Athanas Myonga aibuka Mshindi wa kwanza wa Shindano la Stories of Change 2023

Athanas Myonga aibuka Mshindi wa kwanza wa Shindano la Stories of Change 2023

Alafu wote Wakristo hakuna muumiani hata mmoja liyeshinda nyie vitu kama hivyo hamuwezi andika. Mnachojua ni kuandika threads za kuuponda Ukristo πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜πŸ˜†πŸ˜… au mods ni wadini wamependelea upande wa pili.
Udini tena mgalatia? Sisi tuna Rais na mawaziri kibao 🀣
 
Hongereni sana team ya JF kwa kuendesha shindano na hatimaye kuibuka na washindi ambao mabandiko yao/mada walizoandika zitaleta chachu ya mabadiliko kwenye jamii baada ya kusomwa, kuchambuliwa na kufanyiwa kazi na wawakilishi wa serikali na hatimaye kumgusa mwananchi mmoja mmoja pale alipo.

Mfano bandiko kuhusu ukusanyaji wa kodi, kwenye upande wa mrengo chanya serikali ikifanikiwa kukusanya kodi kutokana na uwiano wa mapato (GDP) na ikatumika ipasavyo kuleta maendeleo kwa jamii haswa kuwaua maadau wakuu watatu (Umasikini, Ujinga na Elimu) na ndugu zake walioongezeka; kila mwananchi atanufaika na maendeleo yatayofanyika (uboreshwaji katika sekta ya elimu utaofua maarifa ya wananchi kujitengenezea namna ya kujimudu kimaisha badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini na mashirika makubwa, sekta ya afya, upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote, kukuza uchumi haswa ujengwaji wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa, kuboresha na kukuza mifumo ya teknolojia kuendana na kasi ya dunia n.k.).

Pia, mada zote zilizoshinda hata ambazo hazijashinda, sio tuu ziachwe kufanyiwa kazi na serikali pekee la hasha, bali hata sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kifaida na mtu mmoja mmoja kwa namna yake anaweza akaona fursa ambayo anaweza ifanyia kazi na kuweza kumkwamua kiuchumi.
Kuna msemo unasema akili ni mtu, na mwingine unasema watu hufa na utajiri wao, maana kila mmoja huwa ananamna yake ya kutafakuri na kuchambua jambo na kuleta suluhisho kwake binafsi, kwa familia na jamii kwa ujumla.

Ingekuwaje watu wengi wangekufa na mawazo yao ambayo yameleta maendeleo makubwa kwa jamii bila kuyaweka wazi mawazo hayo aidha wakayafanyia kazi wao au wengine wakayaboresha na kuyafanyia kazi...πŸ€”

Oohoooo nimeanza kuandika mada badala ya kuchangia mada 😁, my bad.

Hongereni sana bodi ya wakurugenzi, waanzilishi wenzake na Bw. Max, mgeni rasmi, mabalozi na wote waliowezesha na kusherehesha shughuli nzima.

Mwisho wa yote, hongereni sana wafanyakazi wote wa JF kwa ujumla kwa kujitoa na kujituma kwenu kazi yenu imeonekana na binafsi nimetambua huduma yenu. Naamini nje ya mshahara kuna bahasha zinawajia kutoka kwa Bosi, kama hakuwa amewaza hili basi akisoma hili wazo anaweza akafanya kitu 😊.

Shukrani kubwa zifike kwa Muanzilishi wa JF Mr. Maxence (always humble), kongole nyingi kwako na πŸ’ maua yako teleee 😊.

Wasalaaam, Bi. Kasinde πŸ™‚.
 
hopeless ukiambiwa utoe ushahidi utaweza? acha wivu na chuki kwa washindi na huu mtandao wa jamiiforums sawa? halafu unaonekana una stress sana na maisha magumu kwani muda mwingi nakuona ni mtu mwenye makasiriko mengi na una wivu usio na sababu kwa members maarufu hapa JamiiForums. badilika kwani unaboa sawa?
Usikimbilie kusema ni wivu, mimi niliwahi kuweka Post humu JF of GT's nikishauri iboreshwe ili irudi kwenye hali ya awali, Post ilikaa kwa muda mfupi wakaiondoa kisa Mods wa JF hawataki na hawapendi ushauri. Pia Mods huchagua Post za akinanani zikae za nani ziunganishwe na nyingine japo hazina uhusiano! Na wakati mwingine kuhariri kinyume na lengo la ujumbe wa mwandishi, hii imenitokea mara kadhaa, kuna Post kichwa nilikiandika kwa kiingereza wao wakahariri na kupoteza lengo na maana.
 
Sasa mbona hamjashinda na bado hata kwenye matokeo ya Primary na Secondary school shule za kiislam zinaburuta mkia?
Ndio akili yako unafikria udini tu🀣🀣Mbona tupo sana tu kweny vitengo na nfasi za juu kama Raisi na waziri mkuu.

Matajiri wakubwa hapa bongo.
 
πŸ˜€πŸ˜€
Pole sana mkuu. Inaonekana unasumbuliwa na vitu na mambo madogo.
Nimeshakuambia sipo chini ya mtu yeyote.
Wapo waandishi nguli ndio lakini hiyo haiondoi nafasi yangu. Na hakuna yeyote anayeweza kuishika wala kuziba nafasi yangu.

IlΓ  wapo Watu kama wewe ambao mpo chini yangu ambao mnatamani ningekuwa kama ninyi
Huwezi kushinda unaandika porojo...Sina mda wa kutafuta umaarufu ni ushamba .

Sijatokea kijijini so sipendi umaarufu.
 
Kutokea kijijini hakumfanyi mtu kuwa mshamba.
Hapa DSM tuu asilimia 90 ya wakazi wake wenyewe ni washamba ikiwemo wewe mwenyewe kwa kuwa namtazamo wa kishamba kama huo uliosema kuwa mtu kutokea kijijini kunamfanya awe mshamba.

Pili, kitendo cha kumfuatilia mtu ambaye anafanya jambo ambalo hulipendi ni kiashiria tosha kuwa wewe ni mshamba na hujitambui.

Tatu, Ikiwa wewe haupendi umaarufu au jambo fulani hiyo haimaanishi wengine nao wasilipende, kama mtu havunji sheria yoyote.
Ni kiashiria cha ushamba.

Mwisho, usiwe na wivu kwa Watu ambao huwezi kuwafikia kwa kile unachowaonea wivu
Kelele kibao ,punguza sifa .!!
 
Kazi nzuri sana hongereni team nzima ya jamii forum, hongereni washiriki wote na zaidi washindi wote hata mlioshiriki na hamkushinda bado ni washindi tunathamini muda wenu na maono yenu.....

Hivi hafla kama hizo members tunaalikwa? kama ndio kwa utaratibu upi? (Najua sitajibiwa)
 
Back
Top Bottom