Ataweza kuishi Moshi kwa salary ya laki 8?

mkuu Extro, unamwelekeza tena kwenye uasherati, na wakati anatakiwa abane matumizi ipasavyo kwa ajili ya kuweka msingi bora wa maisha yake? Sio vzr kuanza kwa anasa maana kuna mambo yako mbele yake kama: ujenzi wa nyumba, ndoa, kuwakumbuka wazazi, kuweka akiba, nk

Njoro imerithi jina baya tu, kwa sasa iko vizuri. Zamani ndio ilikuwa ya kihuni.
Kwahio sahizi unataka kuniambia ushenzi wa kuibiana hamna njoro?

Labda kama ni mlokole wa kweli ila starehe ni sehemu ya maisha mkuu. Maendeleo tufanye ila tusisahau kuishi. Moshi mji mzuri sana hakika.
 
Moshi hata watokao Dar watumiaji hela huushangaa huo mji maana kwenye matumizi ya Pesa naweza kufananisha na VVT-i. Hela kidogo starehe nyingi ila Dar huku ni V8 hela mlima starehe kiduchu.

Ukiwa na laki tu starehe unayokula Moshi kwa Dar haPa labda uwe na mara mbili ya hela.
 
Kwani moshi bei ya bia ni tofauti na Dar?
 
Kwahio sahizi unataka kuniambia ushenzi wa kuibiana hamna njoro?

Labda kama ni mlokole wa kweli ila starehe ni sehemu ya maisha mkuu. Maendeleo tufanye ila tusisahau kuishi. Moshi mji mzuri sana hakika.
Boss, Njoro ime"change". Uhalifu bado upo kama sehemu nyingine tu za uswahilini.

Extro kwa umri wangu kujidanganya nafsi yangu siwezi. Starehe zipo ila huwa zina majuto mbele. Mimi sasahivi starehe yangu ni kusoma Biblia., Nilipoteza muda na rasilimali nyingi/mwingi sana kwenye anasa. Sitamani mwingine apitie humo maana najuta. Furaha ya kweli ni uzao wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu.

"Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili . Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili ..." Soma WAGALATIA 5:16-25.

YESU NI KRISTO
 
Milele amina mkuu!
 
Moshi hata watokao Dar watumiaji hela huushangaa huo mji maana kwenye matumizi ya Pesa naweza kufananisha na VVT-i. Hela kidogo starehe nyingi ila Dar huku ni V8 hela mlima starehe kiduchu.

Ukiwa na laki tu starehe unayokula Moshi kwa Dar haPa labda uwe na mara mbili ya hela.
Mkuu nipe elimu ya VVT-i na V8 hizo ulizozitaja kwenye gari humaanisha nini
 
Kuna jamaa yangu kapata kazi huko Moshi mkoani Kilimanjaro, salary ni laki 8 baada ya makato yote.
Je ataweza kuishi hapo Moshi kwa huo mshahara, maana anasita kwenda kumwaga wino?
Mwambie aache umama, mi nilipata kazi Arusha mshahara laki nne, kipindi hicho na nikasurvive # kupanga ni kuchagua

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Moshi hata watokao Dar watumiaji hela huushangaa huo mji maana kwenye matumizi ya Pesa naweza kufananisha na VVT-i. Hela kidogo starehe nyingi ila Dar huku ni V8 hela mlima starehe kiduchu.

Ukiwa na laki tu starehe unayokula Moshi kwa Dar haPa labda uwe na mara mbili ya hela.
Kuna Mzaramo alienda kusoma chuo Moshi...anakuambia ukiacha kwao Bagamoyo...sehemu nyingine anayoikubali ni Moshi.
 
Mkuu nipe elimu ya VVT-i na V8 hizo ulizozitaja kwenye gari humaanisha nini
Vvti ni mfumo wa uchomaji wa mafuta kwa kuzingatia throttle response ya mwendeshaji yani
pressure ya mguu unapokanyaga accelerator. Variable valve timing with intelligence ndio kirefu chake.

Ukikanyaga kwa nguvu basi engine control unit valve zaidi na kuruhusu mafuta na hewa nyingi zaidi kuchomwa ili kuzalisha nguvu na mwendo zaidi. Ukikanyaga kwa taratibu vivyo hivyo na valve zitafunguka kidogo ili kusababisha more fuel efficiency.

Tofauti na carburetted engines ambavyo zilikuwa zinasukuma mafuta kama bomba tu na valve zinafunguka na kufunga kwa kipimo constant as long as gari linawaka, linatembea kiwango cha mafuta ni constant. Hii ilipelekea mafuta mengi kupotea na gari kutokuwa na ufanisi maana mda unapohitaji nguvu gari kama kwenye vilima inakula wese, usipohitaji nguvu sana pia gari inakula wese.

V8 ni mpangilio wa Cylinder na piston kwenye block kushoto na kulia zikiwa zimekaa 4 kushoto na 4 kulia kiubavu. Zimetengeneza muonekano wa umbile V. Hii engine iko kwenye Land Cruiser za viongozi kwa jina common VX V8 (vieite) ila ubaya ni kuwa ulaji wake ni mkubwa sana wa mafuta sababu ni engine kubwa sana.
 
Back
Top Bottom