Askofu Niwemugizi amshauri Rais Samia Suluhu kuanza na Katiba Mpya

Askofu Niwemugizi amshauri Rais Samia Suluhu kuanza na Katiba Mpya

Ya kaisari yana uhusiano gani na katiba mpya? Majizi ya kura mkisikia katiba mpya mnachanganyikiwa maana mnajua udhalimu wenu utakosa nafasi. Bila machafuko sioni katiba mpya ikipatikana kwa njia ya amani.
Ahaaaa, Tindo umefikia hali mbaya sana. Na hii ni baada ya kuona wananchi hawawapi sapoti.
 
Hao ni waunini wasiojua dini vizuri sasa ukiona kiongozi wa dini tena askofu yuko kieango cha waumini hapo kuna shida.Huyu Askofu ni zero hajui hata kuwa Askofu maana yake nini?
7
badala ya kysoma biblia anashinda mitandaoni kusoma mada za kisiasa ndio masna kichwani mweupe anahubiri watu waamini katiba badala ya injili

Kama viongozi wa kisiasa wanaohubiri madhabahuni ni waumini, basi maaskofu wanaotaka katiba mpya ni watanzania wenye nia njema na nchi.
 
hakuna anaekubali kujichimbia kaburini lake mwenyewe
 
Ahaaaa, Tindo umefikia hali mbaya sana. Na hii ni baada ya kuona wananchi hawawapi sapoti.
Hayo ni matamanio yako wananchi wasitupe support, kwa bahati mbaya ukweli ni kinyume na matamanio yako. Ndio maana mkisikia katiba itakayotoa haki mnajua fika ukweli wa udhalimu wenu utafahamika.

Ukiona timu ya mpira haitaki technology ya VAR basi ujue timu hiyo haina uwezo wa kushinda kihalali. Na kwa taarifa yako ccm ingekuwa inakubalika na wananchi, wangekubaliana na katiba mpya bila usumbufu wowote.
 
Hao ni waunini wasiojua dini vizuri sasa ukiona kiongozi wa dini tena askofu yuko kieango cha waumini hapo kuna shida.Huyu Askofu ni zero hajui hata kuwa Askofu maana yake nini?

badala ya kysoma biblia anashinda mitandaoni kusoma mada za kisiasa ndio maana kichwani mweupe anahubiri watu waamini katiba badala ya injili
Huyu ni zero bright ni yule aliyepeleka sanamu ya Mama Bikira Maria Chato?
 
Katiba mpya mwaka mwisho apite urahisi uchaguzi mitano tena....iwe rahisi
 
Uwezekano mkubwa ni kuwa hujawahi kuwa na imani nao, na wala hutakuja kuwa na imani nao kama ni mtu unayechukia haki.

Viongozi wa dini ni lazima wahubiri haki, upendo, amani ya mwili na Roho; muhimu zaidi wapinge na wakemee bila woga uovu wote unaotendwa na mwanadamu bila ya kujali cheo chake, utajiri wake au hali yake yoyote.

Wakati tunawasifu baadhi ya viongozi ambao wakati wote walikemea uovu wa uongozi wa awamu ya 5, tunawalaumu kwa uoga na unafiki viongozi wote wa dini waliokuwa wakijishakamanisha na utawala dhalimu wa awamu ya 5. Mungu ni mwenye huruma, wanachotakiwa kufanya hata sasa, ni kuujutia na kuutubia uovu ule.
Mfano ninaowalaumu ni kama wale wa Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo. Maana wale ni kama misukule, anachosema Gwajima wanakiamini.

Wengine ni wa TAG wale waliompa Mwendazake tuzo ya ushindi dhidi ya Corona. Na Mungu akawaonyesha kuwa TAG ni wafuasi wa Shetani kwa kuwa Magufuli alikufa kwa Corona hiyo hiyo aliyoipuuza
 
Be cool my fellow friend, niny huwa mnazungumzia haki gan!!!? Mtu mwenyew anatakiwa kuzungumzia dini na siyo siasa yey si mwana siasa,,, in fact dini na siasa havita kiwi kwenda pamoja vitu hivi,
Kwa hiyo unamanisha mwanasiasa tu ndo anahaki ya kuzungumzia siasa. Basi isingefundishwa mashuleni. Je watu wa fani zingine hawastahili kuzungumzia siasa? Maana tuna wahandisi, wachumi, madaktari n.k je unasemaje juu ya hilo?
 
