Katika hayo majukumu aliyonayo, ndiyo maana hakuweza kudiriki kukaa kimya pindi alipoona misingi ya kanisa inataka kupotoshwa au kupindishwa. Yeye kama mshauri wa Pope, yeye kama mjumbe wa Kanisa Katoliki Tanzania katika vikao vya Vatican, yeye kama candidate wa upope hawezi kukaa kimya pindi anapoona Kanisa linakanyaga misingi yake. Na ndio maana kwenye michango yangu nimesema, Pengo ameongea kufuatana na majukumu anayopewa na Canon Law. Lakini pia katika baadhi ya michango yangu ukisoma page namba mbili nadhani kuna sehemu nimesema wazi kwamba Pengo hayupo juu ya TEC na ndio maana hakuwa na mamlaka ya kuzuia waraka usisomwe makanisani hasa katika jimbo kuu la Dar es salaam analoliongoza. Lakini kutokuwa na madaraka hayo, hakumyimi uhuru wa yeye kama Kardinali kuwakumbusha waumini na wachungaji wa Kanisa misingi ya Kanisa Katoliki. Mimi sioni kosa la Kardinali Pengo, labda uniambie kwamba alipaswa kwanza kwenda kwa Pope akamueleze hili jambo halafu ndio Pope atoe muongozo, kitu ambacho sidhani kama kinahitaji tufike huko.