Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Sasa kama huamini uchawi kwamba upo na unatenda hiyo imani ya kunuiza na kitu kikaja wewe umeitoa wapi.
Kwa herini maana nishawaambia mnaopinga wote ninyi kwenye masuala ya ufahamu wa mambo ni weupe tuu
Wapi nimesema ninatenda hiyo imani ya kunuiza?

Wewe unajua hata kusoma kwa ufahamu au ni ngumbaru usiyejua kusoma kwa ufahamu?
 
1.kumbe mwanamke dah! me nilijua kidume
2.yaani mpaka leo hujajua tu kwamba ulisharogwa? hebu fanya ihsani kawape mil 25 zao wale waliokufanya uhame hekalu lako
3.wachawi mnakwama wapi aisee utajiri nje nje huu
 
Jidanganye,uchawi hutumia majini ambayo husafiri.Na pia unalogeka ukiwa na sababu mda mwingine,Mara nyingi uchawi usio wa kawaida ni kuharibiana nyota,familia za kiafrika hatupendani,watakuonea wivu ili wakuibie nyota.
 
uchawi/mchawi siyo kujua kila kitu acheni hayo mawazo, uchawi ni kufanya/kujua jambo tofauti na kawaida na huwa ni kwa msaada wa mashetani ya kijini.

huyo mchawi anachagua jambo maalumu analolitaka kisha shetani anamsaidia chap. na wala siyo kila jambo atakalotaka basi shetani ataweza kumfanyia/kulifanikisha laa! kuna mengine anapigwa puu tu ndomana mnahimizwa kujiweka safi mda wote, kujiombea dua na kuepuka mambo maovu mda wote kwani ndiyo yanayofanya shetani adunde akikujia

mfano mganga anataka kujua fulani yupoje basi shetani atakwenda kwa spidi ya mwanga kumpeleleza huyo mtu yupoje na kwa vile hiyo siyo kazi kubwa kwa haraka tu analeta majibu. watu kwa kutokuelewa wanabaki kumsifu tu mganga anajua siri kumbe hawajui kwamba kajuzwa na shetani.

wakina kiranga wao wanadhani mtu akiwa mchawi basi anaamua tu lolote na likawezekana mfano kuhack akaunt za fedha, aende popote atakapo kwa muda wowote, anajua mtu anachowaza, ajue kila siri... no huyo sasa atakuwa siyo mchawi tena bali ni mwenyezimungu


hayo mambo yote wanayofanya wachawi na mashetani yao hayafanikiwi ila kwa masharti magumu magumu wanayowekeana wao kwa wao na masharti hayo yanawagharimu/yanawadhuru hata wao wenyewe kwahiyo siyo rahisi kama mnavyodhani.

twende kwa mfano wa muvi tu mtu anataka mali fulani imefungiwa sehemu anaambiwa ramani ya kufika huko anayo fulani na fulani yupo nchi za mbali huko kisha ramani inaonesha kuna sehemu ukifika utakuta vizuizi fulani lets say wanyama wakali inabidi uende na kitu fulani kisha kuna walinzi kadhaa mbele itabidi uende na kitambulisho fulani ndo wakupokee maana yake inabidi ukakipate hiko nacho... mbele huko inabidi uwe na almasi ya kukatia kufuli nk. kwahiyo unakuta mission inahitaji pesa nyingi sana, nguvu za mwili, watu wengi na muhimu, akili nyingi, muda mwingi wa kutosha nk.

kwahiyo mtu akisema nipe jina la mama yako nikuroge ukimwambia alitafute mwenyewe maana yake unampa mission ndani ya mission. au wale wanaosema kwanini mchawi asiweze kujua na kukwapua fedha benki, kwanini asiweze kusafiri popote atakapo na kadhalika hawajui kwamba yote hayo yanagharimu? unakuta jambo lingine unaambiwa kulifanikisha itakubidi utumie miaka 20 sasa wakati huo wewe una 45 ndo unakuta mtu anakata tamaa maana hilo ni moja tu wakati inatakiwa likamilike hilo ndo likamilishe na mengine kama manne mbele
 
Shetani hajawai kuwepo, hizo ni story kama story nyingine tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…