rulenge Ngara Kagera, kuongoza kampeni ya kupinga katiba mpya

... Tunahitaji Maaskofu Kama Hawa, 2ko Pamoja Niwemugizi.!
 
Nani kampa huo uaskofu wa watu. Hajapigiwa kura na yeyote kuwa askofu wa Rulenge.Hajui hata maana ya kura huyo.Kawekwa tu kwa mfumo dikiteta wa kanisa katoliki ambao hauwapi waumini nafasi za kupigia kura maaskofu wao.

Mtu ambaye amewekwa bila kura siasa za kura kazijulia wapi? Akome kabisa.Kama ana cha kuhamasisha akahamasishe kanisa katoliki kuwa Maaskofu wawe wanapigiwa kura na waumini kuwa maaskofu badala ya mfumo wa sasa wa kidikiteta.
Akatoe boriti kwenye jicho la kanisa lake kwanza.

Mimi na wakatoliki wenzangu hatuna shaka na hilo daraja la uaskofu,aliempa tunamwamini hizi ni taratibu zetu za kikanisa
 
Askofu Niwemgizi wa jimbo Katoriki jimbo kuu Rulenge amesema ataongoza kampeni ya kura ya hapana kupinga katiba mpya.
ngoma bado mbichi - tuwaache wafanye bwembwe zao pale dodoma ila kutawashika tu. Asante askofu tupo pamoja.
 
Sijamtishia hapa mtanzania yeyote nimemwambia NIWEMUGIZI mwenye jina la kitusi toka rwanda

Na hiyo ndio silaha pekee mliyobakiza kuwanyamazisha wanaopinga uchakachuaje wenu. Si unaona Jenerali ulimwengu siku hizi kaufyata? Sasa siye wa Dodoma sijui mtatuambia ni wa wa wapi. Oneeni tu wa mipakani kwa hiyo hoja yenu dhaifu. Kipi bora kwako? Mgeni anayetetea haki za watanzania au Mtanzania anayezikanyaga? Amka usingizini mifupa yako itajalaaniwa na wajukuu zako wewe....
 
Kinachokera ni kuona viongozi hao wa kiroho wakitoa matamko baada ya kushinikizwa na mtu anayeutamani urais kwa udi na uvumba

kwani EL hana maslahi na hito rasimu yenu mliyolazimisha mpk aipinge?
 
Unaongea tu wewe,ila hulijui kabsa kanisa katoliki,kuna mwanausalama gani nchi hii anayeweza kumkamata kiongozi wa kanisa katoliki??unafikiri hao wanausalama wanatoka wapi?? Rais wako na mwenyekiti wa chama chako mwenyewe alienda vatican kutambika,halafu dogo unaongea ongea tu kama ulianza kutoa miguu badala ya kichwa..nchi hii atakapotoa kauli askofu wa kanisa katoliki ni tofauti na kauli ya maaskofu uchwara wala mashehe. Katoliki wakiamua wameamua,then vichwa vya wakatoliki wengi viko flexible na asilima kubwa wameenda shule na mchango wa hilo kanisa kwenye nchi hii hauelezeki. Acha kuropoka

You have proved to be a Great Sinker. Below is your profile:

Join Date : 11th August 2013

Posts : 92

Rep Power : 379

Likes Received:17

Likes Given:2
 
Ni Upumbavu Kutumia Dini Kuitisha SERIKALI au Kubeba Ajenda za KISIASA NIWEMUGIZI Anaweza Kuwa na Upande wake KISIASA ni HAKI YAKE na Hajakosea, Kosa no Yeye na Wengine Kutumia Dini Kudrive Agenda za KISIASA.
Hivi na Waislamu Mfano Wakasema Bila 2 Hatukubali???
Walutheri, WAHINDU, nk nk Wakawa na MISIMAMO Yao Tofauti na Wakitoa Vitisho?????
SIASA ni Utawala wa DOLA , Utawala wa DOLA Hauwezi Endeshwa kwa UTASHI WA DINI MOJA ktk TAIFA AMBALO ni SECULAR HALINA DINI.
Ni Mpotofu Kanisa Katoliki Haliwezi Kuibulldozz SERIKALI Hata away mini wake sio Wote Wanaokubali UPUUZI HUU!
Tunawaheshimu Viongozi wa Dini KAMWE HATUWAABUDU.
Tutafuata Maelekezo Yao ya KIDINI SIO YA KISIASA.
"YA MUNGU MPE MUNGU YA KAISARI MPE KAISARI " YESU KRISTO
 
Haitoshi tu kusema kuwa nina mawazo ya kipumbavu ilhali umeshindwa kuyaainisha. Viongozi wa kidini wanapaswa kuhubiri amani, upendo na mshikamano na si kuhamasisha vurugu, utengano na mfarakano

Pia wanapaswa kutoa mwongozo kwa waamini wao pale mambo yenye maslahi kwa wananchi yanapopotoshwa na wachache. That why huwa tunawaskiliza sana katika upuuzi kama huu unaoendelea.
 
Haya ndiyo maneno ya busara tuliyokuwa tukisubiri tangu mchakato uanze, Baba askofu amenena, nchi haiwezi kupoteza mabilioni ya kodi kwa kuandaa mchakato badala yake kikundi cha wahuni kichakachue maoni.Niko pamoja na mhashamu askofu, wengi mtaongea mengi ya uchochezi lakini hakuna ujanjaujanja katika hili lazima viongozi wa dini waingie kati kuokoa mchakato.
 
Back
Top Bottom