Atakayenionesha andiko linalosema mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini nampa laki 1 akale sikukuu

Atakayenionesha andiko linalosema mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini nampa laki 1 akale sikukuu

Kwa mwaka uliopita wa 2022 inaonekana watu wengi hapa JF wanapenda kusoma Biblia. Endeeleni kusoma Biblia kuna sehemu Mungu atawafikisha. Maana mada nyingi ni kuhusu Biblia.
 
Wakuu kwema,

Kuna laki moja hapa nataka nimpe mtu akale na wana wake. Ili uipate nahitaji uniwekee aya, mstari au sura ndani ya Quran au Biblia inayoonesha mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini au walifungishwa ndoa na Mtume, nabii au Kuhani?

Sihitaji Hadithi au andiko lisiloonyesha ninachokizungumza moja kwa moja.

Nimesema nukuu itoke kwenye Biblia au Quran si kwamba siheshimu dini zingine hapana, hivi vitabu ndivyo navifahamu.

Asante.

Naona unaomba Jambo ambalo halipo. Ndoa inafungishwa na Mungu mwenyewe na wanandoa wanakamilisha kufungwa kwa ndoa kwa tendo la ndoa.

So tofautisha kufungwa kwa ndoa na kudhibitishwa kwa ndoa. Wachangaji na mapadri wanadhibitisha ndoa ila hawafungi ndoa.
 
Andiko kama halipo watu wanatumia dini kuwa control watu kama kulikuwa na ulazima mungu angesema
Yesu alikuwa anapenda sana kwenda katika harusi kuna harusi moja alikwenda kama ingekuwa lazima viongozi wa dini kuwafungisha watu ndoa ndio mungu akubali basi siku ile Yesu angefungisha lakini alifanya jambo alilopenda mwenyewe walimuuliza mama ake aliwaambia atakalofanya msikilizeni basi akageuza maji kuwa pombe hapa inaonyesha jamaa kwenye mambo ya pombe yupo poa na itakuwa alikunywa tu

Muhamad alimuoa Khadija mwanamke tajiri kama Leo tunasema zali la mental kwa maana muhamad alikuwa kapuku hana hata hela unaambiwa iyo hela ya mahari katoa khadija je huyo aliefungisha ndoa yake alikuwa sheikh gani?

Ukija kuangalia hayo matukio utakuja kugundua hakuna ya haja ya mchungaji au sheikh au padri au kiongozi yoyote wa dini kuwafungisha watu ndio maana Yesu mwenyewe kaenda katika harusi hakufungisha watu ndoa sana sana kageuza maji kuwa pombe na Muhamad kama mwenyewe kiongozi hajafungishwa na sheikh hakuna ulazima wa sheikh kutaka kufungisha watu ndo nyie wakristo na waislam mumepata wapi huo utaratibu ?

muhamad alifungishwa ndoa na abubakar wakati anamuoa khadija
 
Mimi najua tu ile tu ya Kana ambapo Bwana Yesu alialikwa na kutengeneza mvinyo
Yes hakualikwa kwenye ndoa, Kana ilikuwa harusi. Ambayo ni sherehe baada ya ndoa (lugha inayotumika siku hizi). Hiyo ndoa ya hao maharusi ilifungwa? Ilifungwa na kiongozi was dini au Yesu? Taratibu za kufunga ndoa zilikuwaje?
 
Siyo kweli, mnaweza kutambulika kama mme, na mke, ila siyo wana ndoa, Ndoa ina misingi yake.

Serikali inatambua aina tatu kama siyo nne za ndoa.
1. Ndoa kidini
2. Ndoa ya kiserikali
3. Ndoa ya kimila
Sasa ukiangalia hapo utaona hakuna ndoa ya mme na mke ya kuishi mda mrefu, na ukienda kuomba cheti serikalini hutapewa mpaka mfungoshwe ndoa.
Swali la mtoa mada ni kwamba, hiyo ndoa ya kidini msingi wake ni andiko lipi kwenye biblia?
 
Nimeshaisoma Biblia Yote ya vitabu 66 na Ile ya 72 zote hakuna kitu kama hicho.

Hayo ni Mapokeo tuu.
Mbinu za dini kuteka waumini wapya watakaozaliwa kwenye Ndoa
Naona wewe ndio unaleta siasa.
Kasome Mathayo 18:18 na Marko 10:9.
Hamuezi kujiendeshea mambo kama mbuzi ilhali mna utashi.
 
