Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

Askofu Ruwa'ichi: Asante mliovaa barakoa, nawalaumu msiovaa. Hali ni tete, tumetofautiana na Serikali

Kwa hyo wewe unaamini mzungu ndo atakuponya?
Duh Mkuu ukiumwa njaa si unatafuta chakula ?
Ukisikia kiu si unakunywa maji ?
Ukiumwa au ukiugua sio unafuata wataalamu wanasema nini ?

Je kufanya hayo juu yanakuzuia vipi kufuata Imani yako (iwe ni mizimu, kupiga ramli au chochote kile unachokiamini )?

Ila tatizo la magonjwa ya kuambukiza kama hili uzembe / ukaidi wako wewe sio risk yako pekee bali na wengine (yaani hapa ule msemo wa mchuma janga hula na wakwao, ndio mahala pake)
 
Lakini huu ugonjwa unaambukiza kwa njia ya hewa na madaktari wameshindwa kuudhibiti. Unadhani tumkimbilie nani?
 
Wameshindwa vipi kuudhibiti? Wameshakwambia Virus haina dawa ni mwili wako mwisho wa siku ndio unapambana (hivyo jali afya yako kula vizuri balanced diet n.k)

Wamesema wale ambao wapo vulnerable (wazee, wagonjwa n.k. ndio wanaathirika zaidi ingawa mtu yoyote anaweza kuondoka ) hivyo tufanye social distance ili tusiwaambukize wengi kwa wakati mmoja hata kupelekea Taasisi kuzidiwa hence kuweka watoa huduma kwenye hatari au watu kukosa huduma.

Chanjo haipatikani kwa siku mbili (inabidi kumjua kirusi alivyo na baada ya kupata chanjo inabidi kufanya research) kwa kawaida hii inachukua hata miaka kumi (ila kutokana na shida iliyopo ndio maana sasa hivi baada ya mwaka chanjo zimeanza kutoka ) hapa sio kwamba wameshindwa bali wamefanya kazi extraordinarily hata kupata matokeo kama haya (hivyo tuwapongeze na sio kuwabeza)

Kumbuka struggle is the duty na success ni matokeo, kupambana kutaendelea magonjwa yatakuja kwahio cha maana ni always kuwa tayari (kitu ambacho nadhani hatupo tayari) bora hii Corona na hii mortality rate yake, ikija Ebola hapa na huu mzaha mzaha wetu si huenda tukawa historia ?
 
Magufuli ni jasiri anafundisha na kusimamia anachokiamini, anasema Mungu anaweza yote na anaonyesha kwa vitendo. Hao viongozi wa dini ni wanafiki, wanasema Mungu anaweza yote mioyoni mwao wamembeba Mungu asiyeweza yote.
 
Unasimamia unachokiamini wewe kwa manufaa yako (huenda wewe unaweza kupita kwenye moto na usiungue) fair to you na imani yako.

Ila kuwaambia wengine wapite kama wewe kwenye moto eti hawataungua wakati wanaungua na wanakufa (that is being irresponsible).
 
Mimi ni muislamu lakini lazima niseme ukweli kabisa hawa viongozi dini zingine lazima niwape salute. Nawaheshimu sana mara nyingi wanasimama katika misingi ya imani zao na kama viongozi na nadhani kinachowasaidia sana katika hili wao wanateuliwa na mamlaka ya Vatican na sote tunajuwa tech ile ni nchi wanakuwa loyal na wakubwa wao wa Vatican.

Sasa sisi wenzangu namie teule zetu hazina tofauti na wakurugenzi, lazima watii maana wanajuwa chaguzi fake fake tu kuwa pale walipo vipesa vya mboga kibao hatuna ubavu huo na ukijitahidi basi juwa utaishia segerea tu.

Kama Mufti anasoma au kamuona kiongozi wa Catholic akiongea basi aibu juu yake. yeye juzi kaenda na barakoa msikitini lakini kuongea kama kiongozi kuwataka watu wavae barakoa kama hajaona wala kuongelea changamoto hizi kama kiongozi wa dini.
 
Bahati maneno ya busara kama haya hakuna wa kuyatangaza kila mtu anaogopa ila hapo ingekuwa habari ya udaku inge trend wiki nzima. ndio Taifa la Tanzania hii clip kamili ingefika kila sehemu kwenye TV, Radio na magazeti ingeweza kuokoa hata hicho kidogo.
 
Its sad pale viongozi wa kiroho wanapohamisha imani yao toka kwa Bwana Yesu na kuipeleka kwenye barakoa.. Ndipo Yesu akawakemea wafuasi wake akisema, hata baada ya kukaa na mimi sikubzote hizi, bado tu hamjanifahamu vizuri?
View attachment 1707058i peke yake, Biblia inasomwa na
Biblia sio kitabu cha kunyofoa aya moja na kuisoma kisha kuitafsiri peke yake, Biblia husomwa na kutafsiriwa kwa ujumla wake. Viongozi wa dini ni wataalamu wa Teolojia, huwezi kushindana nao kwa kuwa umesoma aya moja na kuiletea tafsiri yako
 
Nimewafungia kabatini wateule wangu wote. Wao hunisikiliza Mimi tu, nikisema nimeishinda corona wote wataamini hivyo na hawatajikinga.
"Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu,mimi nalikuja ili wawe na uzim,kisha nao tele.Mimi ndimi mchungaji mwema.
Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si Mchungaji ambaye kondoo si mali yake humuona mbwa mwitu anakuja akawaacha kondoo na kukimbia. Na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara, wala mambo ya kondoo si kitu kwake" (YOHANA 10:10-15)
 
Watumishi wa matumbo yao, ni heri wangekuwa kwenye field nyingine kabisa maana kumtumikia Mungu sio kula na kunywa. Kipindi kama hiki ndio tutajua watumishi wa Mungu wa kweli na wale wa Baali (Ibilisi).
 
Back
Top Bottom