Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

Asante Baba Askofu kwa kutimiza wajibu wako. Mchungaji mwema hulinda kondoo wake.
 
Tumeulizana leo asubuhi kuwa msimamo kamili ni upi kila tunapokutana Jumamosi kwenye jumuiya zetu

Leo katika Jumuiya yetu 70% ya wanajumuiya tulivaa barakoa na 30% hawakuvaa ndipo tukaulizana tutaendelea hivi hadi lini?
Kila upande ulikuwa na sababu zake za msingi na tukashindwa kuafikiana na tumekubaliana next saturday tutoke na msimamo wa pamoja.

Msimamo wa Kanisa ni kuvaa barakoa, na mkutano wa jumuiya ni wa kikanisa siyo wa serikali lakini baadhi ya wanajumuiya ni viongozi wa serikali.

Ushauri wenu tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
Sisi tushike imani yetu tu maana serikali mungu wenu ni tofauti. Labda Mungu wenu hajaridhika na kafara za kina Ben Saanane, Azory Gwanda Kanguye, Akwilini Akwilini mlizotoa hivyo anahitaji kafara zaidi ili awasikie.
 
Dini ya kiislamu huwa naikubali sanaaa waumini wake huwa hawajiulizi mara mbili mbili kati ya DINI na SERIKALI wafate lipi jibu lao nimoja2 'DINI'
 
Idiot, kwani serikali imekataza kuvaa barakoa????
Huna haja kutukana mkuu.

Ina maana umesahau kama Rais aliwahi kushambulia uvaaji barakoa? Umesahau kama Rais aliwahi hadi kumshushua spika sababu alikuwa amevaa barakoa bungeni? Baada ya hapo umewahi ona kuna kiongozi wa serekali anavaa barakoa?

Umesahau Meya wa mji wa Moshi aliwaamuru wajumbe wa kikao kuvua barakoa na asiyetaka atone nje ya kikao?

Hawa wote sio serekali? au ulitaka nani akataze ndio ujue serekali imekataza?
 
Hapo itategemeana na mwili wako ni wa nani Kama unamilikiwa na serikali sawa.
Afya ni yako unaeathirika ni wwe serikali haina hasara ukiondoka pengo lako linazibwa
 
Watu wanakufa huku, wewe unaleta hizo hekaya zenu za kwenye Biblia.
Acha uoga, wanaokufa wako ndani ya wigo wa kitakwimu za uzazi na vifo. Wakifa wawili wakazaliwa watatu hapo kimahesabu 'mzani unaenda vizuri.
 
Sawa dogo, ukikua utaacha
Ni nature, ndivyo Mungu alivyoumba Dunia akaiweka kwenye Ecosystem. Lazima kuwe na population balance. Waingie wengi, watoke wachache. The net effect population growth.
 
Mtume Paulo alipong'atwa na nyoka, alimtikisa yule nyoka akaanguka chini bila ya kuwa na hofu yoyote, lakini wale waliokuwa wamemzunguka walifikiri angepata madhara na kufa jambo ambalo halikutokea, wakaishia kumwona Paulo kama asiye mtu wa kawaida au mchawi. Kama viongozi wa dini na wenyewe wanapata hofu kama sisi tunaowazunguka badala ya kusimama kwenye nafasi zao kama mawakala wa Mungu nashindwa kuelewa. Imani yangu ni kwamba Yesu kama kuhani mkuu atasimama na chetezo chenye moshi wa uvumba kati ya waliokufa na walio hai na korona itakoma......
 
Na kiongozi mkubwa mmoja anasema “mwaka jana Mungu alituokoa na hili janga.....”

Wameanza kutoa damu masikioni. Watakiri kwa midomo yao kuwa hata mwaka jana hatukuwa tumeponywa, tulidhihaki jina la Mungu!!

Ugonjwa upo na tujilinde! Uwezo wa Mungu hatuna mamlaka nao, tufanye mambo tulio na mamlaka nayo!!
 
Fuata ulichoagizwa na kanisa. Kama huwezi toka katika Kanisa Katoliki jiunge na Dini iliyoanzishwa na Serikali.
 
Hajawahi kuomba fadhira yoyote toka serikalini.

Kama ni ile ndege ni JPM alijipendekeza mwenyewe kuipeleka.

Kanisa lisingekosa ndege ya kumsafirisha toka Moshi hadi Dar.

Vilevile jiulize kwa nini alianguka wakati jajawahi kuugua hivyo maishani mwake.


Atakumbushwa fadhira aliyopewa.

Ataambiwa hana shukrani. Lakini kwa askofu mwenye msimamo usioyumba kama huyu masimango hayamtetereshi.
 
Hili sasa ndio Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume la Roma ninalolifahamu Mimi. Misimamo thabiti, ya msingi kwenye ishu za msingi. Hakuna utani utani kwenye issues of principle.
 
Mkombozi ni MUNGU PEKEE
hizo nyingine ni mbwembwe
Kwahiyo Mungu ameshindwa kuwakomboa akina Kijazi? mkuu, Mungu hakuwapa akili kwa bahati mbaya, huko aliko atakuwa anawaangalia na kuwasikitikia msivyotumia akili alizowapatia mnabaki kumtupia lawama yeye.
 
Back
Top Bottom