Usimsahau na Dr Shoo wa KKKT, naye amepambana sana dhidi ya UDHALIMU wa Mwendazake
Nilikuwa namtafuta jina lake nikawa nimesahau. Asante kwa ukumbusho. The rest ni manabii wa uongo tu. Mitume wa mashetani.
 
Mfano ninaowalaumu ni kama wale wa Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo. Maana wale ni kama misukule, anachosema Gwajima wanakiamini.

Wengine ni wa TAG wale waliompa Mwendazake tuzo ya ushindi dhidi ya Corona. Na Mungu akawaonyesha kuwa TAG ni wafuasi wa Shetani kwa kuwa Magufuli alikufa kwa Corona hiyo hiyo aliyoipuuza
Kanisa la Tanzania lina changamoyo nyingi sana. Mtu kama Gwajima anakuwaje Mtumishi wa Mungu? Au mtu kama Pengo au Musa alhad?
 
Hayo ni matamanio yako wananchi wasitupe support, kwa bahati mbaya ukweli ni kinyume na matamanio yako. Ndio maana mkisikia katiba itakayotoa haki mnajua fika ukweli wa udhalimu wenu utafahamika.

Ukiona timu ya mpira haitaki technology ya VAR basi ujue timu hiyo haina uwezo wa kushinda kihalali. Na kwa taarifa yako ccm ingekuwa inakubalika na wananchi, wangekubaliana na katiba mpya bila usumbufu wowote.
Hujafanya tathimini? Mbowe katoa tamko juu ya kuporwa bil 2 kapuuzwa.

Kuhusu katiba mpya mnatafuta kisingizio. Maana hata ikipatikana kama wananchi hawakubali mtaambulia nini?
 
Hujafanya tathimini? Mbowe katoa tamko juu ya kuporwa bil 2 kapuuzwa.

Kuhusu katiba mpya mnatafuta kisingizio. Maana hata ikipatikana kama wananchi hawakubali mtaambulia nini?

Ulitaka Mbowe aliposema kaporwa bilioni mbili nini kifanyike? Aliporwa hela za chama au za biashara zake? Aliporwa hizo hela na Ccm? Unaongeaga use@@nge gani we dogo?

Ipatikane hiyo katiba mpya ili udhibitisho wa kutokukubalika uwe wazi.
 
Baba Askofu ameongea hayo alipokuwa anahojiwa na gazeti la Mwananchi.

Amesema ni vema Rais Samia Suluhu akaanza na Katiba Mpya ili kutengeneza msingi imara wa Utawala bora ambao utazingatia haki.

Ameahidi kukutana na Mh Rais ili kumpatia ujumbe huu haraka iwezekanavyo.

-----
“Nikipata nafasi ya kumshauri Rais Samia Suluhu Hassan nitamwambia atengeneze miongozo bora ya kuongoza; na miongozo mizuri inaanza na Katiba inayotengeneza taasisi na mifumo. Tusitegemee uwezo wa mtu binafsi. Mtu anakuja leo na kuondoka kesho.”

Hiyo ni kauli ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi aliyoitoa wakati akizungumzia uongozi na ustawi wa Taifa katika mahojiano maalumu na Gazeti la Mwananchi ofisini kwake mkoani Kagera.