Naona wewe ndio unaleta siasa.
Kasome Mathayo 18:18 na Marko 10:9.
Hamuezi kujiendeshea mambo kama mbuzi ilhali mna utashi.

Nakuwekea hayo maandishi hapa;
Mathayo 18:18-20 BHN
“Nawaambieni kweli, mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni. Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo. Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao.”

Marko 10:9 BHN
Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe.”

Mchungaji au askofu sio anayeunganisha Ndoa, Nafsi zenu na maamuzi ya wanandoa ndio yatafanya Mungu aunganishe ndoa.na sio MTU asiyehusika.

Hizo Aya hazijataja Mchungaji au askofu, au Kuhani, au kiongozi yeyote WA dini Afungishe Ndoa.

Ndoa ni baina ya Watu Wawili, BAADA ya kupendana hatua inayofuata ni Kutambulishana Kwa Wazazi. Mchezo umeishia hapo, wazazi watapendekeza Mahari kulingana na tamaduni husika.
Hakuna Aya yoyote kwenye Biblia inayowaamrisha Watu wafungishwe ndoa Kanisani au na viongozi wa Dini.

Huo utaratibu ni wamadhehebu, sio Sheria za Biblia. Ni Mapokeo.
Tofautisha Mapokeo na SHERIA.

Nakupa mfano mwingine,
Sio lazima MTU akifa ATI Mchungaji au askofu au Kuhani au Nabii akafanye mazishi.
Hayo ni mambo ya kifamilia.
Hata MTU akizikwa na wanafamilia wenyewe Kwa utaratibu watakaoona unafaa ni Sawa
 
Sawa nimekuelewa ROBERT HERIEL
Lakini hoja yangu ni kwamba kutokana na vifungu hivyo. Kama kuna utaratibu wa kufanya na ufuatwe.
Ndio maana hao viongozi wako. Kwa mantiki hio basi hakuna haja ya kwenda nyumba za ibada ikiwa mambo yanafanyika inavyotupendeza.

Aki nashindwa kuwasilisha hoja. Ila nielewe kama nilivyoandika. Wewe piah uko sahihi. Mimi hoja yangu iko kuhusianisha maana hayo mapokeo yamekuwa derived kutoka vitabu vya dini, na ndio msingi wake. Ingekuwa hakuna pahala pa kutolea hata hayo mapokeo. May be ingekuwa ni batili kweli.
 
Ukisema kila kanuni na taratibu zinazofanyika makanisani zimeandikwa wapi kwenye biblia utapata tabu Sana...Biblia ni Muongozo kama ilivo KATIBA na Sheria zinavotungwa nchini zinafuata KATIBA.
Makanisa yanatengeneza Miongozi,kanuni na taratibu za Mambo mengi kufanyika kanisani ikiwemo suala la ndoa.Mwanzilishi wa ndoa asili yake ni Mungu .So Mambo ya Mungu yanaanzia makanisani..ni utaratibu tu.
 
Sawa nimekuelewa ROBERT HERIEL
Lakini hoja yangu ni kwamba kutokana na vifungu hivyo. Kama kuna utaratibu wa kufanya na ufuatwe.
Ndio maana hao viongozi wako. Kwa mantiki hio basi hakuna haja ya kwenda nyumba za ibada ikiwa mambo yanafanyika inavyotupendeza.

Aki nashindwa kuwasilisha hoja. Ila nielewe kama nilivyoandika. Wewe piah uko sahihi. Mimi hoja yangu iko kuhusianisha maana hayo mapokeo yamekuwa derived kutoka vitabu vya dini, na ndio msingi wake. Ingekuwa hakuna pahala pa kutolea hata hayo mapokeo. May be ingekuwa ni batili kweli.

Upo sahihi.
Ila hoja ya Mtoa Uzi ilitakiwa kujibiwa kuwa Hakuna Aya yoyote kwenye Biblia inayompa Mamlaka Mchungaji, kuhani, askofu, padri na viongozi wengine Kwa majina Yao kufungisha Ndoa.
Ila ni utaratibu wa makanisa mengi waliojiwekea.
Kumaanisha kufunga ndoa hata nje ya Dini sio dhambi wala sio kosa.

Kama wanavyojaribu kuaminisha wachungaji kuwa Watu ambao hawajafunga ndoa Kanisani ATI wanazini Jambo ambalo sio kweli.

Mwanaume na Mwanamke wakishakubaliana kuishi kindoa, hiyo tayari ni Ndoa. Bila kujali wameenda Kanisani, msikitini, serikalini au wapi.
Ndoa inahusu Watu Wawili na kama itatokea nyongeza basi wazazi wa Pande mbili.

