Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Baba Askofu ameongea hayo alipokuwa anahojiwa na gazeti la Mwananchi.
Amesema ni vema Rais Samia Suluhu akaanza na Katiba Mpya ili kutengeneza msingi imara wa Utawala bora ambao utazingatia haki.
Ameahidi kukutana na Mh Rais ili kumpatia ujumbe huu haraka iwezekanavyo.
-----
“Nikipata nafasi ya kumshauri Rais Samia Suluhu Hassan nitamwambia atengeneze miongozo bora ya kuongoza; na miongozo mizuri inaanza na Katiba inayotengeneza taasisi na mifumo. Tusitegemee uwezo wa mtu binafsi. Mtu anakuja leo na kuondoka kesho.”
Hiyo ni kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi aliyoitoa wakati akizungumzia uongozi na ustawi wa Taifa katika mahojiano maalumu na Gazeti la Mwananchi ofisini kwake mkoani Kagera.
Askofu Niwemugizi alisema katiba bora na imara itazaa sheria nzuri itakayoweka miongozo na dira inayowabana wote wanaokabidhiwa dhamana ya uongozi bila kutegemea utashi binafsi. “Rais Samia akitaka kuacha legacy ya kudumu kabisa, aanze na wananchi wanataka wajitawale namna gani na nchi iongozwe vipi; kwa asilimia 90 rasimu ya Katiba mpya ya Tume ya Jaji Warioba iliweka miongozi mizuri, ukiacha vitu vichache kama Serikali moja, mbili au tatu ambavyo vinaweza kuwa changamoto. Tuanzie pale,” alisema Askofu Niwemugizi.
“Hata masuala ya nidhamu, maadili ya viongozi na mambo yakupambana na rushwa yaliwekwa vizuri. Ule ulikuwa ni mwongozo mzuri ambao ungetengenezewa sheria na mfumo unaoeleweka mambo yangekwenda vizuri.”
Alisema Taifa linahitaji Katiba ngumu isiyowapa viongozi mchakato mwepesi wa kufanya mabadiliko kwa utashi na masilahi binafsi.
“Katiba inayoongoza Taifa haipaswi kuchezewa kwa kubadilishwa kirahisi kwa kutoa ukurasa mmoja na kuchomeka nyingine. Hapana! Tutengeneze Katiba ya nchi, sio ya mtu wala ya chama. Tuweke mfumo usiobadilika kwa utashi wa mtu wala ushabiki wa vyama vya siasa,” alisema.
Matumaini kwa Rais Samia
Akizungumzia matarajio kwa uongozi wa Samia, Askofu alisema: “Rais Samia ameamsha matumaini mapya ya wananchi, ameonyesha utashi wa kutaka uwepo wa utawala bora. Amewaagiza anaowateua kurekebisha baadhi ya mambo yaliyoonekana hayako sawa. Lakini utashi huo uanze kwa kurekebisha sheria.”
Alisema baadhi ya mambo aliyotaka yarekebishwe ni kufungulia vyombo vya habari vilivyofungwa pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuacha kutumia nguvu kufunga na kuchukua fedha kwenye akaunti za wafanyabiashara, hivyo lazima sheria hizo zirekebishwe.
“Hapo ndipo utashi wa kauli za Rais zitakapoonekana kuleta matumiani kwa wananchi. Tusitegemee utashi na maneno ya mtu. Tuyawekee mfumo mzuri na imara wa sheria,” alisema.
Ripoti ya CAG
Askofu Niwemugizi alitumia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayoonyesha mianya ya matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za umma kama mfano hai wa hitaji la taasisi huru na mifumo imara inayoundwa na katiba na sheria badala ya kutegemea uimara wa viongozi waliopo madarakani.
“Tuliamini Serikali tuliyokuwa nayo ilikuwa imara sana; na tulikuwa na kiongozi asiye na simile kwenye masuala ya rushwa na ubadhirifu. Lakini ripoti ya CAG imekuwa tofauti kwa kuonyesha mianya ya matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za Taifa,” alisema Niwemugizi.
“Kwa hiyo tunarudi kulekule kwenye umuhimu wa mifumo na taratibu zinazojulikana za kuwadhibiti wanaosimamia masuala ya fedha na kuziba mianya ya matumizi mabaya nje ya bajeti,” alisema Askofu Niwemugizi.
Mahojiano zaidi na Askofu Niwemugizi kuhusu masuala mbalimbali ya Taifa, ikiwamo nini kifanyike kufikia maendeleo endelevu yalikuwa kama ifuatavyo:
Swali: Nini maoni yako kuhusu mwelekeo wa Tanzania kiuchumi, kijamii na kisiasa, hasa ukitilia maanani Katiba mpya?
Jibu: Mimi ni mmoja wa waumini wa sifa au mambo manne aliyoyasema Mwalimu Julius Nyerere kuwa ili nchi iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Sasa Watanzania wapo wengi na tunaendelea kuongezeka. Ardhi ipo kubwa, nafikiri Tanzania bado ina eka nyingi tu. Nikitazama kwa jicho la kawaida tu nafikiri tatizo letu lipo kwenye siasa safi na uongozi bora.
Serikali zilizopita zilionekana zinachapa kazi kweli kweli na watu wakawa na matumaini makubwa. Lakini kwa kadri tulivyokwenda mambo yalionekana ni uongozi wa mtu mmoja ndiye anayesema hiki kifanyike na wakati mwingine anafanya yeye mwenyewe. Kwa mtindo huo mambo yalikuwa magumu sana.
Mfano kwenye siasa wakiwamo wanaokuwa na macho ya kuona na kufikiri tofauti, wale wenye mawazo mbadala wanaoitwa wapinzani wakifika mahali wanazuiwa kusema hakuna wa kukosoa. Ukiwa kipofu utabaki kipofu na hakuna wa kukuambia usiende huko utaanguka kwenye shimo. Nafikiri tuna matatizo katika siasa na uongozi bora.
Swali: Bila kuingiza masuala binafsi ya viongozi, unaizungumziaje Serikali ya awamu ya tano na hii ya sasa ya awamu ya sita?
Jibu: Mimi siyo mtaalamu wa uchumi, lakini ukiangalia na kusikia manung’uniko kwenye jamii unajua mambo sio mazuri sana, japo Serikali imetuambia tumefika kwenye uchumi wa kati wa chini.
Inawezekana vigezo vilivyotumika imetumia mizania ya nchi ikaonekana mapato na uchumi wa nchi yako juu. Lakini waliowezesha kufikia vigezo hivyo ni wachache sana. Mifukoni mwa watu hakuna; kama Rais Samia alivyosema katika moja ya hotuba zake.
Hivyo mambo hayajawa sawa na kunahitajika sera, sheria na mfumo virekebishwe kujenga mazingira yanayowezesha watu wengi zaidi kufanya biashara na kuwezesha uchumi kukua.
Watu na sekta binafsi ndiyo injini ya uchumi wa Taifa. Wawekewe mfumo utakaoboresha biashara. Wawekewe kodi na mazingira rafiki. Makadirio ya kodi yafanyike bila kuua mitaji.
Swali: Baadhi ya viongozi walikuwa marafiki zako na walikuwa nyuma ya suala lako la kuhojiwa uraia. Umewawekea kisasi au umesamehe saba mara sabini kama mafundisho ya Bibila?
Jibu: Mimi nimesamehe na ninaendelea na shughuli zangu. Tunayaachia hapo
Chanzo: Mwananchi