Uchaguzi 2020 Askofu Niwemugizi ataka walioenguliwa wote warejeshwe kwenye kinyang’anyiro, Uchaguzi uwe wa Haki

Uchaguzi 2020 Askofu Niwemugizi ataka walioenguliwa wote warejeshwe kwenye kinyang’anyiro, Uchaguzi uwe wa Haki

Kama ni kweli nitarejesha imani kwa askofu huyu. Ampigie JPM amshauri hilo atoe maelekezo, kama yeye JPM karidhia wengine kina nani?
Huyu hanaga desturi ya unafiki huwa ana msimamo siku zote rejea swala la katiba mpya
 
Acha uduanzi,yaani askofu anakuteteeni bado mnashupaza shingo na kuropoka utopolo.

Kule south Africa haohao mnaowaita magaltia wanawapigania adhana yenu iendelee kulizwa baada ya mamlaka kunipiga 'bani'

Muwe waungwana,Askofu anapigania maslahi ya wote acha uzwazwa!

Sawa pamoja na matusi yote hayo, ponda alizungumza nini akasweka ndan na huyu anazungumza nini? Uislam haitaj mgalatia autete unaenda kama Allah alivyoukadiria. Lakini kwanini wengine wanyimwe sauti na wengine washupaze shingo katika ajenga moja? Unaweza usione hoja yangu lakin tafakari kwanza.
 
Sawa pamoja na matusi yote hayo, ponda alizungumza nini akasweka ndan na huyu anazungumza nini? Uislam haitaj mgalatia autete unaenda kama Allah alivyoukadiria. Lakini kwanini wengine wanyimwe sauti na wengine washupaze shingo katika ajenga moja? Unaweza usione hoja yangu lakin tafakari kwanza.
Siwezi kutafakari hoja nyepesi kiasi hicho.

Na hapo unaposema uislamu auhitaji mgalatia autete, kwani huyo askofu hapo anautetea uislamu au anahitaji haki itendeke?
Wewe jamaa ni hopeless umekaa kiudinidini tu!

Askofu anachokipigania ni the same anachokipigania Sheikh Issa Ponda, Sasa hapo unadhani ni yupi wa kumkabili na kumnyoshea kidole Kati ya Askofu 'mgalatia' , Sheikh Issa Ponda au Mtawala ambaye ni Magufuli na vyombo vyake vya dola?
 
Siwezi kutafakari hoja nyepesi kiasi hicho.

Askofu anachokipigania ni the same anachokipigania Sheikh Issa Ponda, Sasa hapo unadhani ni yupi wa kumkabili na kumnyoshea kidole Kati ya Askofu 'mgalatia' , Sheikh Issa Ponda au Mtawala ambaye ni Magufuli na vyombo vyake vya dola?

Sasa wewe umedandia hoja ujue hoja haijaelekezwa kwako, sasa sijui unataka nini kimsingi ni kwamba angekuwa Issa Ponda ndio anaandika haya sa hzi ameshazibwa mdomo
 
Ukiona hadi maaskofu wa Kikatoliki wameanza kuingilia kati basi ujue mwisho wa utawala wa ccm ni oct 28/2020
 
Sasa wewe umedandia hoja ujue hoja haijaelekezwa kwako, sasa sijui unataka nini kimsingi ni kwamba angekuwa Issa Ponda ndio anaandika haya sa hzi ameshazibwa mdomo
Haijalishi hoja imeelekezwa kwangu au kwa mwingine...itajibiwa kihoja tu.

Hapo ili utoe ukakasi mlaumuni Magufuli na vyombo vyake vya dola vinavyomdhibiti Sheikh Ponda ambaye anautetea Haki kwa watanzania na waislamu mkiwemo
 
NEC walitakiwa wawasaidie kujaza form wagombea na si kuwazuia kugombea. Mbona tukienda kupata huduma sehemu zinazotuhitaji kujaza form kama huelewi jambo kwenye form unarudi kwa wahusika kuwauliza namna sahihi ya kujaza form na unapewa maelekezo ili form yako ikamilike vizuri, Mfano umeacha tarehe, hujaandika labda mwaka wa kuzaliwa, hujaweka picha nk. Vyote utaambiwa kuvikamilisha ili swala lako likamilishwe. LAKINI NEC wamefanya kugombea kama mashindano ya kufanya mtihani kumbe ni swala la kikatiba na mtu hawezi kuenguliwa kwa sababu ya kukosea kujaza form labda asiwe na sifa ya kugombea.
Hao watu hawakukosea kujaza fomu. Kinachosumbua , ni Ile kauli "NIKUPE NYUMBA, GARI, MSHAHARA, ULINZI NK. HALAFU UMTANGAZE MPINZANI".

Wameona wawaengue mapema isiwe tabu .
 
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwetu ninyi nyote mnaosoma uzi huu ama kijiswali hicho kidogo. Asalaam alaykm!

