Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

jina lenyewe PENGO so lazima kuna akili za Pinda ma CCM
 
Kulikoni Gwajima na Matusi ya nguoni kwa Pengo?

Hivi karibuni Mchungaji Gwajima amemvurumishia matusi ya nguoni askofu Pengo kutokana na kutoa msimamo wake binafsi kuhusu kupiga kura ya Hapana kwa Katiba iliyopendekezwa

Hii inamaana gani, Je ni kuwa ushirikiano kati ya Makanisa dhidi ya Uislam umeingia dosari? maana pia kuna Makanisa mengine yamemkosoa Pengo kwa msimamo wake huo japokuwa si kwa Matusi ya nguoni
 
Hutakiwa kimtetea mpuuuzi,mnufaikaji wa peza za escrow pengo. unatakiwa kua zezeta kumtetea pengo,sitaki kuamini kama wewe pia uko hivyo.


Jifunze lugha za watu.

Teh teh teh. Profile picture yako inadhihirisha waziwazi akili yako ilikoegemea!
 
Hutakiwa kimtetea mpuuuzi,mnufaikaji wa peza za escrow pengo. unatakiwa kua zezeta kumtetea pengo,sitaki kuamini kama wewe pia uko hivyo.


Jifunze lugha za watu.

Hapo kwenye nyekundu. Ukiwa kwenye nyumba ya vioo. Usiwarushie wenzako mawe. Jifunze lugha yako kwanza.
 
Hao maaskofu wa TEC kuna muumini gani aliwahi kuwapigia kura kuwachagua hao maaskofu au kuwachagua kuwa wawakilishe kwenye hilo baraza la maaskofu? Representative Democracy inataka uchaguliwe na hao unaowawakilisha.

Hao maaskofu wa TEC hawajawahi chaguliwa na muumini yeyote wa kikatoliki kuwa awawawakilishe kwenye hilo baraza la maaskofu.Wako pale wakijiwakilisha wenyewe na nafsi zao ndio maana lile tamko halikuzingatia matakwa ya waumini ya kupiga kura kwa hiari kidemokrasia.

Tamko lao ni lao kama kikundi cha watawala wachache wa kanisani wakiwakilisha maoni yao wanavyofikiri kwenye kikao chao ambacho hawajatumwa na muumini yeyote Kwani hajawachagua wala kuwatuma wakaandike hilo tamko.

Pengo alifanya utafiti akaona kuwa watu wanahitaji uhuru katika upigaji kura ndio akatoa tamko hao wengine walikurupuka tu kwa mihemko ya ushabiki wa kisiasa badala ya kutafiti kwanza.


AISEE WEWE JAMAA KUMBE NI KILAZA!!
Hebu mwambie aliyekutuma akufundishe na vya kuandika basi ili uwe logic kidogo mana unaandika utumbo na utaahira mtupu humu ndani. Yani unataka na viongozi wa dini wanaowakilisha makanisa yote katika Baraza la Maaskofu nao uwapigie kura? HIZO NI AKILI ZA MILEMBE

Utaratibu uko vizuri kwani kila kanisa lina maaskofu wake ambao kimsingi ndio walezi wakuu wa makanisa au madhehebu nchini sasa kwa makubaliao yao ambayo yapo kikatiba na waliyoridhia juu ya namna ya kupata uwakilishi wa kila kundi la kikristo ndani ya Baraza.

ILA Kwa hoja yako hiyo ya kipuuzi wewe unaweza kumwambia hata Mungu angekupa nafasi ya kumpigia kura baba na mama yako waliokuzaa.

Na, ikumbukwe hakuna utafiti alioufanya Pengo ila aliongea MAHABA yake na CHAMA CHA MAPINDUZI. Na kwa taarifa yako kama ulikua hujui au aliyekutuma hajakuambia, Pengo ndiye aliyekua mtu wa kwanza kudandia hoja ya Katiba Mpya na kusema kuwa Muungano upo na anatambua serikali mbili ila Askofu Paul Ruzoka alimuumbua kuwa hakuna serikali mbili ni uongo.

Kwahiyo mahaba ya Pengo na CCM ndio yanayomfanyaga awe anakurupuka siku zote..... ACHANA KABISA NA KUMTETEA MSALITI HUYU KADA WA CHAMA CHA MAPINDZUI ALIYEJIVIKA VAZI LA DINI.

#Kumbuka mabomu ya Arusha pale kanisani huyu huyu Pengo ndiye alikuwa wa kwanza kusema kuwa aliyerusha bomu ni mkristo, sasa atuambie hayo yote nayo alifanya uchunguzi gani? PENGO TUNAMFAHAMU VYEMA ANAPENDA KULAMBA MIGUU YA WATAWALA.

