Uwezekano mkubwa ni kuwa hujawahi kuwa na imani nao, na wala hutakuja kuwa na imani nao kama ni mtu unayechukia haki.
Viongozi wa dini ni lazima wahubiri haki, upendo, amani ya mwili na Roho; muhimu zaidi wapinge na wakemee bila woga uovu wote unaotendwa na mwanadamu bila ya kujali cheo chake, utajiri wake au hali yake yoyote.
Wakati tunawasifu baadhi ya viongozi ambao wakati wote walikemea uovu wa uongozi wa awamu ya 5, tunawalaumu kwa uoga na unafiki viongozi wote wa dini waliokuwa wakijishakamanisha na utawala dhalimu wa awamu ya 5. Mungu ni mwenye huruma, wanachotakiwa kufanya hata sasa, ni kuujutia na kuutubia uovu ule.