Mkuu Hata ya wakristo pia ningeweza kujibu kwa kuwa na ufahamu mzuri wa dini hiyo..
Katika ndoa zote za Mtume muhamadi ndoa kama sikumbuki vizur 12
Ni moja peke yake ndo alifungishwa na ndo kama nilivyoelezea hapo nyuma kuwa ni misingi ya kiislamu ndoa ifungishwe na walii(Walii ni baba wa mwanamke,Kaka yake, babu kama hawapo wote basi mjomba wake kama hayupo bhasi mwenye kuchukua jukumu hiko huwa ni Qadhi)
Kwa hiyo Mtume alifungishwa ndoa yake ya 1 na bi Khadija na aliyewafungisha alikuwa mjomba wake na bi khadija Aitwaye Waraqa ibn Nawfal
Ama kuhusu ndoa zingine aliwatwaa wanawake na tanko la mke likafuata...
Hakuna aya hiyo na wala hutaipata popote na ndo maana nimenza kwa mlolongo wa walii..
Anyway sharti za ndoa kukubalika (kuswii) katika dini ya kiislamu ziko tano
- Iwepo ridhaa ya mwanaume na mwanamke both side
Hapa namaanisha mkuu hakuna janja ya nyani...lazima mwanamke akubali kuolewa na wewe na lazma mwanaume akubali kuoa kama kuna mmoja atakataa kuolewa au kuoa bhasi ndoa kwisha kazi yake haitafungwa
(Najua kuna wale wakubisha basi someni sahihi AlBukhari Hadithi Na. 4843)
Kama nilivoelezea nyuma kidgo hapo walii ni ndugu mwanaume wa karibu kwa mwanamke, kama vile baba yake ,kaka yake wa kuzaliwa,hata babu yake.
Na ni lazima Walii awepo na akubali,Na ndio mfungishaji wa ndoa na akikataa kufungisha ndoa hakuna..Na mtume mwenyew alisema pasipo kuwepo walii ndoa hiyo ni batili na hakusema pasipo kuwepo kwa sheikh alisem waliii nakazia..kwa wale wenye kubisha jamani nawapa vitabu
(SUNANAbuudaud, Hadithi Na. 2085. Tirmidhiy, Hadithi Na. 1102) .
Japo kama hakuna walii aliyepatikana wa dini ya kiislamu kwa mfano watu wanasilimu sasa hivi na gule mtoto wa nje ya ndoa na wale wengine wote ambao hawana ndugu bado wamekumbukwa sasa hapo Qadhi au sheikh au imam atachukua sehemu ya walii na atakuwa walii iki kufungisha ndoa
jamani kwa wabishi tena soma
(Tirmidhiy, Hadithi Na. 1084. SunanIbnmaaja, Hadithi Na. 1967).
- kuwepo kwa mashahidi mawili.
Uislamu unaweka sharti kwamba ndoa itangazwe kwa watu na kufanyika hadharani ili kuondoa tuhuma kwa mume na mke. Kiwango cha chini sana cha kutangaza ndoa ni kuwepo kwa mashahidi wawili wanaoshuhudia kufungwa kwa ndoa.
- Awe ametimiza masharti ya kuolewa
Hapa ikiwemo umri,Awe mwislamu au mkristo(alkitaba),Awe na akili timamu
- Apewe mahali yake
- Na isomwe hotuba
Sio lazma sheikh na nimetoa uthibitisho chief
Shukran