Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Huwezi kupiga ramli ukaviona mwenyewe? [emoji23]
Acha mbambamba watu tunazitaka hizo 25m
Nipo hapa na mjukuu wa adui chongo Zenji anasubiria data lete jina yako na la bi mdashi wako. Ila kama unajiamini wewe ni mtoto wa baba ako kweli hata la mdingi litafaa.
Majini wanatembelea ramani ya nasaba
 
Sasa mtu akiweka jina hata majambazi unaweza kumtumia.

Kwani uchawi wako hauwezi kupata jina la mtu kwa kuangaliamuandiko wake hapa?
Haya tuma inbox sasa.
😅😅😅muandiko upi sasa maana wote tuko na keyboard.
Tatizo ni kubwa sana wakoo,kwa fikra hizi bado sanaa sanaa
 
Sasa wewe kama.mchawi unashindwaje kumjua huyu mtu. hadi uambiwe jina.
Kila kitu huendeshwa kwa utaratibu,si unataka kulogwa fuata utaratibu. Maana yeye ndo keshasema hakuna wa kumtengeneza basi aandike jina hapo
 
Haya tuma inbox sasa.
😅😅😅muandiko upi sasa maana wote tuko na keyboard.
Tatizo ni kubwa sana wakoo,kwa fikra hizi bado sanaa sanaa
Kwani nikikutumia inbox wewe huwezi kuwa ndiye jambazi mwenyewe?

Ukisikia muandiko wewe unaelewa nini? Unaelewa digital forensic ni nini? Unaelewa Unabomber alikamatwaje?

Kama watu wanaweza kutumia sayansi tu kumjua mtu kwa anachoandika kama ilivyokuwa kwa Theodore Kaczynski, nyie mnaosema mna uchawi mnashindwa vipi kumjua Kiranga ni nani kwa kuangalia anachoandika?

Unamjua Theodore Kaczynski? Unajua alikamatwaje?

Hapo fikra za nani ndiyo bado?
 
Usilete historia,huwezi pimiwa mchele kituo cha mafuta.
Kasema halogeki, ndo maana wakuu wa kazi wakamuomba hizo kitu tatizo like wapi mbona ni kama mnataka kututoa kwenye reli ya mada.
 
Usilete historia,huwepi pimiwa mchele kituo cha mafuta.
Kasema halogeki, ndo maana wakuu wa kazi wakamuomba hizo kitu tatizo like wapi mbona ni kama mnataka kututoa kwenye reli ya mada.
Habari za kulogana ni ujinga tu.

Na ujinga huu unaanza kuthibitika mnapoanza kuomba majina, mnathibitisha uchawi wenu hauwezi kujua watu majina.

Mngekuwa na uchawi kweli, mngenuiza tu kwenye uchawi mpewe jina la Kiranga, lingekuja kamili mpaka fingerprint mngepata.
 
shuleni walisomea ujinga
 
Hello Africans.

Hakuna binadamu ninaowadharau kama wanaoamini mauchawi na mauganga.

Huwa nawaona ni watu wenye kasoro kubwa kichwani na wameoza kiasi kwamba hata uwaambie nini huwezi kuwabadili imani.

Hizi imani pumbavu zinaonesha vile Africans tuko na IQ ndogo. Na ndio maana pamoja na utajiri uliopo ktk hili bara tunateseka na shida karne kwa karne huku wenzetu wasioamini haya maujinga wakituacha mbali kwa maendeleo. (Najua kuna wazungu wachache vichaa pia wanaamin ushirikina).

Ukweli hizi imani zinanikera sana maana mbali ya kuchelewesha maendeleo ya hili bara pia ni hatari. Tushaua sana wenzetu wasio na hatia sbb ya hizi imani pumbavu. Albino, Vipara, wazee with red ayes na wengine wengi.Upumbavu mtupu.

Mimi binafsi nilishahama sehemu kwa kusingiziwa eti mimi ni freemason. Nilifanya kosa nikaporomosha hekalu wanakoishi wajinga. Mjengo wetu uko tofaut by far na nyumba zingine zote.

Wale wapuuzi walishindwa kujua kuwa kufanikiwa hakuna uchawi bali janja janja na timing kwenye fursa, basi yenyewe yakajiongoza eti hapa ni masonic na makafara tu.

Mwanzoni niliwapuuza ila badae kuna kitu ilitokea nikaona hawa wapuuzi kuna siku wanaweza wakajiunga wakanichoma mle ndani wakiamin mie natoa damu za watu kafara.Ikabidi niondoke.

Yupo mfanyakazi wangu alinichana Live kuwa "boss najua huwez kutoa siri zako ila siwez amini umefika hapa ulipofika bila ndumba kuhusika"

Mimi siamini kama kuna mtu yeyote anayeweza fanya kitu digits zangu bank zikaongezeka. Siku zote ninaamini katika kutumia akili ktk kutafuta.

Pia siamini kama kuna mjinga yeyote anayeweza kuniloga kitu kibaya kikanipata sbb havifanyi kazi. Mnadanganywa tu.

UCHAWI NA UGANGA NI UONGO havipo na havifanyi kazi. Mpo wengi humu mnaoamini hayo matakataka sasa nawapeni ofa ya 25M kwa atakayeweza kuniloga.

Nifanyeni chochote kibaya na mhakikishe hamnisamehi mpaka nije hapa niandike uzi wa kuomba msamaha na kukiri kuwa kweli uchawi upo nimelogwa na pia nilipe hiyo 25M kwa mchawi wangu.

Mkitaka niwatukane babu na bibi zenu wanaoogopwa kwa uchawi ili hasira ziwapande mniloge vizuri semeni. Nitawavurumishia mitusi hao babu/bibi zenu hamjapata kuona. Nitawatukana na kuwakashifu ma hawatanifanya chochote wajinga hao[emoji23]

Haya kazi kwenu.

NILOGENI

UPDATE:Mnaotaka jina ili mniloge siwezi kuwapa sbb ua Privacy ila nawawekeeni picha yangu muitumie kuniloga. Kateni mikono,vidole,nifanyeni niwe na miguu 4 kama ng'ombe vyovyote.

View attachment 2615624

Naomba jina la baba yako na mama pm na advance nikakushuhulikie
 
Habari za kulogana ni ujinga tu.

Na ujinga huu unaanza kuthibitika mnapoanza kuomba majina, mnathibitisha uchawi wenu hauwezi kujua watu majina.

Mngekuwa na uchawi kweli, mngenuiza tu kwenye uchawi mpewe jina la Kiranga, lingekuja kamili mpaka fingerprint mngepata.
Sasa kama huamini uchawi kwamba upo na unatenda hiyo imani ya kunuiza na kitu kikaja wewe umeitoa wapi.
Kwa herini maana nishawaambia mnaopinga wote ninyi kwenye masuala ya ufahamu wa mambo ni weupe tuu
 
Neno Kunuiza ni sawa na neno dragon.
Vipo lakini havipo
 
Back
Top Bottom