Athari za Mfumo wa Kichama kwa Idara za Usalama na Ulinzi Kabla na Baada ya Uhuru

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Kutoana na kutoka ukoloni mpaka kuwa watawala kuna utofauti kati ya idara za usalama na ulinzi kabla na baada ya uhuru, hasa katika muktadha wa Afrika na mataifa mengine yaliyojitawala kutoka kwa wakoloni.

Kabla ya uhuru, idara za usalama na ulinzi mara nyingi zilikuwa zikitumika kama vyombo vya kulinda maslahi ya wakoloni badala ya raia. Mara nyingi ziliongozwa na sera zilizokuwa na mwelekeo wa kuzuia harakati za ukombozi na uhuru wa kisiasa. Wakati wa harakati za kupigania uhuru, vyama vya kisiasa vilianzisha vikundi vyao vya ulinzi ambavyo viliweza kuwa na mvuto mkubwa katika mwelekeo wa taasisi hizo baada ya uhuru.

Baada ya uhuru, nchi nyingi zilihamia kwenye mfumo wa vyama vya siasa vinavyotawala kwa muda mrefu, na mara nyingi idara za usalama na ulinzi zilikuwa na uhusiano wa karibu na chama tawala. Hii ilisababisha changamoto kadhaa, kama vile:

  1. Upendeleo wa kisiasa – Idara za usalama na ulinzi zilianza kuwa vyombo vya kulinda chama tawala badala ya kulinda raia wote kwa usawa.
  2. Kukandamiza upinzani – Vyombo vya usalama vilitumika kudhibiti upinzani wa kisiasa badala ya kutekeleza haki na sheria kwa usawa.
  3. Kutokuwa na uhuru wa taasisi – Badala ya kuwa taasisi huru zinazoongozwa na katiba na sheria, mara nyingi idara hizi zilikuwa zinafuata matakwa ya wanasiasa.
Nchi nyingi za Afrika na zisizo kuwa za Afrika bado zinapitia hii haya.
 
Hii inatutafuna Hadi keshokutwa,huwezi amin ni rahisi kuingia kwenye mfumo ukiwa na mapenzi na chama kuliko ukidhihilisha kuipenda nchi, kwenye chama mahaba makubwa na nchi ni mwiko na unapaswa kuepukwa
 
Kweli kabisa kuna RPC mmoja alitamkia kuwa hawezi kuona wapunzani wananyanyasa chama tawala.....lazima watasaidia tuu....alisema live namsikiaaa
 
Kutoana na kutoka ukoloni mpaka kuwa watawala kuna utofauti kati ya idara za usalama na ulinzi kabla na baada ya uhuru, hasa katika muktadha wa Afrika na mataifa mengine yaliyojitawala kutoka kwa wakoloni.

Kabla ya uhuru, idara za usalama na ulinzi mara nyingi zilikuwa zikitumika kama vyombo vya kulinda maslahi ya wakoloni badala ya raia. Mara nyingi ziliongozwa na sera zilizokuwa na mwelekeo wa kuzuia harakati za ukombozi na uhuru wa kisiasa. Wakati wa harakati za kupigania uhuru, vyama vya kisiasa vilianzisha vikundi vyao vya ulinzi ambavyo viliweza kuwa na mvuto mkubwa katika mwelekeo wa taasisi hizo baada ya uhuru.

Baada ya uhuru, nchi nyingi zilihamia kwenye mfumo wa vyama vya siasa vinavyotawala kwa muda mrefu, na mara nyingi idara za usalama na ulinzi zilikuwa na uhusiano wa karibu na chama tawala. Hii ilisababisha changamoto kadhaa, kama vile:

  1. Upendeleo wa kisiasa – Idara za usalama na ulinzi zilianza kuwa vyombo vya kulinda chama tawala badala ya kulinda raia wote kwa usawa.
  2. Kukandamiza upinzani – Vyombo vya usalama vilitumika kudhibiti upinzani wa kisiasa badala ya kutekeleza haki na sheria kwa usawa.
  3. Kutokuwa na uhuru wa taasisi – Badala ya kuwa taasisi huru zinazoongozwa na katiba na sheria, mara nyingi idara hizi zilikuwa zinafuata matakwa ya wanasiasa.
Nchi nyingi za Afrika na zisizo kuwa za Afrika bado zinapitia hii haya.

Ni lazima wabadilishe Mifumo yao yote kabisa, ikiwemo na kubadilisha utaratibu Wao wa RECRUITMENT ya Maafisa wao.

Hili ni jambo la lazima kabisa ambalo haliwezi kuepukika kwa Sasa katika Idara hiyo.
Ni Lazima Wabadilike ili kuendana na Mahitaji halisi ya Dunia ya dunia ya Sasa.

Mamlaka Kuu ya Ujasusi ya Marekani ya CIA Baada ya Mashambulizi makali Sana ya kigaidi yaliyofanyika katika Kituo Kikuu Cha Biashara Cha Dunia (WTC), Pentagon, n.k hapo tarehe 11 Septemba 2001, CIA walikiri kwamba kulikuwa na Mapungufu makubwa Sana kwenye Mifumo ya Utawala, Mifumo ya Kuajiri Maafisa wa Taasisi hiyo na kwenye Mifumo ya Kiutendaji ndani ya CIA hali ambayo ilisaidia Sana kutoa mwanya kwa Magaidi wa Al Qaeda chini ya Osama bin Laden kuweza kuishambulia Marekani kwa urahisi Sana.

Baada ya mashambulizi hayo ya kigaidi ya September Eleven, CIA ilifumuliwa na kisha kusukwa tena upya. Kwa sasa, Maafisa wa Idara hiyo ya CIA Wanaajiriwa kwa utaratibu wa kutoa Matangazo ya Ajira zao kwenye vyombo mbalimbali vya Habari. Hii inawasaidia kutoa wigo mpana zaidi wa kuwapata Watu/ Waajiriwa mbalimbali walio sahihi zaidi, wenye weredi katika fani tofaufi tofaufi wakiwa na mitazamo tofaufi tofauti kinyume na hali ilivyokuwa hapo awali kabla ya mashambulizi ya 'September Eleven.'
 
Hii inatutafuna Hadi keshokutwa,huwezi amin ni rahisi kuingia kwenye mfumo ukiwa na mapenzi na chama kuliko ukidhihilisha kuipenda nchi, kwenye chama mahaba makubwa na nchi ni mwiko na unapaswa kuepukwa
Changamoto sana
 
Back
Top Bottom