Askofu Niwemugizi alisema katiba bora na imara itazaa sheria nzuri itakayoweka miongozo na dira inayowabana wote wanaokabidhiwa dhamana ya uongozi bila kutegemea utashi binafsi. “Rais Samia akitaka kuacha legacy ya kudumu kabisa, aanze na wananchi wanataka wajitawale namna gani na nchi iongozwe vipi; kwa asilimia 90 rasimu ya Katiba mpya ya Tume ya Jaji Warioba iliweka miongozi mizuri, ukiacha vitu vichache kama Serikali moja, mbili au tatu ambavyo vinaweza kuwa changamoto. Tuanzie pale,” alisema Askofu Niwemugizi.

“Hata masuala ya nidhamu, maadili ya viongozi na mambo yakupambana na rushwa yaliwekwa vizuri. Ule ulikuwa ni mwongozo mzuri ambao ungetengenezewa sheria na mfumo unaoeleweka mambo yangekwenda vizuri.”

Alisema Taifa linahitaji Katiba ngumu isiyowapa viongozi mchakato mwepesi wa kufanya mabadiliko kwa utashi na masilahi binafsi.

“Katiba inayoongoza Taifa haipaswi kuchezewa kwa kubadilishwa kirahisi kwa kutoa ukurasa mmoja na kuchomeka nyingine. Hapana! Tutengeneze Katiba ya nchi, sio ya mtu wala ya chama. Tuweke mfumo usiobadilika kwa utashi wa mtu wala ushabiki wa vyama vya siasa,” alisema.

Matumaini kwa Rais Samia

Akizungumzia matarajio kwa uongozi wa Samia, Askofu alisema: “Rais Samia ameamsha matumaini mapya ya wananchi, ameonyesha utashi wa kutaka uwepo wa utawala bora. Amewaagiza anaowateua kurekebisha baadhi ya mambo yaliyoonekana hayako sawa. Lakini utashi huo uanze kwa kurekebisha sheria.”

Alisema baadhi ya mambo aliyotaka yarekebishwe ni kufungulia vyombo vya habari vilivyofungwa pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuacha kutumia nguvu kufunga na kuchukua fedha kwenye akaunti za wafanyabiashara, hivyo lazima sheria hizo zirekebishwe.

“Hapo ndipo utashi wa kauli za Rais zitakapoonekana kuleta matumiani kwa wananchi. Tusitegemee utashi na maneno ya mtu. Tuyawekee mfumo mzuri na imara wa sheria,” alisema.

Ripoti ya CAG

Askofu Niwemugizi alitumia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayoonyesha mianya ya matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za umma kama mfano hai wa hitaji la taasisi huru na mifumo imara inayoundwa na katiba na sheria badala ya kutegemea uimara wa viongozi waliopo madarakani.

“Tuliamini Serikali tuliyokuwa nayo ilikuwa imara sana; na tulikuwa na kiongozi asiye na simile kwenye masuala ya rushwa na ubadhirifu. Lakini ripoti ya CAG imekuwa tofauti kwa kuonyesha mianya ya matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za Taifa,” alisema Niwemugizi.

“Kwa hiyo tunarudi kulekule kwenye umuhimu wa mifumo na taratibu zinazojulikana za kuwadhibiti wanaosimamia masuala ya fedha na kuziba mianya ya matumizi mabaya nje ya bajeti,” alisema Askofu Niwemugizi.

Mahojiano zaidi na Askofu Niwemugizi kuhusu masuala mbalimbali ya Taifa, ikiwamo nini kifanyike kufikia maendeleo endelevu yalikuwa kama ifuatavyo:

Swali: Nini maoni yako kuhusu mwelekeo wa Tanzania kiuchumi, kijamii na kisiasa, hasa ukitilia maanani Katiba mpya?

Jibu: Mimi ni mmoja wa waumini wa sifa au mambo manne aliyoyasema Mwalimu Julius Nyerere kuwa ili nchi iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Sasa Watanzania wapo wengi na tunaendelea kuongezeka. Ardhi ipo kubwa, nafikiri Tanzania bado ina eka nyingi tu. Nikitazama kwa jicho la kawaida tu nafikiri tatizo letu lipo kwenye siasa safi na uongozi bora.

