Hakuna aliyenidanganya, na ninafahamu kuwa yupo chini ya TEC, lakini ukisoma Canon Laws utapata picha ya kwa nini nimesema ni mkuu.
Kuwa mkuu haimaanishi kuwa na mamlaka juu ya TEC, waweza kuwa mkuu kiheshima lakini si kimaamuzi ndiyo maana Mwadhama Kardinali Pengo hakuwa na mamlaka ya kuzuia waraka huo usisomwe makanisani licha ya kuwa aliona una mapungufu ndani yake.
Na ieleweke wazi, katika kikao kilichotoa waraka huo Pengo hakuwepo, alikuwa India kwenye matibabu, pengine angekuwepo kwa influence aliyonayo, na heshima aliyonayo ndani ya Maaskofu angeweza kutoa hoja zake na wakamuelewa.
Tukiacha hayo, hata kama Pengo kakosea, bado si sahihi kwa mtu anayejiita kiongozi wa dini kumtukana mtu tena akiwa madhabahuni.
Si sahihi hata kidogo na wala biblia haisemi hivyo. Alichokifanya Gwajima ni kinyume kabisa na maadili ya kichungaji. Kama ana hoja za kupingana na Pengo alipaswa azitoe kwa njia iliyo sahihi na si kwa kutukana.