Vvti ni mfumo wa uchomaji wa mafuta kwa kuzingatia throttle response ya mwendeshaji yani
pressure ya mguu unapokanyaga accelerator. Variable valve timing with intelligence ndio kirefu chake.
Ukikanyaga kwa nguvu basi engine control unit valve zaidi na kuruhusu mafuta na hewa nyingi zaidi kuchomwa ili kuzalisha nguvu na mwendo zaidi. Ukikanyaga kwa taratibu vivyo hivyo na valve zitafunguka kidogo ili kusababisha more fuel efficiency.
Tofauti na carburetted engines ambavyo zilikuwa zinasukuma mafuta kama bomba tu na valve zinafunguka na kufunga kwa kipimo constant as long as gari linawaka, linatembea kiwango cha mafuta ni constant. Hii ilipelekea mafuta mengi kupotea na gari kutokuwa na ufanisi maana mda unapohitaji nguvu gari kama kwenye vilima inakula wese, usipohitaji nguvu sana pia gari inakula wese.
V8 ni mpangilio wa Cylinder na piston kwenye block kushoto na kulia zikiwa zimekaa 4 kushoto na 4 kulia kiubavu. Zimetengeneza muonekano wa umbile V. Hii engine iko kwenye Land Cruiser za viongozi kwa jina common VX V8 (vieite) ila ubaya ni kuwa ulaji wake ni mkubwa sana wa mafuta sababu ni engine kubwa sana.