Wakuu kwema,
Kuna laki moja hapa nataka nimpe mtu akale na wana wake. Ili uipate nahitaji uniwekee aya, mstari au sura ndani ya Quran au Biblia inayoonesha mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini au walifungishwa ndoa na Mtume, nabii au Kuhani?
Sihitaji Hadithi au andiko lisiloonyesha ninachokizungumza moja kwa moja.
Nimesema nukuu itoke kwenye Biblia au Quran si kwamba siheshimu dini zingine hapana, hivi vitabu ndivyo navifahamu.
Asante.
Kwenye uislam sio lazima sheikh kufungisha ndoa. Masheikh wamekuwa wakifungisha ndoa kwa niaba ya mawalii incase walii anaupunguf wa elim
Kweny uislam hizi ndo sharti za ndoa:
Mwanamke awe Muislamu au Mtu wa Kitabu (kwa maana awe Myahudi au Mkristo) mfuasi wa dini yake. Lakini Uislamu unatuhimiza kuchagua mwanamke Muislamu mfuasi wa dini, kwa sababu yeye atakuwa mama mlezi wa watoto wako, na msaidizi wako katika mambo ya kheri na msimamo wa kufuata dini. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Basi wewe mpate (muoe) mwenye dini». (Bukhariy, Hadithi Na. 4802. Muslim, Hadithi Na. 1466).
Mwanamke awe mwenye kujiheshimu, mwenye kujihifadhi. Ni haramu kumuoa mwanamke anayefahamika kwa mambo machafu na uzinzi, kama alivyosema Allah Mtukufu kuwa: «Na (mmehalalishiwa pia kuoa) wanawake waumini wenye kujihifadhi, na pia wanawake wenye kujihifadhi miongoni mwa wale ambao walipewa vitabu». (Almaaida, aya 5)
Mwanamke asiwe miongoni mwa Maharimu zake ambao ni haramu kwake kuwaoa uharamu wa kudumu Pia ni haramu kuoa kwa pamoja mtu na dada yake au mdogo wake, au shangazi yake, au mama yake mdogo au mkubwa.
Ni sharti kwa mwanaume awe Muislamu. Ni haramu katika Uislamu mwanamke wa Kiislamu kuolewa na kafiri; vyovyote dini yake iwavyo, awe Mtu wa Kitabu au sio Mtu wa Kitabu
Ndoa inakamilika kwa Walii kumtamkia mwanaume kwamba: Nimekuoza binti yangu, au dada yangu, na amtaje kwa jina lake. Na mwanaume atasema kwamba: Nimekubali au nimeafiki. Mkataba wa ndoa utakuwa umekamilika kwa kutumia maneno haya au maneno mengine yenye maana hiyo kwa lugha yoyote ambayo watu wanaifahamu.