Askofu Zakaria Kakobe Aungana na Tundu Lissu: Ni Kuhusu Tanganyika na Zanzibar. Afafanua kwa mapana

Askofu Kobe ana laana ya kutelekeza mtoto wake wa damu, lissu naye risasi za mbowe zilimlemaza sio miguu tu Hadi ubongo zililemaza, asa ukiwasikiliza watu hawa na ukawaelewa basi ujue uwendawazimu unakunyemelea.
Kama risasi zikamlemaza Lissu ubongo halafu bado mnashindwa kujibu hoja zake, basi nyie mtakuwa ndio mazezeta kabisa.

Na huyo mtoto wa damu aliyetelekezwa na Kakobe, wewe ndie mama wa mtoto?!
 
Ukweli ni kwamba Muundo wa Muungano wetu ni wa kipekee, pengine kidogo unaweza ukawa unafanana na ule uliokuwa wa Senegal na Gambia.

Kama alivyouliza Askofu, ni jambo la kushangaza kwamba kwa upande wa bara, mambo yasiyo ya muungano yanasimamiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano. Hata kuna nyakati ambazo Wizara ambayo si ya muungano inasimamiwa na Waziri kutoka upande wa Zanzibar, mfano Mbarawa ashawahi kuwa waziri wa wizara ya maji.

Kwanini nguvu kubwa itumike kulinda jambo ambalo kwa macho ya wengi linaonekana lina kasoro, kuna haja gani ya kuongoza watu wanaonung'unika? Kwanini isifanyike kura ya maoni kuamua kama kuna haja ya kuwa na Muungano au la, kama haja ipo ndipo turudi kwenye muundo wake.

Hili la Muundo wa Muungano ndo lilikuwa sababu kubwa ya Bunge la katiba kuvurugika. Kama alivyosema Askofu hapo juu, jambo hili tunaliahirisha tu ila kiukweli litakuwa linatuwinda na kujadiliwa kila wakati.

Mungu ibariki Tanzania na Watanzania.

Ahsante.
 
Asante kwa kufafanua vizuri
 
Back
Top Bottom