Nataka niulize kajiswali kadogo.....Je, kazi za wasimamizi wa uchaguzi ni kuwaengua wagombea kwa mitego midogo midogo au kuwasaidia ili wapate sifa za kugombea?
Ni kwanini wasimamizi wa uchaguzi anapoona mgombea amekosea kujaza form au kuna kitu amekisahau asichukue nafasi yake kama kiongozi kumwelekeza ajaze vizuri? Anashindwa nini kumpigia simu kamaameondoka arudi ili aijaze vizuri?

Kwanini refa ndio anakua adui wa mchezaji badala ya kumwelekeza kufuata utaratibu?
Kwanini refa ndio anamtegeshea penati mchezaji?
Nia ni kuwaengua au kupata wagombea watakaoshindana ili mshindi apatikane kwa njia halali?
Ni sahihi kuwachagulia wananchi mgombea badala ya wao?
Mkuu haya ndy maswali mhimu sana..kwani jukum la tume ni kupokea form tu si ni pamoja na kutoa elimu?hapa tume kwanini imeshndwa kutumikia mshahara wake kwa mjibu wa utaratibu?Kuna Nia ovu hapa!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Baadhi yao wamekuwa purchased mkuu...

Hata wakirudishwa watakataa[emoji3][emoji3]
Na aliyepita bila kupingwa ndo mnunuzi so ni wajibu wa NEC na Takukuru kushirikiana ili kumwajibisha mnunuzi na mnunuliwa wote wamevunja sheria za uchaguzi!
 
nakusoma ila ngumu kuwagundua kaka...

Unakumbuka ya Mb Nassari.... Anaitwa afanye press conference kulalamika anajichelewesha kijanja ....

leo kijani....
Na aliyepita bila kupingwa ndo mnunuzi so ni wajibu wa NEC na Takukuru kushirikiana ili kumwajibisha mnunuzi na mnunuliwa wote wamevunja sheria za uchaguzi!
 
Kuwaengua wagombea ni uwendawazimu wa hali ya juu. Mwenye akili timamu hawezi kuufanya upumbavu huo.

Sioni sababu ya mtu kuenguliwa eti hakujaza form vizuri. Upumbavu mkubwa!! Tulistahili kuwa na sababu za msingi chache sana za kuweza kumwondolea mtu sifa ya kuwa mgombea, kama vile:

1) Mgombea kutokuwa raia (nayo ili isitumike vibaya - iwe jukumu la mlalamikaji kuthibitisha kuwa mgomvea siyo raia. Na wala isiwe jukumu la mlalamikiwa kuthibitisha kuwa ni raia

2) Mgombea aliwahi kuthibitika mahakamani na kuhukumiwa kuwa ni jambazi

3) Mgombea aliwahi kuthibitika mahakamani kutumia madaraka yake vibaya kwa kugandamiza wapinzani wake kisiasa

Mahakama ndiye kiwe chombo pekee cha kutoa hukumu ya kumwondoa mgombea, na Mwenyekiti wa NEC atangaze maamuzi ya mahakama.

Huu upumbavu wa iuengua wagomvea kwa sababu za kijinga na kwa hila; tusikubali. CCM wameweka na kupitisha sheria nyingi za kijinga kwaajili ya kupokonya haki ya wananchi katika kufanya maamuzi. Tupinge kuwa mateka wa ushetani wa CCM.

Kiongozi mzuri hupata faraja kubwa anapokuwa na uhakika kuwa anaowaongoza wanataka awaongoze. Sasa wewe uliyepitishwa bila kuolpingwa kwa hila, una uhakika gani unaowaongoza wanakutaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba kamanda Askofu anataka kuwapangia NEC, kama mtu hana umakini kwenye kujaza tu fomu hawezi pia kuwa na umakini kwenye mambo muhimu mengine ya uongozi.
Nashangaa ufisadi ulifanywa nawaliojaza form vibaya? Niswali tu
 
ASKOFU NIWEMUGIZI ATAKA WALIOENGULIWA WARUDISHWE WOTE, UCHAGUZI UWE WA HAKI


Ikifanyika hivyo, walioenguliwa halafu wakaamua kukata rufaa, watakuwa hawajatendewa haki kwa sababu:

Rufaa ipo iliwekwa kisheria na ina haki ya kukubaliwa au kukataliwa

Kukubaliwa rufaa ni haki ya mrufani, na kukataliwa rufaa ni haki ya mrufani pia

Kumkubalia mrufani rufaa kwa shinikizo nje ya mamlaka ya tume, ni kutokumtendea haki mrufani na vilevile

Kumkutalia mrufani rufaa kwa shinikizo nje ya mamlaka ya tume, ni kutokumtendea haki mrufani

Tume ikiilazimishwa kukubali au kukataa rufaa, inakuwa haijaitendewa haki, na inakosa maana na mamlaka ya kuendelea kuwepo
 
Huyu asikofu kichwa chake ni kizima sana,siyo wale mapadre,maasikofu na wachungaji wa Bariadi na Musoma.
 
Back
Top Bottom