Serikali zilizopita zilionekana zinachapa kazi kweli kweli na watu wakawa na matumaini makubwa. Lakini kwa kadri tulivyokwenda mambo yalionekana ni uongozi wa mtu mmoja ndiye anayesema hiki kifanyike na wakati mwingine anafanya yeye mwenyewe. Kwa mtindo huo mambo yalikuwa magumu sana.

Mfano kwenye siasa wakiwamo wanaokuwa na macho ya kuona na kufikiri tofauti, wale wenye mawazo mbadala wanaoitwa wapinzani wakifika mahali wanazuiwa kusema hakuna wa kukosoa. Ukiwa kipofu utabaki kipofu na hakuna wa kukuambia usiende huko utaanguka kwenye shimo. Nafikiri tuna matatizo katika siasa na uongozi bora.

Swali: Bila kuingiza masuala binafsi ya viongozi, unaizungumziaje Serikali ya awamu ya tano na hii ya sasa ya awamu ya sita?

Jibu: Mimi siyo mtaalamu wa uchumi, lakini ukiangalia na kusikia manung’uniko kwenye jamii unajua mambo sio mazuri sana, japo Serikali imetuambia tumefika kwenye uchumi wa kati wa chini.

Inawezekana vigezo vilivyotumika imetumia mizania ya nchi ikaonekana mapato na uchumi wa nchi yako juu. Lakini waliowezesha kufikia vigezo hivyo ni wachache sana. Mifukoni mwa watu hakuna; kama Rais Samia alivyosema katika moja ya hotuba zake.

Hivyo mambo hayajawa sawa na kunahitajika sera, sheria na mfumo virekebishwe kujenga mazingira yanayowezesha watu wengi zaidi kufanya biashara na kuwezesha uchumi kukua.

Watu na sekta binafsi ndiyo injini ya uchumi wa Taifa. Wawekewe mfumo utakaoboresha biashara. Wawekewe kodi na mazingira rafiki. Makadirio ya kodi yafanyike bila kuua mitaji.

Swali: Baadhi ya viongozi walikuwa marafiki zako na walikuwa nyuma ya suala lako la kuhojiwa uraia. Umewawekea kisasi au umesamehe saba mara sabini kama mafundisho ya Bibila?

Jibu: Mimi nimesamehe na ninaendelea na shughuli zangu. Tunayaachia hapo

Chanzo: Mwananchi
Tunamshukuru kwa Ibada ya Mazishi.Ila viongozi wengine waige mfano wa huyu askofu,naonaga anaongea ukweli mtupu,ambayo ni sifa ya mhimu sana kwa kiongozi mkubwa wa dini.maskofu wengi ni waoga sana,hasa linapokuja kutoa hoja ambayo itatofautiana na viongozi waandamizi wa serikali.

Ila mara hii hata nyang'anywa pasport
 
Ulitaka Mbowe aliposema kaporwa bilioni mbili nini kifanyike? Aliporwa hela za chama au za biashara zake? Aliporwa hizo hela na Ccm? Unaongeaga use@@nge gani we dogo?

Ipatikane hiyo katiba mpya ili udhibitisho wa kutokukubalika uwe wazi.
Mbowe aliongea mengi mojawapo ni kuporwa bil 2 ambazo kihalisia hajaporwa. Nia hasa ni kuonyesha kuna utawala usiofaa ni tarajio lake kuwa angewin support ya umma.

Ila nakuhakikishia katiba mpya ni kisingizio tu. Chadema ilishapoteza legitimacy mbele ya umma.
 
Mbowe aliongea mengi mojawapo ni kuporwa bil 2 ambazo kihalisia hajaporwa. Nia hasa ni kuonyesha kuna utawala usiofaa ni tarajio lake kuwa angewin support ya umma.

Ila nakuhakikishia katiba mpya ni kisingizio tu. Chadema ilishapoteza legitimacy mbele ya umma.

Sioni uhusiano wa support ya kisiasa na Mbowe kuporwa 2b. Huna jipya bali naona unaongea utoto tu.
 
Back
Top Bottom