Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

...
Screenshot_20210219-185042.jpg
 
Kinjekitile mwingine huyu hapa. Anawaaminisha watu kitu ambacho si sahihi. Unajua ukimuweka bacteria 'side by side' na virus, virus ataonekana kama mbuzi na bacteria ataonekana kama tembo.

Virus ni mdogo sana, ili kuweza tu kumuona ni lazima utumie electron microscope, embu niambie kuna tundu gani la kwenye barakoa linaloweza kumzuia virus asipite?
Ni bora tu watu wajue ukweli kwamba 'nothing is working so that they can brace themselves for impact' kuliko kuendekeza huu udanganyifu.
 
Askofu Ruwaichi ameongea kama mchungaji halisi,Viongozi wa serikali ni lazima wawe na huruma ya kutetea uhai wa watu wao hasa makundi yaliyo hatarini kama wazee wasipate CORONA kwa kutoa taarifa sahihi na kuchukua hatua stahiki.
Cha kushangaza 'wanaoishi kwa sadaka' ndio wanaoogopa kufa kuliko wanaoishi kwa jasho lao. Inaonekana huko madhabahuni ni kunono ndio maana wengi wanaogopa kupaacha na kwenda 'kwa Baba' wakihisi kule juu hawatapata maslahi manono kuliko wanayoyapata hapa Duniani.
 
Ameongea vizuri sana ila amesahau kukazia jambo la muhimu kuliko hiyo barakoa. Mungu asipoulinda mji, wakeshao wakesha bile.

Angekazia Hilo Kwa nguvu zote, kwani kuna waliokufa huku wakiwa na barakoa zao na hawakuwahi kuziacha, na kuna wengi tu ambao wanaambukizwa mbali na uaminifu wao wa kuvaa barakoa.
 
Askofu Jude amesahau Ukuu wa Mungu, anausujudia Ukuu wa Wanasayansi wa Duniani. Jamani tahadhari zimetolewa, ila wote tunajua hiki kitu kinapiga utosini na kinaenda kusumbua mfumo wa upumuaji.

Swali kwa huyo Askofu, kuufunika mdomo na pua aoni yeye pekee kama anaudisturb mfumo wa ppumuaji wa kawaida? Ma kuufanya utaratibu wa kuvaa barakoa kuwa sehemu ya Covid 19 yenyewe.
 
Mungu ni mkuu na mwenye mamlaka kwa kila kiumbe alichokiumba na kwenye biblia tumeambiwa tuseme ukweli na ukweli utakuweka huru
Ukweli unaongelewa kwenye Biblia ni Yesu. Yeye ndio ukweli utakao tuweka huru. Samahani, tafsiri nyingi kuhusu kauli hii zinapotoshwa.
 
Back
Top Bottom