Mambo ambayo yanapaswa kufundishwa kwenye nyumba za ibada, ni ishu ya Torati, na visa vya Biblia Kwa kuvihusisha na Maisha ya kileo.

Mambo mengine kama Ndoa, Afya, mahusiano, uchumi, Sayansi, sheria, teknolojia n.k hayo yanafundishwa nje ya kanisa, lakini bila kuvunja sheria kuu za Mungu ambazo ni Torati.
 
Basi kwa mantiki hio, hakuna kifungu ambacho moja kwa moja kinaelekeza hayo.
Ila kwa swala la ndoa kwamba wanandoa ambao hawajafungia ndoa kanisani ni wanazini, ndio nasikia kwako.
ROBERT HERIEL
Mimi nimeelewa. Shukurani.
 
Shukrani Sana.
Hujasikia majina wanayopewa Watu walioamua kuishi kindoa?
"Wamesogezana"
"Sogea tuishi"
" Wanaishi kiharamu bila ya ndoa"
" Wanafanya zinaa, mpaka Wabariki ndoa"

Mwanamke na Mwanaume hawawezi ishi pamoja kama hawajafunga ndoa, yaani hawajakubaliana kuishi pamoja.

Tofautisha na wale wanaonunua Makahaba, hiyo inajulikana.
 
Sio tuu kifungu kinachoelekeza hayo.
Bali pia hakuna hata kisa kimoja cha manabii au makuhani au walioandikwa kwenye Biblia ambao ndoa zao zilifungishwa na Makuhani au viongozi wa Dini.
Hii inamaanisha sio sheria/sio lazima.

Ila kama MTU atapenda kufanya afanye lakini akae akijua haina tofauti na ambaye hajafanya
 
Mimi nljua unamzungumzia ndoa inayotambulika ni ya Kikristo Hapo ningesema sio.
Ila hao sogea tuishi ni kweli wanazini, maana utaratibu haujafuatwa. Na kumbuka kwenda kinyume na utaratibu mliojiwekea ni ukosefu wa nidhamu, simply ni dhambi. kama lengo lao ni ndoa kwa nini wasifuate utaratibu? Watambulishane kwa jamaa na ndugu vinginevyo ni sawa na kula chakula cha wizi ndio hutaki wengind wafahamu.
 
Lakini Biblia yenyewe imeandika, yaliyomo humu sio matukio yote yaloweza kutokea kipindi, bali yale tu yalionekana kuwa yafaa. huenda ilikuwa hivyo sema waandishi hawakuona umuhimu wa kuandika hayo.
Je Wayahudi utaratibu wao kuhusu ndoa ukoje?
 
Wakuu kwema,

Kuna laki moja hapa nataka nimpe mtu akale na wana wake. Ili uipate nahitaji uniwekee aya, mstari au sura ndani ya Quran au Biblia inayoonesha mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini au walifungishwa ndoa na Mtume, nabii au Kuhani?

Sihitaji Hadithi au andiko lisiloonyesha ninachokizungumza moja kwa moja.

Nimesema nukuu itoke kwenye Biblia au Quran si kwamba siheshimu dini zingine hapana, hivi vitabu ndivyo navifahamu.

Asante.
Kuna laki mbili kwa atakayeleta fungu la biblia linatuambia Yesu alizaliwa tarehe 25/12
 
Mimi nljua unamzungumzia ndoa inayotambulika ni ya Kikristo Hapo ningesema sio.
Ila hao sogea tuishi ni kweli wanazini, maana utaratibu haujafuatwa. Na kumbuka kwenda kinyume na utaratibu mliojiwekea ni ukosefu wa nidhamu, simply ni dhambi. kama lengo lao ni ndoa kwa nini wasifuate utaratibu? Watambulishane kwa jamaa na ndugu vinginevyo ni sawa na kula chakula cha wizi ndio hutaki wengind wafahamu.

Kuzini ni neno linalohusiana na Sheria za dini.
Mwanaume na Mwanamke wakikubaliana kuishi pamoja tayari ni Ndoa. Hakuna nje ya hapo.
Kisheria za Mahakama hakuna msamiati Kuzini.

Ndio maana nikakuambia Kwa waumini WA dini za kanisa wao Kuzini wanamaanisha MTU kutokufunga ndoa Kanisani.
Jambo ambalo tayari nimeshasema ni uongo
 
Back
Top Bottom