Ukweli lazima usemwe hata kama utamuumiza na nyie aliowatuma mwambieni awaambie ukweli sio kuja hapa hamjui chochote..

PENGO MSALITI TU, HAKUNA NAMNA NI MSALITI NA MNAFIKI KATIKA HILI.
 
kwenye kusema ukweli ndio unamuita mtu mzima mjinga, mpuuzi, hana akili, kalogwa! uhuru wa maoni unaishia pale unapoingilia haki ya mwenzako. kila mtu ana haki ya kuheshimiwa na kutunza dignity yake. huyo gwajima kwa kutoa maneno ya dhihaka kapoteza diginity yake na ya mwenzake.

kuhusu suala la CAG kutaka kujengewea msikiti ni upuuzi na kama unamfuata gwajima i feel sorry for you. mwislam unahitaji mswala tu, msikiti wa kazi gani kwani CAG kazi yake ni kuswalisha jamaa'. kivuli cha simu yako ni kirefu kuliko uwezo wako wa kufikiri, please usiwaaibishe wazazi wako kwa kulea kilaza
 
"angebalance kidogo kwa kuionya pia serikali kuwachagulia maoni wananchi" kwa nini usingeingia kwenye kichwa chake ili atoe maoni kama unavyofikiria!? ni mawazo yake punguza munkar
 
Sio wote wasikiao sikio la kufa,nashangaa kama kweli mchungaji wa watu anaweza kutoa matosi kama haya kwa mchungaji mwenzie,kama amekosea si anakwenda kumsahihisha tu,wanaochungwa na gwajima angalie msije kuingia kwenye moto wa milele kwa kumfuata mpumbavu wenu Gwajima
 
Kweli nimeamini humu ndani kuna watu matusi kwao ni sehemu ya chakula. Hivi unaweza kuunga mkono hayo aliyosema ngwajima? hata kama asingekuwa ni kiongozi wa dini, kwa mtu wa kawaida tu utagundua kwamba si mtu mwenye busara/hekima/ maadili hata kidogo. Mimi nimeshindwa kumwelewa kama ailpata ukichaa wa muda ama vipi, manake hayo maneno ni ya kuhuni kabisa, sijui anaimba taarabu eti ni kiongozi wa dini na kuna watu hapa wanamsifu kwa nguvu zao zote!!!? Kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
Inasikitisha sana..Wanasema hayo matusi ya Gwajima amepewa na Roho Mtakatifu
 
Mahaba yako kwa Pengo yatakuua, wewe unadhani kushabikia hiyo kura ya Ndiyo ndo sahihi? Utashinikiza kukubali kitu ambacho wananchi hawajakisoma na kutafakar? Wangapi kijijini kwenu wana nakala ya Katiba pendekezwa?

Umeelewa alichokizungumzia Pengo au ndo ushabiki mandazi...
 
gwajima huyu anayepora wake za watu? ni mtu wa kumuamini kweli...Muadhama Policarp Kadinali Pengo hawezi kumjibu kwani huwa hapendi malumbano. na Gwajima anachotafuta hapo ni ili aje amilikishwe TP
This is too much..
 
Je maneno mpuuzi,mjinga,mpumbavu,mlevi ni matusi ya nguo au maneno ya sifa ?
Mpumbavu ni asiyeamini Mungu
{ZABURI 14:1-2
 
Nimesikiliza kwa makini maelezo ya Pengo kuhusu azimio la baraza la maaskofu wa kanisa katoliki na nikiri tu kwamba Pengo kwenye hili AMEKURUPUKA!

Ni jambo la kushangaza kumuona mzee mzima anazuia wahumini wake kufanya jambo jema kwa maslahi ya taifa lao na vizazi vijavyo kwa hoja ya "uhuru wa kuamu!" au kwa kingereza "free will".

Kama ni hivyo, kwanini huko makanisani wachungaji utusii kudhibiti nafsi zetu dhidi ya maovu, kwanini tunaonywa kuacha kufanya dhambi? kwanini wasituache tu tufanye tupendalo, after all sisi ni watu wazima! Kwanini linapokuja suala la kutenda jambo jema kwa taifa ndio inapozuka hoja ya "watu waachwe waamue wao wenyewe?"

Pia kuhusu kauli ya Gwajima, kwa hoja yupo sahihi kabisa ingawa ametumia nguvu kubwa zaidi kuifikisha. Ila nampa hongera mchungaji Gwajima (ingawa mimi sio fun wake) kwa kuwa muwazi katika hili na kumchana mnafiki Pengo.

Pengo, it time to go away!
 
Back
Top Bottom