Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

"Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa hekalu, akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde na ya kwamba,Mikononi mwao watakuchukua,Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe,Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako"
 
Anaitegemea barakoa imwokoe, pole yake huyo Askofu.
Its sad pale viongozi wa kiroho wanapohamisha imani yao toka kwa Bwana Yesu na kuipeleka kwenye barakoa.. Ndipo Yesu akawakemea wafuasi wake akisema, hata baada ya kukaa na mimi sikubzote hizi, bado tu hamjanifahamu vizuri?
Screenshot_20210220-093130.png
 
Kupoteza kondoo kwa ajili ya uongo unaoasisiwa awamu hii kanisa limeona si vyema bali ni kuwa tayari kuwalinda waumini wake.
Kabisa-Changamoto ya kijani ni kujifanya wanajua kila kitu na kwamba wao wana imani na kujua maandiko kuliko yeyote duniani,huu ndo upumbavu wa kwanza.
 
Kuvaa barakoa siyo njia pekee ya kinga dhidi ya covid. Iko haja ya wataalam kuelimisha watu jinsi ugonjwa unavyoambukizwa
 
Askofu Jude Thaddaeus Ruwa'Ichi wa jimbo Katoliki la D'Salaam ametoa hotuba nzito akiwa kanisani kuonya kuhusu corona.

Kasema kanisani kwamba corona ipo na watu wanaangamia kwa corona.

Kasema mengi na ninaamini mmeiona. Lakini hiyo mliyoiona imekatwa sehemu kadhaa.

Kwa mfano kuna sehemu askofu Jude Thaddaeus amesema kwamba nchi kadhaa duniani zimejikita kutafuta chanjo au kuipokea hiyo chanjo iliyopatikana.

Askofu kauliza kama nchi zingine zimefanya hivyo sisi Tanzania tunakwenda wapi?

Hapa dawa ni moja tu. Baraza la Maaskofu liweke clip nzima kwenye tovuti yake kuwakomesha hawa wanaosambaza hii iliyokatwakatwa.
 
Acha kusumbua watu, mbona wewe hujaweka hapa hiyo iliyokatwa katwa.
 
Itafute uweke, hakuna sheria inakuzuia kufanya hivyo hapa JF.
 
Hapa dawa ni moja tu. Baraza la Maaskofu liweke clip nzima kwenye tovuti yake kuwakomesha hawa wanaosambaza hii iliyokatwakatwa.
Hiyo tovuti si itapigwa na changamoto ya virusi hence kupelekea watu kukosa hata habari zingine ? Cha maana aendelee kuongea anachoamini popote pale atakapokuwepo ili hata wale wasio na uwezo wa kupata clip huenda mwisho wa siku watasikia (word of mouth) yaani mwambie na mwenzio
 
Cha kushangaza 'wanaoishi kwa sadaka' ndio wanaoogopa kufa kuliko wanaoishi kwa jasho lao.. Inaonekana huko madhabahuni ni kunono ndio maana wengi wanaogopa kupaacha na kwenda 'kwa Baba' wakihisi kule juu hawatapata maslahi manono kuliko wanayoyapata hapa Duniani!
Kuna mtu aliwahi kukuambia kuwa yawezekana ukawa wew ndiye mwenye akili kuliko wote kwenye ukoo wenu, sasa kama wew uko hivi vp wengine sasa
 
Anayevaa unajua analinda wengine kuliko kujilinda yeye hawa wamevaa ili wawalinde wengine lakini hawa ambao eti wamekuja kuwafariji wao hawajavaa (naweza kusema kwa mujibu wa Wataalamu huenda hawa wamekuja kuwaua hawa waliopatwa na majanga) kwahio hizo fariji zao bora wangekaa nazo.... (kwa mujibu wa WHO wanaoshauri kuvaa Barakoa na faida ya Barakoa)
 
Back
Top Bottom