USALITI ALIOUFANYA PENGO HAUVUMILIKI.
Nilishasema tangia awali ya kuwa Pengo amekosa na tena amekosa sana sana. Yawezekana mtu mwingine wa kawaida na mdandia mada ambaye umeona tu au kusikia audio clip za viongozi hawa wawili ukasema Pengo ametukanwa. LA HASHA AMEPATA ALICHOKUA ANAKITAFUTA.
Dawa ya MSALITI na MTU MNAFIKI duniani kote ni kuambiwa ukweli wake hadharani tena mbele ya kadamnasi, na kwakua aliongea hadharani yeye mwenyewe Pengo ndio alikua wa kwanza kuvunja utaratibu kama mmoja wa viongozi na wajumbe wa Baraza la Maaskofu Tanzania.
Hakuna namna, PENGO NI MSALITI na ni MNAFIKI...
Pengo anasema...."NIMEKUBALIANA NA BARAZA LA MAASKOFU TAMKO LISOMWE KWENYE MAKANISA, NA PIA KWENYE MAKANISA YOTE YA JIMBO LA DAR ES SALAAM" Swali ni kwamba kama alikubaliana na hayo kwanini tena aseme kuwa ILA MIMI BINAFSI NAONA HIVI NA VILE wakati yalishapita maazimio ya pamoja ambayo naye aliyakubali?
Pili, Hoja yake binafsi ilitakiwa iwasilishwe kwa utaratibu kwa kuipeleka mbele ya Baraza la Maaskofu ili kuonyesha kutoridhika kwake na sio kuitisha vyombo vya habari na kuongea kama alivyofanya hukuakijua nafasi yake ni ipi katika jamii.
Tatu, Pengo ni lazima aambiwe hadharani na alichoambiwa na Askofu Gwajima kwanza ni kidogo kutokaa na namna ambavyo ameutangazia umma wa Watanzania ya kuwa HAKUNA KITU KINAITWA UMOJA BAINA YA WAKRISTO WA TANZANIA ila kila mtu anafuata matakwa yake mwenyewe huku ikumbukwe ya kuwa Pengo huyuhuyu ndiye aliyekuwa miongoni mwa waasisi wa awali kabisa wa Baraza hili la Maaskofu Tanzania.
Tatu, je baada ya Pengo kusema aliyoyasema amewaweka katika hali gani maaskofu wengine wote waliokubaliana na kuweka saini katika TAMKO lile? Wameonekana kana kwamba ni viongozi wanaotaka kuligawa taifa kwahiyo kwa mtu mmoja PENGO amewafanya wenzake kuwa sio kitu mbele ya jamii.
Bado, unasema huyu jamaa Pengo hajafanya makosa? PENGO ni msaliti na wasaliti wote hufa au kupotea ghafla kwa mawazo kutokana na usaliti wao. Njia ya wasaliti haijawahi kuwa ya mafanikio hata siku moja..
#PENGO THE TRAITOR