Askofu Zakaria Kakobe Aungana na Tundu Lissu: Ni Kuhusu Tanganyika na Zanzibar. Afafanua kwa mapana

Askofu Zakaria Kakobe Aungana na Tundu Lissu: Ni Kuhusu Tanganyika na Zanzibar. Afafanua kwa mapana

Askofu Kobe ana laana ya kutelekeza mtoto wake wa damu, lissu naye risasi za mbowe zilimlemaza sio miguu tu Hadi ubongo zililemaza, asa ukiwasikiliza watu hawa na ukawaelewa basi ujue uwendawazimu unakunyemelea.
Mimba zilizizoharibikiwa zikazaliwa kwa bahati mbaya mnakera sana kwa hoja zenu za makalioni
 
Mama apige kimya tu mpaka watachoka! Na angefanya haraka DP World waanze shughuli pale!
DPW ni karata yake mbovu ya kummaliza kisiasa.
Hadi sasa hana ujasiri wowote.

Nyie mpeni kiburi akaze fuvu hamjui kuwa huu ni mtego toka kwa wanaccm kindaki ndaki?
Mnafikiri eti wapinzani ndio tunapinga DPW.
Subiria mtaona muda si muda
 
Safari hii kazi wanayo, wakisema ni upepo tu, matokeo yake ndio kila wengi wanazidi kuibuka kadri siku zinavyosogea..
Huu si upepo. Huu ni uhalisia. Mkataba watanzania wanasema haufai. Unahitaji marekebisho.
Mwenye masikio na asikie
 
Ukweli ni kwamba Muundo wa Muungano wetu ni wa kipekee, pengine kidogo unaweza ukawa unafanana na ule uliokuwa wa Senegal na Gambia.

Kama alivyouliza Askofu, ni jambo la kushangaza kwamba kwa upande wa bara, mambo yasiyo ya muungano yanasimamiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano. Hata kuna nyakati ambazo Wizara ambayo si ya muungano inasimamiwa na Waziri kutoka upande wa Zanzibar, mfano Mbarawa ashawahi kuwa waziri wa wizara ya maji.

Kwanini nguvu kubwa itumike kulinda jambo ambalo kwa macho ya wengi linaonekana lina kasoro, kuna haja gani ya kuongoza watu wanaonung'unika? Kwanini isifanyike kura ya maoni kuamua kama kuna haja ya kuwa na Muungano au la, kama haja ipo ndipo turudi kwenye muundo wake.

Hili la Muundo wa Muungano ndo lilikuwa sababu kubwa ya Bunge la katiba kuvurugika. Kama alivyosema Askofu hapo juu, jambo hili tunaliahirisha tu ila kiukweli litakuwa linatuwinda na kujadiliwa kila wakati.

Mungu ibariki Tanzania na Watanzania.

Ahsante.
Kusema kweli, Kakobe kaongea maneno machache lakini ana hoja nzito
 
DPW ni karata yake mbovu ya kummaliza kisiasa.
Hadi sasa hana ujasiri wowote.

Nyie mpeni kiburi akaze fuvu hamjui kuwa huu ni mtego toka kwa wanaccm kindaki ndaki?
Mnafikiri eti wapinzani ndio tunapinga DPW.
Subiria mtaona muda si muda
Wachache Ndio watakuelewa. Most of people don't know how the game is
 
Muungano utavunjika na wala hakuna mtu atalala njaa ...Na taratibu tutaanza kugawa kanda kila mtu akae kwao ...Na wale wageni wengi wataanza kuondoka kabisa.

Ni ujinga kwa vile hata hao waliounganisha watu washakufa naona ,leo wanakuja watu na ujinga .

Kingine hata iweje hatuwezi kuongozwa na Chadema labda wagawe nchi yao ya kaskazini lakini kutawaliwa na wabaguzi hatutaki.
 
Back
Top Bottom